Nchi Takatifu:Kuwekwa Wakfu kwa Askofu Mteule Rafic Nahra:Ajifunze kuwa baba
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mahubiri ya Patriki wa Kilatini wa Yerusalemu, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, huko Nazareth, akiongoza Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu kwa Askofu mteule Pier Rafic Nahra, ambaye ni Askofu Msaidizi wa Upatriaki hivi karibuni alisema: “Hakika Askofu lazima awe msimamizi mzuri, lazima awepo katika maisha ya kichungaji, kijamii na kisiasa kwa ajili ya watu aliokabidhiwa, ajue jinsi ya kuliongoza kundi katika maisha ya Kanisa, afundishe, aitunze imani, anapaswa kujua jinsi ya kukabiliana, kwa ufupi na matukio mbali mbali ya maisha ya kikanisa na ya jumuiya ambamo Kanisa limeingizwa, akitetea haki za Mungu na za mwanadamu. Hili liko wazi. Lakini kwanza kabisa ili kufanya hivyo kunahitajika kujifunza kuwa baba”.
Askofu ni baba kwanza kwa ajili ya makuhani
Katika misa hiyo pia walishiriki Askofu William Shomali, ambaye ni Msaidizi wa Upatriaki wa Yerusalemu, na Askofu Thibault Verny, msaidizi wa Paris ambapo Patriaki Pizzaballa akiendelea na mahubiri hayo alisema Askofu ni “Baba kwanza kabisa kwa ajili makuhani. Utambulisho wa kuhani unahusishwa na ule wa askofu. Kuhani hawezi kuwepo peke yake. Huduma yake inashuka na inahusishwa na ile ya askofu”. Kwa maana hiyo alimshauiri kwamba “Uwe baba kwa waamini wote. Usijenge vizuizi vingi kati yako na watu. Umbali fulani kwa wakati mwingine ni muhimu, ili kuhifadhi uhuru wa ndani wa mtu na usijiruhusu kushindwa na hali. Hata hivyo, itakuwa muhimu kupata uwiano sahihi, ambao unajiacha wazi vya kutosha kwa mahitaji mengi ya waamini, kwa maombi yao ambayo wakati mwingine hayafai, yametiwa chumvi mno, magumu, bila kufanya tofauti au mapendekezo. Usichanganye ubaba na urafiki rahisi. Huduma yako ya kiaskofu itajieleza katika muktadha maalim wa jamii ya Israeli”, alisema Patriaki Pizzaballa.
Ushuhuda kwa vijana
Askofu Mkuu Pizzaballa alisema kuwa: “Ni ulimwengu mgumu na kama hali zetu zote tofauti za kichungaji, katika mabadiliko makubwa na kwa juhudi nyingi na mivutano.” Kwa maana hiyo alitoa baadhi ya maelekezo kuhusu mafundisho ya Kikristo na kwa vijana kwamba itakuwa kazi yake kusaidia Kanisa lao hili kutambua, katika eneo hilo la kichungaji mifumo na njia za malezi yanazoendana na nyakati zao na vijana wao, kuwafanya wawe na uwezo wa kukabiliana wakiwa Wakristo watu wazima na jamii ya Israeli yenye dini nyingi na tamaduni nyingi. Wakati huo huo alisema ni lazima aongeze pia kwamba ana uhakika mikakati ya kichungaji itabaki kama barua iliyokufa, ikiwa haitaambatana na ushuhuda wa kweli na wa ukweli wa imani, ambavyo lazima kwanza viwe vyake na vya makuhani wote.
Sinodi na ushiriki
Kuhusu vijana, Patriaki Pizzaballa alikumbusha kwamba labda hawapendezwi na hotuba kuhusu Yesu, nadharia za kidini, au hotuba zisizoeleweka. Wao labda wanasubiri ushuhuda wa kuaminika. “Leo hii aliyefufuka hukutana juu ya yote kupitia mashuhuda.” Kutokana na hili kwa hakika hakukosa kuzungumzia juu ya mchakato wa Sinodi na ushiriki, kwa maana hiyo alisema kuwa: “Sinodi na ushiriki, ni njia ya kuwa Kanisa. Kwa hakika ni rahisi zaidi na kwa ufanisi zaidi kujiamualia mwenyewe, moja kwa moja na kuamuru. Lakini mwishowe pia ni njia tasa, ambayo haitoi maisha katika Kanisa, kwa sababu haiwafanyi wa kukutana na Kristo. Kwa hiyo inasaidia sehemu hiyo ya Kanisa lao la Yerusalemu, ambalo wanajali sana, kiukweli kuwa jumuiya kubwa na nzuri, ambapo washiriki na kushirikiana hatua kwa hatua kuwa ukweli unaoonekana wa Kanisa.