Mkutano wa Watu Rimini 2022:Kard.Nzapalainga,thubutu kuleta mawazo ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Neno la Amani lilikuwa katikati ya siku ya kwanza ya Ufunguzi wa Tamsha la Urafiki wa Watu Rimini ambapo kufikia tarehe 25 Agosti, takriban midahalo 100 inayotunga tukio zima yenye mada: “Mapenzi kwa mwanadamu”, kifungu kilichochukuliwa kutoka katika maandishi ya Padre Giussani,Mwanzilishi wa Harakati ya Muungano na uhuru(CL). Sera kuu za siasa za kimataifa,u fufuo wa thamani ya amani,mazungumzo kati ya dini ni mambo msingi katika tukio hilo.
Kardinali Nzapalainga:Neno ni kuthubutu, kuthubutu katika kuleta mawazo ya amani
Na kwa upande wa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Bangui katika jamhuri ya watu wa Afrika ya Kati, Kardinali Diedonne Nzapalainga, alisema kwamba kuna sharti muhimu la kufikia mazungumzo ambalo kila mtu lazima atoke kwenye msingi wake na ni muhimu kuwa wapenda amani katika nyayo za Kristo. Kardinali baadaye alizungumzia juu ya matokeo chanya ambayo jukwaa la maungamo ya kidini katika Afrika limefikia hadi sasa. “Suluhisho la vita si ghasia bali ni kuanzisha mazungumzo. Mazungumzo ina maana ya kuacha barakoa kuanguka. Lazima tumtazame mwingine kama mwanadamu kwa sababu amani inafanywa kwa kuwa na maadui”, alisema Karidnali na kutoa mfano kwamba: “Niliona maadui ambao hawakutaka tena kutazamana machoni na sisi, viongozi wa kidini, tulifanya kuwa kama daraja”. Hatimaye, Kardinali alitoa mwaliko wa kuleta amani pia, nchini Italia. Kardnali alitoa mwaliko na kuhimiza kwamba: “Ikiwa unafahamu familia za Kiukreni na Kirusi, waombeni kuonana, kula pamoja, kuzungumza na kila mmoja Tayari ni mwanzo wa amani. Neno ni kuthubutu, kuthubutu katika kuleta mawazo ya amani, lakini subira kubwa inahitajika”, alimalizia Kardinali Nzapalainga.
Patriaki Pierbattista Pizzaballa wa Kilatini wa Yerusalemu
Patriaki Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, wakati wa kutoa tafakari yake Usiku wa Jumamosi 20 Agosti katika mjadala alithibitisha kwamba tumaini ni binti wa imani. Na akazungumza baadaye kuhusu hali ya nchi ya Mashariki ya Kati, huku akitoa nuri jinsi Waisraeli na Wapalestina wanavyokatishwa tamaa, na hasa Wapalestina wanahofia zaidi kwamba wametelekezwa na jumuiya ya kimataifa. Kwa maana hiyo, kujitolea kwa ajili ya kutafuta amani lazima iwe jambo la kwanza la wale walio na imani. Patriaki alisema “ikiwa leo ni kweli kwamba kuzungumza juu ya haki na amani katika Mashariki ya Kati kunamaanisha kuwa upande wa wale wanaopigana na mitambo ya upepo, ni kweli kwamba tamaa ya amani na haki lazima ipate nafasi kwa kila mtu, hasa kwa wale ambao wana wajibu.” Kujitoa kwa ajili ya amani na haki, alisema Patriaki Pizzaballa kwenye mjadala huo kuhusu “ufundi wa amani”. Shauku ya kupatanisha 'katika Tamasha la Rimini sio' zaidi ', kama kipengele cha nyongeza ambacho kinaweza kufanywa tu bila, bali kinyume chake, imani katika Mungu mara moja hujitokeza hamu ya mema kwa kila mtu, shauku isiyozuilika kwa mwanadamu, ili apate maisha yanayostahili wito wake kama mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu”.
Askofu Mkuu Paolo Pezzi wa Moscow Urussi
Hata kwa upande wa Askofu Mkuu Paolo Pezzi, wa Moscow Urussi, alisisitizia nguvu ya msamaha, nguvu alizopata alipokuwa paroko wa kawaida, lakini pia alisisitiza kwamba kutetea nchi ni thamani muhimu. “Hakuna ukweli kwa kila mtu. Kuna ukweli wa sehemu: hii inaonekana wazi wakati maadili fulani yanasisitizwa na nguvu. Amani leo ni thamani si uzoefu. Ikiwa maadili haya yanasisitizwa kiitikadi, yanarudi nyuma. Katika mikono ya mamlaka, maadili haya yanakuwa uhalali wa vurugu mbaya zaidi, kwa sababu kila mamlaka inahisi kuwa mtoaji wa wito wa kimasiha ”alihitimisha.
Ujumbe wa Rais Materella
Katika ujumbe wake, Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella aliweka nuru hata hivyo, jinsi vita vya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, pamoja na huzuni, uharibifu, chuki inayoendelea kuzalisha, inavyotikisa ubinadamu wote katika maadili yake ya msingi na. Ulaya katika utambulisho wake. Na tena, kifungu juu ya ikolojia: kwamba “Siku zote uaminifu kwa mtu unatukabili na changamoto kubwa zaidi ya wakati wetu: wokovu wa sayari kutoka kwa unyonyaji ambao mwanadamu mwenyewe amejifanya kuwajibishwa. Wakati ni Wetu kama Papa Francisko anavypenda kutudia kusema kuhusu ikolojia fungamani kwamba mwanadamu lazima ajenge tena usawa na mazingira na maliasili na anaweza kuifanya tu kwa roho ya mshikamano”.