Tafuta

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 

AMECEA:Viongozi wa Kanisa na mashirika waombe Ufadhili kwa ajili ya Mapadre na watawa

Katika ujumbe wa Mshikamano kutoka Shirika la kimataifa la Kanisa Hitaji liliwashauri viongozi wa Kanisa na mashirika waliokuwa katika Mkutano Mkuu wa AMECEA kuwaombea ufadhili mapadre,watawa na waamini kwa ajili ya masomo mbali mbali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shirika la Kimataifa la Kanisa Hitaji (ACN) liliwaomba   maaskofu na wakuu wa Mashirika katika kanda ta  AMECEA kuomba ufadhili wa masomo kwa ajili ya mafao ya masomo kwa mapadre, Watawa au waamini Walei. Makundi ambayo yanalengwa ni walimu wa wakati ujao, wafundaji na wakurugenzi wa kiroho katika seminari kuu na ndogo; Mashirika ya watawa pia kwa matayarisho kwa ajili ya utume maalum. Wataalam wa siku zijazo katika masomo ya sheria za kanoni ya kuanzishwa kwa mahakama ya kikanisa, ili kurekebisha ukosefu walimu wanasheria wa kanuni waliofunzwa ndani ya majimbo au mashirika ya kikanisa. Hayo yalisemwa na Bwana  Tony Zelender, mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Kanisa Hitaji (ACN) akisoma ujumbe wake wa mshikamano kwa viongozi wa AMECEA waliokuwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA kuanzia tarehe 10 -18 Julai 2022.

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Bwana Zelender alibainisha kuwa shirika hilo (ACN) linatoa aina mbili za ufadhili wa masomo kwa ajili kozi za kiuchungaji: kwa upande mmoja, ufadhili wa masomo yanayofanyika katika eneo la nyumbani yaani Kanisa mahalia, kwa upande mwingine udhamini wa masomo Ulaya. Akiendelea na maelezo Bwana Zelender alisema sehemu ya Ufadhili inatoa misaada ya masomo kwa njia ya ufadhili wa masomo kwa kozi za uzamili katika taalimungu, falsafa, sheria ya kanoni ya Sheria, na mawasiliano ya kijamii katika vyuo vikuu vya kikanisa na vyuo vikuu, hasa huko Ulaya na katika sehemu nyingine za masomo zilizochaguliwa Amerika Kaskazini, ambazo sio hupatikanaji wa maeneo ya nyumbani ya washirika wao na pia kwa kozi za ulinzi katika Taasisi ya  Anthropolojia (IADC) katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian Roma.

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Kwa kufafanua zaidi pia alisema kwamba wenye ufadhili wa masomo wanatoka katika mjimbo na mashirika kutoka nchi zote ulimwenguni ambapo Kanisa linateswa, chini ya shinikizo, au lina uhitaji. Kuhusu Afrika, alisema kwamba kwa mwaka 2020/21 ACN ilikuwa na nafasi za masomo 104, kati ya hizo 39 kwa wenye nafasi za masomo kutoka nchi za AMECEA. Pia alitaja baadhi ya masharti yanayopaswa kuzingatiwa kwa kuomba udhamini ni pamoja na kurejea majimboni baada ya masomo, maombi lazima yafanyike kabla mtahiniwa hajatoka jimboni kwake, hakuna msaada wa shahada ya kitaaluma ambayo mtu huyo aliwahi kusomea.

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Mtahiniwa anapaswa kuwa na uzoefu angalau usiopungua miaka miwili ya kichungaji mara baada ya kupata daraja la ukuhani; kikomo cha umri kama sheria, mtahiniwa hapaswi kuwa na zaidi ya miaka 40,  lakini, hasa kwa mapadre wanaofanya kazi kama waalimu wa seminari na wasimamizi wa seminari, wanaweka tofauti, kwa mapadre walio na digrii ya leseni ambao tayari wamefanya kazi katika seminari/mhadhiri na wataendelea kufanya hivyo, askofu wake anaweza kuomba ufadhili wa masomo ya udaktari, kwa watahiniwa wenye umri wa zaidi ya miaka 40, hata hivyo, mwaka wa sabato unaweza kuombwa kila wakati.

Ikumbukwe: Mkutano Mkuu wa AMECEA kwa kawaida hufanyika kila baada ya miaka minne. Kwa maana hiyo viongozi hao walihitimisha kwa kuchagua mada na nchi mwenyeji kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 21 ujao  utakaofanyika mnamo 2026 jijini Kampala Uganda.

UFADHILI WA MASOMO KWA MAPADRE, WATAWA NA WAAMINI WALEI
11 August 2022, 15:54