Bi Amalia mpwa wa Luciani asimulia mkutano wake na Papa Yohane Paulo I
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika fursa ya kutangazwa kuwa Mwenyeheri Papa Yohane Paulo I, Dominika tarehe 4 Septemba 2022, mjini Vatican, katika misa itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, Bi Amalia Luciani mtoto wa kaka yake mdogo wa Mwenyeheri mtarajiwa amethibitisha juu ya mambo ya kumbu kumbu katika mantiki ya kifamilia kuwa kama baba yake mdogo alikuwa wa aina yake kama mtu ambaye kila mmoja anatamani kuwa naye. Bi Amalia amesema kwamba Albino alipokuwa akirudi nyumbani huko Kanali ya Agordo "kamwe hakuwahi kumkaripia hata mmoja, bali angalau alikuwa na uso mzito, wenye wasiwasi, lakini tabasamu lake lilirudi kila wakati", alisema mtoto wa Edoardo Luciani, kaka wa Papa wa Veneto.
Ilikuwa majira ya joto ya 1978alipokutana na Baba yake mkubwa kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka kwenda kwenye uchaguzi mjini Vatican. Almmsindikiza kwa gari kutoka Canale ya Agordo kwenda Belluno, mahali ambapo alikuwa anafanya kazi na kuishi kwa kupanga. Wakiwa katika safari hiyo, kipindi hicho akiwa ni Patriaki wa Venezia, Bi Amalia alimwomba aweze kuingia nyumbani kwake ili aibariki. Lakini kwa sababu ya muda, Patriaki alimjibu kwamba itakuwa vizuri kufanya hivyo wakati mwingine. Na yeye akamwambia, labda wakati mwingine hatuwakuwapo, utafikiri lilikuwa jibu la kinabii kwa Papa huyo Mtarajiwa. Yeye akamuuliza ikiwa katika nyumba yake angalau ametundika msalaba, na jibu lake lilithibitisha uwepo wa msalaba huo, na yeye akasema kwamba afikirie kama vile ameisha ingia ndani na kuubariki.
Bi Amalia amesema jinsi ambavyo anakuwa na hisia kali kila wakati anapoona picha ya Yohane Paulo I iliyopambwa ndani ya nyumba yake. Na anakumbuka kwa namna ya pekee siku zile ambazo aliweza kulala kwenye kohi wakati wa kipindi kigumu cha ndoa yake. Ma daima aliendelea kuitazama picha hiyo akisema endelea kubariki nyumba yake. Simulizi ya Bi Amalia Luciani, pia inathibitisha hata juu ya historia za baba yake Edoardo, ambaye ni mdogo kwa miaka mitano kuliko Papa. Kwa mujibu wake alisema kwa wote wawili walikuwa na maelewano, karibu kama marafiki wawili ambao wanataka kucheza mizaha pamoja. Mtu anaweza kushangaa ikiwa Albino Luciani, tayari akiwa kama mtoto, alionesha dalili za mapema za maisha yake ya baadaye. Kwa kujibu kwa Tabasamu Bi Amalia, ambaye alisimulia wakati ndugu hao wawili walipocheza na watoto wengine wa Kanale, hasa kipindi cha mchezo wa kusaka hazina ambacho kilimalizika kwa kuvua samaki kama zawadi. Mchezo huo ulikuwa ni kuchukua kikaratasi na kusoma ambapo kulikuwa na kushinda mdori uliotengenezwa kwa koni ya mpine au penseli, lakini kulikuwa na watoto wengine ambao walikuwa na baba zao huko Marekani ambao waliwatumia chokoleti.
Wakati ulipofika wa kuchukua tuzo, kijana Albino alimuashiria kaka yake ambaye alikuwa hajuhi kusoma kwamba atoe barua na akafanya vivyo hivyo. Kwa njia hiyo wote wawili walishinda vipande viwili vya chokoleti. Baba yake Amalia, alimuuliza kaka yake ni kwa jinsi gani amefanya. Na yeye alifunua njama aliyokuwa amefanya na kwamba alikuwa amepata njia ya kuandika tuzo nje ya kadi. Kulingana na Bi Amalia Luciani, alisema kuwa baada ya yote, huo ni ushuhuda wa jinsi ambavyo kila mtu anaweza kuwa mtakatifu kwani inatosha kuwa na utashi na kujitolea. Upeo ambao unatazama maisha ya kila mtu aliyebatizwa na ambao unaweza kupokea msukumo fulani kwa kugundua kwa upya na kusoma wasifu na hali ya kiroho ya Papa wa Veneto. Ushuhuda wa mpwa wa Papa Luciani, umewekwa katika kipindi cha Yohane Paulo I Mwenyeheri katika televisheni ya Telepace katika usiku wa tarehe Mosi Septemba 2022 na wakati wa kesho la kutangazwa kuwa Mwenyeheri kwenye uwakilishi kwa waandishi wa habari katika Ofisi za Vyombo vya habari Vatican, mnamo tarehe 2 Setemba 2022.