Maaskofu wa Italia Maaskofu wa Italia  

Maaskofu wa Maeneo ya Ndani:Ni lazima wafikirie kwa upya utenda wa kikuhani

Ofisi ya Kitaifa kwa ajili ya mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Italia,imetoa tamko la mwisho baada ya mkutano wa Maaskofu wa Maeneno ya ndani 30-31 Agosti uliofanyika Benevento.Katika tamko hilo maaskofu wanabanisha wao kama Nazareti ndogo,ya pembezoni,lakini walinzi wa ukweli wa thamani zaidi,hawatachoka kusindikiza wagonjwa hadi mwisho,vijana na wahamiaji ambao ni utajiri mkubwa wa jamii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 30 hadi 31 Agosti 2022 umefanyika Mkutano katika Kituo cha Amani huko Benevento, Italia, wa maaskofu katika “Maeneo ya Ndani ambapo walishiriki maaskofu zaidi ya 30 kutoka Mikoa 12. Mwisho wa mkutano wao, Maaskofu wameshirikisha uthibitisho wa mwisho. Maaskofu hao wanasema "kama maaskofu kutoka nchi yote tuliokutana  huko  Benevento ili kutafakari mikitadha ya mang’amuzi kwa lengo la kufanya kazi uchungaji katika Maneno ya ndani, tunamshukuru awali ya yote Bwana kwa uzoefu wa umoja tuliouishi. Kwa maana hiyo katika siku hizi zimetusaidia kujuana vema na kuwa na msimamo wa uhusiano zaidi wa kidugu kati yetu ili kufanya uzoefu wa sinodi, kwa kukua katika huduma ya umoja, wote pamoja kuunganika bila kengele kama tulivyokumbushwa katika Barua ya Papa Francisko".

Ulinzi wa kweli wa thamani ya binadamu

Maaskofu aidha wamebainisha kuwa Maeneo ya ndani yanajumuisha sehemu ya Nchi ambayo wameunganishwa na baadhi ya mambo muhimu na kuwa mlinzi wa utajiri wa ajabu na ambao bado unakuwa wa aina mbalimbali. Kwa mfano wao, kama Nazareti ndogo, ya pembezoni, lakini wanakuwa walinzi wa ukweli wa thamani zaidi.  Maaskofu wanabainisha kuwa hawatachoka kuwasindiza wagonjwa hadi mwisho katika aina ya kuendelea kwa matibabu, lakini wanataka kuunda ngome, nguvu ya kuwatetea, kutoa uhai kwa mitandao ya mshikamano inayoweza kuamsha maelewano. Kwa maana hiyo maaskofu wanaomba sera za kisiasa za uingiliaji wa dhati, madhubuti, wa kiakili, unaochochewa na mipango tarajiri, isiyochafuliwa na masilahi finyu au mafanikio ya uchaguzi: kwa maana hiyo, ikiwa uhuru wa kutofautisha utaanza kutumika, hii ingeongeza ukosefu wa usawa tu nchini. Na kama jumuiya ya Kikristo maaskofu wanataka kukua katika ufahamu na ushiriki.

Kuwa na ujasiri wa kuvunja mantiki za "ilizoeleka kufanyika kwa njia hiyo"

Maaskofu pia wanabainisha kwamba masuala ni mengi yaliyotolewa kwenye meza, ambayo haikuwezekana kutoa majibu ya kutosha. Kwa hali yoyote, wanaombwa kuwa na ujasiri wa kutoka kwa mipango ya sasa iliyogandamana, na  kuvunja mantiki ya daima isemayo “tumezoea kufanya namna hii" na kutafakari kwa upya uhusiano kati ya utamaduni  na uvumbuzi, utayari wa kusikiliza sauti ya Roho, ili kurudisha ukuu tendaji kwa Neno la Mungu na kwa utangazaji wa Injili, pia kuunganisha vyema uchungaji ambao mara nyingi hauna usawa katika nyanja ya kiutamaduni na kiliturujia. Maaskofu wa Italia kwa maana hiyo, wanabainisha kuwa ni lazima wafikirie kwa upya utendaji wa huduma ya kikuhani na kuendeleza kwa uthabiti ukuhani wa pamoja wa wabatizwa wote. Aidha katika huduma mbalimbali na zenye kuwajibika, kuimarishwa kwa ushemasi wa kudumu, nguvu za walei, hasa wanawake, jambo ambalo ni muhimu sana,  sehemu ambayo inayondwa kwa hakika na kiungo cha jumuiya zao, bila kusahau waheremiti na jumuiya za watawa, ambazo katika maeneo ya ndani ya pekee ni nguvu ya siri ambayo huweka nguvu nyingi kuwa hai. Zaidi ya yote, wanapaswa kuzingatia ubora wa mahusiano, kwa sababu hii ndiyo inahitajika sana. Uwepo mkubwa wa wazee unajumuisha, katika uhalisia wao huo  urithi wa ubinadamu na uzoefu wa maisha ambao lazima uthaminiwe kabisa.

Uhamiaji unaweza kuwa fursa ya kufufua hali nyingi za upunguaji wa watu

Maskofu vile vile katika tamko lao wamebainisha juu ya suala la mtiririko wa uhamiaji  kwamba unaweza kuwa fursa ya kufufua hali halisi nyingi chini ya kupungua kwa kasi kwa idadi ya watu, lakini pia ni muhimu kuboresha zaidi na zaidi nia ya kusikiliza, kudhani, kwa kufuata sheria, mantiki ambayo ni jumuishi, si ya kutengwa. Maaskofu kwa maana hiyo wanajitoa  kubaki kwa sababu Kanisa halitaki kuacha maeneo haya, bila hivyo kujikaza katika maumbo, mitindo na mazoea ambayo yangeishia kuwa ya kudhoofika. Kwa njia  hiyo, wamejitolea kuwasaidia vijana wao wanaotaka kubaki, wakijaribu kuwapa mshikamano madhubuti, na wamejitolea kuwasindikiza wale wanaotaka kwenda, wakiwa na matumaini ya kuwaona wakirudi tena siku moja wakiwa wametajirishwa na ujuzi na  uzoefu mpya. Maaskofu vile vile wamebainisha kwamba wanahisi kusikia sauti ya nabii iliyo hai: “Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? (Isa 21:11). Mtume anajibu: "Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru" (Warumi 13:12). Kwa maana hiyo wanaliomba Kanisa, wakianza na wao wenyewe kabisa, jamii, siasa, kuchukua himizo hili kwa uzito. Maeneo ya ndani, ambapo maisha hayataki kufa, yanaweza kuwa maabara ya mawazo, rasilimali hai, hazina ya ajabu kwa nchi nzima: ni juu yao, wote  kwa pamoja ( wachungaji, jumuiya ya Kikristo, jumuiya ya kiraia, siasa ) ili  kufanya hamu hiyo iwe ukweli.

TAMKO LA MAASKOFU WA ITALIA MARA BAADA YA MKUTANO WA 30-31 AGOSTI
31 August 2022, 15:48