Tafuta

2022.05.23 Tanzania: Kongamano la Mapadre vijana , watawa wa kike na kiume lilioandaliwa na Jimbo Kuu la Mbeya Tanzania 16-19 Mei 2022 2022.05.23 Tanzania: Kongamano la Mapadre vijana , watawa wa kike na kiume lilioandaliwa na Jimbo Kuu la Mbeya Tanzania 16-19 Mei 2022 

Tanzania,Pd.Mwadende:Kukosa mahusiano ni kurudisha hatua nyuma za utume

Katika hitimisho la Kongamano la Mapadre Vijana,watawa wa kike na kiume kutoka Jimbo Kuu la Mbeya,Songea na Jimbo la Sumbawanga,Tanzania kuanzia 16-19 Mei 2022,wakati wa mahubiri ya Padre Mwadende Dekano wa Dekania ya Chunya B.alihimiza suala la mahusiano mema kuanzia ngazi ya chini hadi kufikia ya juu hasa kuwajali na kuwaheshimu mapadre wazee."Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu."

Sr. Marta Mwalugala & Thom Mpanji-Mbeya.

Mapadre, Watawa wa kike na kiume, waamini walei na familia ya Mungu kwa ujumla wajitahidi kujenga mazingira ya mahusiano na mawasiliano mema mahali pa kazi ili kuleta tija na maendeleo endelevu ya kimwili na kiroho kwa Kanisa na Taifa la Mungu kwa ujumla. Ndiyo mwaliko uliotolewa na Padre Pascal Mwadende Dekano wa Dekania ya Chunya B, na Paroko wa Parokia ya Mwambani, wakati wa mahubiri yake katika Misa takatifu iliyoadhimisha tarehe 18 Mei 2022, katika Kanisa la Mtakatifu Peter Clavery, Parokia ya Mlowo. Katika misa Takatifu hiyo iliudhuriwa na Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, wa Jimbo Kuu la Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Mapadre Vijana kutoka Jimbo Kuu la Mbeya, Songea na Jimbo la Sumbawanga, waliofanya Kongamano la Mapadre Vijana katika Kituo cha kichungaji cha Mlowo, Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe, Tanzania lililohamasishwa na Jimbo Kuu Katoliki Mbeya kuanzia tarehe 16 na kumalizika 19 Mei 2022 katika ufukwe wa Matema Ziwani Nyasa.

KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA
KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA

Katika fursa ya Misa hiyo naye Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa Jimbo Kuu la Mbeya aliwatangazia juu ya Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 22 Februari 2022,kuridhia kumpa hadhi ya heshima ya kuwa monsinyori Padre Edwin Mdeba, Paroko wa Parokia ya Shewa. Padre Mwandende kwa kuongozwa na somo lililosomwa wakati wa Misa hiyo alisema Paulo na Barnaba walikuwa na mahusiano na Kanisa la Yerusalemu, kwa njia hiyo suala la mahusiano halikutumika hovyo hovyo au kwa watu wasiohusika. Kwa maana hiyo Padre alitoa swali: Je leo hii Kanisa lina mahusiano?  Kwa kujibu alisema: “ la hasha kwani zaidi ya asilimia 80 hatuna mahusiano, kwa sababu parokia moja inakosa mahusiano na mawasiliano na parokia nyingine katika kutoa misaada mbalimbali  hivyo kukosa  hata kupiga hatua za mbele”. Kwa kutoa mfano mwingine Padre Mwadende alisema: “inawezekana kutokea hata Padre au Mapadre wakakosa mahusiano na mawasiliano mazuri na Askofu wa Jimbo,  mahali ambapo inapelekea manung'uniko, presha, kisukari na mwisho wake ni nini…? katika sehemu yeyote ya kazi  ni lazima uwe na mahusiano na mlezi au  mkuu wa malezi ambapo haijalishi unampenda ama haumpendi ili uweze kufanikisha kile kilichokupeleka hapo”.

KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA
KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA

Padre Mwadende akiendelea na msisitizo huo alisema ‘umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’ kwa kutoa hata tahadhali ya kutafuta mahusiano na mawasiliano yasiyo na tija  kwa  afya  ya kimwili na kiroho na kuonya kuhusu  dhambi ya ubaguzi wa namna yeyote katika Kanisa. Kwa kuhitimisha mahubiri yake Padre Mwadende alitoa mwaliko wa kuendelea kujenga mahusiano miongoni mwa waamini,  jumuiya ndogo ndogo za kikristo hadi ngazi ya juu huku wakiwa karibu hasa kwa  kuwajali na kuwaheshimu mapadre wazee.

KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA
KONGAMANO LA MAPADRE NA WATAWA VIJANA JIMBO KUU MBEYA,SONGEA NA SUMBAWANGA,TANZANIA

Hata hivyo awali akizungumza na Mwandishi wa Habari, Padre Joseph Zaya, Mwalimu  na Mlezi wa Seminari ya Kaengesa Jimbo la Sumbawanga , alimshukuru mwenyezi Mungu kwa kukutana na mapadre vijana kwa wazo alilompatia Askofu Mkuu Nyaisonga. Kwa mujibu wake alisema, Askofu Mkuu Nyaisonga amewakutanisha mapadre Vijana waliowahi kukutana katika safari zao za utume ikiwemo katika mashule na vyuo hususani Seminarini, pia wamepata fursa ya kujifunza kwa kusaidiana, kufahamu lengo lao katika utume pamoja na kujiimarisha kiafya kwa michezo mbalimbali.

Huo ni mwendelezo wa Kongamano la Mpadre wazee, Machi 2022

Ikumbukwe, Kongamano la Mapadre, Vijana katika Jimbo Kuu la Mbeya, limefuatiwa na Kongamano lilotanguliwa la Mapadre Wazee Jimboni humo, lililofanyika mwezi Machi mwaka huu na kuhitimishwa kwa ibada ya Misa tarehe 25 Machi 2022. Askofu Mkuu Nyaisonga katika misa hiyo alisema katika huduma yao ya kikuhani, wao wanafanya Mungu awe katikati ya watu wao, wanapokea jukumu, la kumjengea Mungu nyumba. Kwa maana hiyo ni kufanya mwendelezo ule wa ufalme wa milele wa Kristo kwa sababu ni Kristo mwingine. Padre mwingine, “Alter Christus”,  kwa kuwa wao wanaendeleza uwepo wake Kristo , wanashiriki kiti cha kifalme, kile cha milele hapa duniani na wanakuwa ishara iliyo wazi ya ufalme unaodumu kati kati ya watu. Kwa njia hiyo wao moja kwa moja wanashiriki kujenga nyumba ya Milele ya Mungu. Na hiyo ndiyo fursa kubwa waliyo nayo, nafasi kubwa ambayo imetokana na kusudio la Mungu na kudhihirishwa wazi wazi na mwitikio wa Bikira Maria na kuendeleza nafasi yao kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

KONGAMANO LA MAPADRE WAZEE JIMBO KUU KATOLIKI MBEYA TANZANIA MACHI 2022
KONGAMANO LA MAPADRE WAZEE JIMBO KUU KATOLIKI MBEYA TANZANIA MACHI 2022
Kongamano la Mapadre Vijana Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Tanzania
23 May 2022, 10:02