Tafuta

2022.09.03 Kesha la sala lilioongozwa na Kardinali Angelo De Donatis katika fursa ya kutangaza kwa Papa Yohane Paulo I kuwa Mwenyeheri. 2022.09.03 Kesha la sala lilioongozwa na Kardinali Angelo De Donatis katika fursa ya kutangaza kwa Papa Yohane Paulo I kuwa Mwenyeheri. 

Kesha la maandalizi ya kutangazwa mwenyeheri Papa Yohane Paulo I

Katika kesha kwa ajili ya kutangazwa Papa Yohane Paulo I kuwa Mwenyeheri,katika Kanisa Kuu la Mtakati Yohane huko Laterano,Jumamosi 3 Agosti,miongoni mwa waliokuwepo pia waamini kutoka Belluno Feltre,Vittorio Veneto na Venezia pamoja na maaskofu na mapadre.Katika mahubiri yake,Kadinali De Donatis Makamu wa Papa alisisitiza unyenyekevu kama njia kuu ya maisha yake.Katika shuhuda walionesha urahisi wa maisha na dhamana yake ya kudumu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Badhi ya maneno ambayo Papa Yohane Paulo wa I alitamka, akiwahutubia Waroma, mnamo tarehe 23 Septemba 1978, katika mahubiri ya maadhimisho ya kusimikwa rasmi katika Kanisa Kuu la Kirumi la Mtakatifu Yohane huko Lateranoalisema:“Ninaweza kuwahakikishia kwamba ninawapenda na  ninatamani kuingia tu kwenye huduma yenu na kufanya nguvu zangu dhaifu zipatikane kwa wote, kile kidogo nilicho nacho na kile ambacho nilicho”.  Sauti yake ya wakati ule  bado ilisikika katika Kanisa hilo wakati wa mkesha wa maombi usiku wa kuamkia Dominika tarehe 4 Septemba, ulioongozwa na Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa kwa kushirikiana na  maaskofu wasaidizi wa jimbo la Roma. Akikumbuka kile ambacho shemasi wa Kirumi Lorenzo alisema, katika tukio hilo, Papa Luciani alithibitisha, kwamba kati ya mambo mengine, “maskini ni hazina ya kweli ya Kanisa”, huku akifikiria watu wengi wanaohitaji katika mji mkuu Roma. Moyo wa mkesha huo ulikuwa ni kusikiliza Neno la Mungu.

Masomo yaliyochaguliwa wakati wa sala iliyotangulia Misa ya kumtangaza Papa Luciani  kuwa Mwenyeheri  kuwa yalikuwa ni sawa na yale ya madhimisho la tarehe 23 Septemba 1978. Somo la kwanza lilitolewa katika kitabu cha nabii Isaya 60, 1-6; la pili kutoka katik Barua kwa Waebrania 13, 7-8. 15-17. 20-21; kifungu cha Injili kilitoka kwa mwinjili Mathayo 28, 16-20, ambapo Yesu aliwaahidi wafuasi wake kwamba: “Tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.  Kila usomaji ulifuatiwa na sauti ya ufafanuzi wa maneno kutoka kwa Papa Yohane Paulo I, kwenye kurasa hizo za Maandiko, yaliyohifadhiwa katika Pango Hifadhi la Vatican, huku picha za Papa wa tabasamu zikipita kwenye skrini kubwa, zikonesha picha na vipende vidogo vidogo vya video vikionesha  ziara yake katika Kanisa mama la Jimbo la Roma.

Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano  kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I
Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I

Baada ya kila usomaji na ufafanuzi, ushuhuda ulifuatwa na muda mwingine  wa ukimya.  Walitoa ushuhuda niLina Petri, mhusika wa Mfuko wa Vatican wa Yohane Paulo 1, na ambaye ni mpwa wa Papa Luciani; Sista Margherita Marin, wa shirika la  Maria Bambina, aliyekuwa katika huduma yake katika muda mfupi wa Upapa wake; na Padre Juan José Dabusti, padre wa jimbo kuu la Buenos Aires nchini Argentina ambaye alifanya kujulisha muujiza kwa maombezi ya Papa Yohane Paulo I kwa ajili ya Candela Giarda kijana aliyekuwa na umri wa miaka 11 wakati huo akisumbuliwa na kifafa kibaya. Hao ndio waliosimulia kwa hisia za kumbukumbu kali zaidi zilizounganishwa na Papa Luciani kwa  maneno ya mwisho, salamu ya mwisho iliyopokelewa, na mafundisho muhimu zaidi yalibaki moyoni na kubebwa katika kumbukumbu zao daima. Kwa upande wa Lina Petri aliweza kuangazia, miongoni mwa mambo mengine mengi, juu ya kiasi cha Papa. Alieleza kwamba: “Siku zote nimemjua mjomba wangu kuwa maskini: katika Upatriaki wa Venezia, zaidi ya vyombo vya 'kihistoria', hakukuwa na kitu cha kifahari au cha thamani fulani. (...) Mwisho nilimwona akiwa amelala kitandani baada ya kifo. Ninakumbuka chumba chake katika ghorofa ya papa ... kutoka pale nilipokuwa nimekaa nilimtazama na mbele yangu upande wa kulia kati ya madirisha mawili ya kona ya chumba  na  dawati ... kulikuwa na msalaba tu na picha ya wazazi wake”.

Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano  kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I
Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I

Kwa upande wa Sr. Margherita Marin alisema kuwa: “Alitukaribisha kwa urahisi, bila ya kututia hofu. Alituambia tuombe, kuwa Bwana alikuwa amempa mzigo, lakini kwamba kwa msaada wake na maombi yetu ataupeleka mbele...”. Katika mwezi huo siku zote nilimwona akiwa mtulivu, mwenye utulivu, hakika, alionekana kuwa Papa siku zote , akiomba msamaha kwa usumbufu. Sikuwahi kumwona akiwa na ishara za kukosa subira na mtu yeyote. Kisha picha ya  jioni ya mwisho: “baada ya kutusalimia tayari, Baba Mtakatifu alikuwa kwenye mlango  akageuka tena na kutusalimia tena, kwa mkono wake, akitabasamu ...hadi leo kwangu namwona bado  yuko pale mlangoni. Mtulivu  kama kawaida”. Hatimaye, Padre Juan José Dabusti, akirejeea alikiri hivi: “Ninakumbuka matokeo ambayo kifo chake cha ghafula kilinisababishia. Nilipokuwa nikikua nilimsihi anisaidie kutambua wito wa kufuata, kitu fulani. ? ... Na nina hakika kwamba Albino Luciani alikuwa baba wa kiroho wa ajabu na mwombezi kimya lakini mwenye ufanisi kwangu katika kuamua kukumbatia wito wa ukuhani “. Hatimaye, Padre Juan José Dabusti, akirejelea kuwa kwake kasisi, anakiri hivi: “Ninakumbuka athari ambayo kifo chake cha ghafula kilinisababishia. Nilipokuwa nikikua nilimsihi anisaidie kutambua wito wa kufuata kitu fulani ... Na nina hakika kwamba Albino Luciani alikuwa baba wa kiroho wa ajabu na mwombezi kimya, lakini mwenye ufanisi kwangu katika kuamua kukumbatia wito wa ukuhani".

Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano  kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I
Mkesha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano kuombea kutangazwa mwenyeheri Yohane Paulo I

Katika mahubiri yake Kadinali Kadinali Angelo De Donatis ambayo yalitolewa karibu na mwisho wa mkesha, kana kwamba ni katika kutoa sauti kwa mawazo na hisia za kila mmoja wa wale waliokuwa wamehudhuria, kardinali alizungumzia furaha na faraja kuu katika kumbukumbu ya tukio alilopitia na Papa Luciani kwa miaka arobaini na nne iliyopita. Kardinalinalisema:  “Mimi pia nilishiriki Ekaristi katika Kanisa hili lililojaa waamini na mapadre waliokuja kumkaribisha askofu mpya”. Kwa kuongezea alisema: "Nilikuwa mseminari kijana karibu kupewa daraja la ushemasi, lakini nina kumbukumbu nzuri ya furaha ya kusanyiko la jimbo lililokuwa na furaha katika Kanisa Kuu hili, na uchungu uliompata kila mtu, siku chache baadaye, katika hafla ya kuadhimisha mazishi ya Papa Luciani, ambapo nilipata heshima ya kutoa huduma ya kiliturujia”.

Kardinali De Donatis baadaye aliendeleza na  tafakari yakekuhusu neno Humilitas, yaani Unyenyekevu ambalo lina ubora kuliko mengine, na  ushuhuda wa utakatifu wa Albino Luciani, aliyechagua si kwa bahati mbaya katika kauli mbiu yake ya kiaskofu. Kardinali alisema: “Albino amekuwa mmoja wa 'wadogo' ambao Yesu anawainua katika Injili”, alikuwa amefanya unyenyekevu kuwa nguvu ya maisha yake ya Kikristo. Kiukweli, unyenyekevu kwa Albino Luciani haujawahi kuwa mawazo ya chini, bali maisha ya kukaribisha udogo wa mtu mwenyewe, kumtegemea Mungu kabisa na si kwa nguvu zake mwenyewe, kujitoa kwa wengine kwa urahisi na bila malipo". Kardinali akirejea vifungu viwili vilivyochukuliwa kutoka katika katekesi ya kwanza iliyotolewa na Papa Yohane Paulo wa I kwenye mnamo tarehe 6 Septemba 1978, ilikuwa inahudu  hasa mada ya fadhila ya unyenyekevu alisema: “Mbele ya Mungu msimamo sahihi ni ule wa Ibrahimu  ambaye alisema: Mimi ni mavumbi na majivu mbele zako ee Mungu” Kiuweli, watoto wadogo tunapaswa kujihisi wenyewe mbele ya Mwenyezi Mungu". na akiendelea alisema: "Unamwamini mama yako; “Ninaamini katika Bwana aliyonifunulia”

Papa Luciani alikuwa amehitimisha katekesi hiyo kwa mwaliko wa unyenyekevu ambao, Kardinali De Donatis alithibitisha, kwamba wote wanatarajia kuukaribisha jioni hiyo. Maneno ya Yohana Paulo I alisema: “ Ninajiwekea kikomo, kupendekeza wema unaopendwa sana na Bwana. "Jifunze kutoka kwangu kwamba mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.” Bwana anapenda unyenyekevu sana na kwamba, wakati fulani, anaruhusu madhambi makubwa kwa nini ili wale waliotenda dhambi hizi baada ya kutubu wabaki kuwa wanyenyekevu, hutaki kujiamini kuwa nusu mtakatifu nusu malaika wakati unajua kuwa umefanya makosa makubwa, kwa maana hiyo lipendekeza sana 'kuwa wanyenyekevu.' Hata kama umefanya mambo makubwa, sema: 'sisi ni watumishi wasiofaa' .

MAHUBIRI YA KARD DE DONATIS KATIKA KESHA 3SEPT 2022
04 September 2022, 10:06