Tafuta

2022.08.17 Kongamano la Kimataifa la  SIGNIS nchini  KOREA 2022 2022.08.17 Kongamano la Kimataifa la SIGNIS nchini KOREA 2022 

Kongamano la dunia la SIGNIS 2022 huko Seoul,Korea Kusini!

Jumanne huko jijini Seoul,Korea Kusini, Kongamano la Dunia la SIGNIS 2022 lilifunguliwa rasmi.Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Dk.Paolo Ruffini,alisoma ujumbe wa Papa Francisko katika kongamano hilo la siku nne lililokusudiwa kwa wawasilianaji wote wa Kikatoliki.Hotuba mbali mbali,mijadala,ziara na ubunifu vimetoa ladha ndani ya kongamano hilo la kina.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

SIGNIS ni Chama cha Kikatoliki cha Wanataaluma wa Mawasiliano Ulimwenguni, abacho kimefanya Kongamano la Ulimwengu la SIGNIS huko Seoul, nchini Korea kuanzia 15 hadi 18 Agosti 2022 kwa mara ya kwanza katika muundo wa mseto, yaani kwa wanahabari wapatao 100 wa vyombo vya habari vya Kikatoliki kutoka mataifa 34 tofauti wakihudhuria ana kwa ana huku washiriki wengine wakihudhuria kwa kufuatilia kwa njia za mitandao mipya ya kidijitali, na pia kwenye Zoom na YouTube.

Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS
Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari Vatican, Padre Paulo Samasumo na Mwenyekiti Msaidizi wa SIGNIS akiwa huko Seoul katika kongamano hilo amebainisha kuwa mada kwa  ujumla ya Kongamano ilikuwa ni “Amani katika ulimwengu wa kidijitali.” Na katika siku ya kwanza kwa hakika ilitengwa kwa ajili ya kuzamishwa kwa ajili ya kiutamaduni katika jamii ya Wakorea, chakula na kutembelea baadhi ya maeneo muhimu, hasa yale yanayohusiana na amani na utatuzi wa migogoro. Hata hivyo Kongamano lilifunguliwa na usomaji wa Ujumbe kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko ambao uliosomwa na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Dk Ruffini,Mwenyiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano
Dk Ruffini,Mwenyiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano

Kwa mujibu wa Padre Samasumo ameeleza kuwa Wataalamu wa vyombo vya habari vya Kikatoliki vya SIGNIS walitumia muda wao kujifunza kuhusu athari za kuendelea kwa mgawanyiko kati ya Korea mbili-Kaskazini na Kusini. Katika uzoefu huo walijifunza kwamba kufikia leo hii kuna mamilioni ya familia za Korea Kusini ambazo bado zinayumba yumba kutokana na utengano kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Ni mjadala mchungu na mgumu unaogusa familia nyingi, alisistiza Padre Samasumo. Hata hivyo washiriki pia walitembelea sehemu moja iitwayo Odusan ambayo ni eneo la kielimu ambalo linatoa muhtasari mzima wa maisha nchini Korea Kaskazini. Kwa upande mwingine, ni Kituo cha Amani na Umoja wa Kikatoliki, ambacho wajumbe pia walitembelea, na ambacho kimejitolea kuhamasisha na kuombea upatanisho kati ya Korea Kaskazini na Kusini.

Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS 2022
Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS 2022

Akiwa kando ya Kongamano hilo, Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa  Baraza la Mawasiliano, alisema kwamba matukio ya ufunguzi huo yanawapatia washiriki fursa ya kukusanyika pamoja na kubadilishana mawazo juu ya mustakabali wa ulimwengu wa kidijitali na jinsi ya kujenga amani katika ulimwengu huu uliogawanyika sana. Pia alisema kwamba ndani ya mikutano ya awali pia ilionesha umuhimu wa SIGNIS na kuwa na maono ya siku zijazo na kwamba washiriki walikuwa na wasiwasi wa kutafuta njia ya mawasiliano ili kuwaunganisha watu bila teknolojia kuwa nyingi. Lakini "Kuunganishwa katika mawasiliano, inamaanisha kujenga ulimwengu ulio bora, amani, matumaini; na kupambana na upweke wa nyakati zetu, licha ya matatizo tuliyo nayo", alisema Dk Ruffini.

Tamasha la Vijana katika Kongamono la Signis 2022 huko Seoul
Tamasha la Vijana katika Kongamono la Signis 2022 huko Seoul

Na katika hotuba yake ya awali kwa Kongamano Dk. Ruffini alisema kwamba “SIGNIS katika utambulisho wake ina neno ishara, kama ishara ya kupingana kwamba hii inatufanya kuelewa jinsi wawasilianaji wa Kikatoliki wanaweza kuwa ishara ya kupingana, isiyoidhinishwa, lakini wakati huo huo si inapokuwa, na si tofauti na dunia ambayo sisi lazima kuwa. Hivi ndivyo Yesu katika Injili anaomba kwa kila mtu, lakini hasa anauliza mawasiliano. Shauku ya vijana inaambukiza wao wanatuambia: urasimu kidogo na hamu zaidi ya kufanya, hamu zaidi ya kuwa pamoja, kuvumbua mambo mapya, sio kufikiria na mipango ambayo mara nyingi hupunguza Kanisa, mfumo wa nguvu. Vijana wanaomba hivyo; hawana tamaa ya madaraka, wanatamani uhusiano, uzoefu, upendo, ukweli na shauku ambayo kwayo wanakaribisha mambo yanayozungumzia na hili ni somo kwetu sote. Dk. Ruffini akiendelea na hotuba yake alisema kuwa: "Tunafanya kila tuwezalo na labda lazima tujitahidi kuonesha kwamba Kanisa, kwamba mawasiliano ya Kikatoliki ni juu ya haya yote, bila kujisikitikia, kwa sababu mambo ambayo sio sawa yanaweza kubadilishwa kila wakati. Ni juu yetu kuzibadilisha, tunaweza na lazima tuwaombe vijana watusaidie”.

Kongamano la Kimataifa la Signis huko Seoul,Korea 2022
Kongamano la Kimataifa la Signis huko Seoul,Korea 2022

Tarehe 18 Agosti wawakilishi wa Chama cha Kikatoliki cha Mawasiliano Ulimwenguni, wakiwakilishi nchi 34, waliounganika Seoul, nchini Korea wanaondoka, baada ya kujadili kwa kina mada ya  “Amani katika ulimwengu wa kidijitali. “Tunaishi katika ulimwengu ambapo mgawanyiko wa kidijitali na  unaathiri pengo kati ya matajiri na maskini, na kusababisha ukosefu wa usawa katika kupata matunda ya mapinduzi ya kidijitali. Ulimwengu unakabiliwa na hatari za mitengano ya kijamii na kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, kidini, kiroho na ikolojia, ambayo husababisha kutengwa, kuchanganyikiwa na kukata tamaa, michezo ya mtandaoni, picha mbaya za mitandaoni kuoneshwa vurugu kupita kiasi na maudhui ya asili yanayogawanya vyombo vya habari ambayo husababisha tabia mbaya na athari mbaya za habari za uwongo kwa jamii ya kisasa", ndivyo inasomeka taarifa ya mwisho. Kwa njia hiyo kutoka katika Kongamano la SIGNIS 2022 huko Korea  ndipo wanatoa wito wa kuhama kutoka kujitolea kwa mtu binafsi hadi ujenzi wa kijumuiya. 

 Kongamono la Signis 2022 huko Seoul
Kongamono la Signis 2022 huko Seoul

Hata hivyo katika wito wao wa mwisho wanabainisha kwamba kama Papa Francisko anavyosema, kuwa “Mtindo wa Mungu ni ukaribu, huruma na upole". Kwa njia hiyo: “Tunahitaji kufuma mtandao kwa ukweli na uzuri wa imani na matumaini. Teknolojia lazima ijazwe na maadili na ufikirio". Na wakitiwa moyo na historia za vijana duniani kote kuhusu kujenga amani, wanawataka wataalamu wa vyombo vya habari na raia kuchukua hatua ili kulinda haki za binadamu zinazohusika na vita na maeneo ya migogoro. Naye Rais wa SIGNIS Bi Helen Osman," alisema kuwa "Mmefanya kile ambacho wengi walidhani kuwa hakiwezekani, huku akiishukuru timu ya Korea iliyoandaa Kongamano hilo kwa undani sana, na kusisitiza hasa mchango unaotolewa na vijana kwa ubunifu na nguvu zao.

18 August 2022, 11:29