Tafuta

Kijiji cha Bunagana katika eneo la Rutshuru  nchini Cong DRC Kijiji cha Bunagana katika eneo la Rutshuru nchini Cong DRC  (AFP or licensors)

Congo DRC:Tukio la vita na ukosefu wa usalama kutesa watu Mashariki mwa nchi!

Mtazamo wa Kanisa la Bukavu nchini DRC unaelekea hasa katika hali mbaya kufuatia uvamizi wa hivi karibuni wa jiji la Bunagana katika eneo la Rutshuru na kikundi cha waasi cha M23 ambacho kimeanza mapigano katika mzunguko wa vurugu,upotezaji wa maisha,uhamishaji wa watu na makazi yao,uharibifu wa mfumo wao wa kiuchumi na kijamii.Hii ni historia inayojirudia ambayo Askofu Mkuu Rusengo,ameeleza.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu François-Xavier Maroy Rusengo, wa Bukavu, na mji mkuu wa Kivu Kusini, moja ya majimbo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo wanamgambo na magenge yenye silaha yamekuwa yakifanya maafa bila kuadhibiwa kwa miongo kadhaa, kuwanyanyasa watu, amesema kkwamba "hali ni mbaya, kwa sababu upepo wa vita na ukosefu wa usalama unavuma tena katika sehemu hii ya mashariki ya nchi yetu”.  Askofu Mkuu alibainisha kuwa mtazamo wao unaelekea hasa katika hali mbaya kufuatia uvamizi wa hivi karibuni wa jiji la Bunagana katika eneo la Rutshuru na kikundi cha waasi cha M23 ambacho kimeanza tena mapigano katika mzunguko wa vurugu, upotezaji wa maisha, uhamishaji wa watu na makazi yao, uharibifu wa mfumo wao wa kiuchumi na kijamii. Ni historia inayojirudia ambayo Askofu Mkuu Rusengo, katika taarifa yake aliyoituma kwenye Shirika la habari za kimisionari Fides anaifafanua.

Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha
Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha

M23 ni harakati moja la msituni ambayo  tangu mwaka 2013 lilikuwa limetia saini mkataba wa amani na serikali ya Kinshasa lakini ambayo imechukua  kwa mara nyingine tena silaha hivi karibuni. Mamlaka za Congo inashutumu pai nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono kikundi hiki M23; japokuwa shutuma  pia zinarudi tana kutoka kwa  Serikali ya Kigali dhidi ya Kinshasa kwamba wanatunza badhi ya makundi ya wapinzani wa Rwana wenye silaha wenye makao yake nchini DRC.

Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha
Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha

Hata hivyo Askofu Mkuu Rusengo wa Bukavu amesema kuwa:  “Cha kushangaza ni kwamba  msaada wa nje siku zote ni uleule, wenye mpango uleule na wenye malengo yale yale: kuondolewa kwa sehemu hii ya nchi kutoka kwa udhibiti wa serikali yetu kuu na pengine kuunganishwa na nchi jirani”, na wakati huo huo lakini anawatia moyo waamini kutojiacha wenyewe kwa mawazo yasiyo ya kimaadili kwani amesema kuwa maono ya kushindwa na kijuu juu katika sehemu wa Injili huwaongoza wengine kuona katika kila jambo linalotokea ni mapenzi ya Mungu, au hata adhabu; wengine wanafikiri kwamba Mungu tawafanyia kila kitu.  Kinyume chake sio hivyo”. Askofu Mkuu Rusengo alisisitiza kwamba Kanisa Katoliki linajisikia ndani yake na kushiriki kilio cha watu wa Congo na linataka kwa nguvu zake zote kukomesha umwagaji damu wa watu wengi wasio na hatia”.

Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha
Watu wa eneo la Rutshuru kuwa mashakani kutokana na makundi ya waasi yenye silaha

Watu wa Congo wamekasirishwa na hali ya sintofahamu ya jumuiya ya kimataifa dhidi yao alisema tena askofu Mkuu na kwamba ukiukwaji mkubwa umefanywa dhidi ya Wakongo, iliyoandikwa na Ripoti ya Ramani ambayo lakini karibu hakuna chochote kinachofanyika kuwawekea vikwazo na kuwalipa fidia waathirika  alisema Askofu Mkuu  Rusengo katika kukemea hali ya jumuiya ya kimataifa ambayo kwa zaidi ya miaka 25 imeanzisha operesheni ya kulinda amani (MONUSCO) ambao ni ghali zaidi wakati wao kwa wastani wa dola bilioni  kwa  mwaka, lakini matokeo yake  ni duni. Askofu Mkuu Rusengo kwa maana hiyo ameiomba serikali ya Congo kupitia kwa upya uhusiano wake na jumuiya ya kimataifa ambayo inaichukulia nchi yao kama taifa la daraja la pili ambalo usalama na maendeleo yake vinahesabiwa kidogo, na kuunda jeshi la kweli na sio muunganisho wa waasi wa zamani ambao hawakuunganishwa kiukweli.

28 June 2022, 15:22