Mkutano wa Rimini Agosti 2022:Kard. Zupi ,“Kanisa ni mama”
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Matteo Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Italia (CEI,) aliwaalika Wakristo kujitolea zaidi, katika jamii na pia katika siasa. Kardinali alizungumza hayo katika Mkutano wa tamasha la Urafiki Wa Watu Nchini Italia Agosti 2022 unaofanyika jijini Rimini ambalo linaongozwa na kauli mbiu :”Mapenzi kwa mwanadamu, ambapo pia aliadhimisha Dominika 21 Agosti asubuhi. Kardinali alisema “Wakatoliki lazima waangalie manufaa ya wote, kwa hiyo siasa inapaswa kuwa upendo wa kisiasa na sio urahisi au maslahi madogo. Nadhani ni dalili kubwa kwa kila mtu hata kufikiria kuhusu mustakabali wetu wa karibu, alisema Kardinali wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kuna baadhi ya wasiwasi, kwa elimu, kwa kazi, kwa amani, kwa familia, kwa sekta ya tatu ambayo si 'tatizo la tamasha lakini ni matokeo ya shauku kubwa na kutafsiri mateso mengi na tamaa nyingi na ndio maana Kanisa linapendeza kwani yeye ni mpatanishi muhimu na anayeamua kwa ajili ya taasisi, za sasa na za baadaye”.
Kardinali Zuppi aidha akathibitisha tena juu ya thamani ya Sekta ya Tatu kwamba “Kanisa linapendezwa na Sekta ya Tatu kwa sababu ni tunda la shauku kubwa kwa mwanadamu na ni mpatanishi madhubuti kwa Taasisi za sasa na zijazo.” Wazo pia kwa ajili ya dharura za wakati huu ambapo alisema kwamba: “Ninapofikiria magonjwa ya milipuko, ninafikiria Uviko lakini pia janga la vita vya kutisha katika sehemu zake zote, katika sehemu hii kubwa na ya kushangaza ambayo inaathiri kila mtu kidogo, ambayo ni Ukraine”.
Kardinali Zuppi wakati wa mahubiri yake kwenye misa Takatifu aliyoingozwa kwa washiriki wa Tamasha, hata hivyo, alikumbusha jinsi Wakristo wanavyo paswa kufuata Injili hadi mwisho, kwa maana hiyo wanapaswa kupitia kwenye “mlango mwembamba”, kama jinsi ambavyo Injili ya siku ya Mwinjili Luka ilikuwa inapendekeza. Kardinali alisema: “Tunaingia kwa njia hii tunaposhiriki katika sadaka tuliyo nayo na wasio nayo; tunapomkomboa mtu kutoka kwenye mateso ya upweke; tunapofanya pumzi ya uhai kupendwa kwa kuisindikiza tangu mwanzo hadi mwisho wake; na wakati huo huo tunapowaalika wale ambao hawawezi kurudisha chakula cha mchana”, alisisitiza rais wa CEI na askofu mkuu wa Bologna.
Mlango mpana kwa maana hiyo basi unakuwa, kwa upande mwingine, mwembamba sana, kwa sababu unapunguza kila kitu cha kibinafasi. Ulimwengu na Kanisa vinahitaji shauku isiyoweza kupunguzwa na yenye nguvu kwa mwanadamu, iliyojaa Kristo na ambayo inatambua hamu ya Mungu katika hilo. Kardinali alionesha jinsi Kanisa lilivyo mama na kwamba ni ukweli usioweza kuepukika, wa kufikirika, wa kutojua kuzungumza kama mtoto, lakini unakubali sifa za kibinadamu na za kiroho za “uzoefu wetu wa kidunia.” Uzuri wa kuwa hapa unatufanya tufurahie ushirika huu unaotuunganisha sisi wenyewe na Kanisa zima”.
Kwa upande wa Kadinali Zuppi pia alisema utaifa si chochote zaidi ya u'mimi' mkuu ambao hutetea wengi waliotengwa na umimi. Kinyume chake, ni kwa kugundua wengine tu ndipo tunapojipata sisi wenyewe na tunahisi dhaifu zaidi lakini tunapata nguvu katika kukutana na wengine kwa kutotunza udhaifu wetu mara kwa mara lakini kwa kufanya hii kuwa sababu ya kukutana na wengine. Kwa sababu hiyo aliongeza “hatupaswi kuzoea vitisho vya vita, unyama, kuwatazama wengine kana kwamba hatuguswi.