AMECEA:Mwenyekiti wa AMECEA anathamini jitihada za Sekretarieti
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Wanachama wa Afrika Mashariki (AMECEA), Askofu Charles Sampa Kasonde, katika ziara yake ya kikazi katikaSekretarieti ya AMECEA, iliyoko Nairobi Kenya amewashukuru wafanyakazi kwa kujitolea hata katika kipindi cha janga la UVIKO- 19. Akiwahutubia wafanyakazi hao mnamo Alhamisi, tarehe 19 Mei 2022, Askofu Kasonde alisema kwamba pamoja na Janga la UVIKO- 19 ambalo lilikwamisha shughuli nyingi katika kanda, nzima yeye binafas anafurahi kusema kwamba kazi yao ya kujitoa na uwajibikaji kunaonekana vizuri katika kwa mikutano yao yote. Wao wameweza kuendesha Mikutano na kutekeleza vyema baadhi ya program na kuendesha Sekretarieti bila kujali changamoto waliweza kuishi kulingana na matakwa ya maaskofu wa AMECEA. Askofu Kasonde wa Jimbo Katoliki la Solwezi nchini Zambia, alieleza kwa maana hiyo hisia zake kwa wafanyakazi wa Sekretarieti wakati wa ziara yake, wajibu wake kwamba ni kuthamini kile walichofanya na kuwatia moyo kuendelea kufanya vyema wawezavyo.
Kutekeleza maazimio ya AMECEA
Katika Tovuti ya AMECEA, Sr. Jecinter Antoinette Okoth, FSSA; anahabarisha kwamba Askofu Kasonde akiwakumbusha wafanyakazi wa AMECEA kutambua wajibu wao kama kitovu cha kuratibu cha Kanda, Mwenyekiti alizungumza kwa kuwahusu Mabaraza 8 ya Maaskofu yanayounda kanda hiyo kwamba wao wanatakiwa kuwa na mabawa manane ya kufanyia kazi hasa wanapojaribu kuendelea kuingiliana na mikutano yote. Kama Sekretarieti, mara kadhaa wamekuwa wakishirikiana na Mikutano husika ili kuhakikisha kuwa mipango ya AMECEA, hasa maazimio yanatekelezwa. Kwa maana hiyo Mwakilishi huyo ambaye amekuwa mwenyekiti wa AMECEA hivi karibuni 2018 aliweza kuwahimiza washiriki wa mkutano huo ili kuendelea kufanya ufuatiliaji wa ufanisi wa maazimio yaliyotekelezwa.
Uhusiano na wanachama wa SECAM, Ofisi za Balozi wa Vatican na Ofisi ya KCCB
Askofu Kasonde aidha, kwa kuongezea aliwahimiza watumishi wa Sekretarieti kuendeleza uhusiano na kushirikiana na Mabaraza wanachama wa kanda, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar (SECAM) ambapo kanda ya AMECEA ni mwanachama, Ofisi ya Ubalozi wa Vatican na Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, KCCB ambayo ofisi yake iko karibu na sekretarieti kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi pamoja kama familia moja na Kanisa zima. “Tutumie uhusiano ambao Mungu ametupatia ili kuimarisha kuwa kwetu hapa na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi, na tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu katika eneo hili alisema mwenyekiti huyo. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa AMECEA Padre Anthony Makunde alimweleza mwenyekiti huyo kuhusu mbinu za kufanya kazi ambazo sekretarieti hiyo imeitumia kama nguzo zake kwa miaka minne iliyopita.
Njia ya kupanda moyo wa kufanya kazi
Njia moja ambayo wametumia ni kupanda ule moyo wa kufanya kazi pamoja, alisema huku akifafanua kuwa idara katika sekretarieti hiyo zimekuwa zikifanya kazi kwa mshikamano kwa ajili ya kufanikisha mipango mbalimbali ya mikutano hiyo. Hata hivyo kando na roho ya mshikamano, Padre Makunde alisimulia kuwa wafanyakazi wa Sekretarieti wamekuwa wakikumbushwa kukumbuka kuwa AMECEA inavuka Sekretarieti na kwamba ni Mikutano minane kwa pamoja. Kwa kufafanua zaidi, alisema kwamba njia hiyo ilikuwa ya kuwasaidia kuondoka na kukutana na wengine katika Mikutano ya wanachama ambapo AMECEA inapatikana lakini kwa kukatizwa kwa UVIKO-19, hawakujiorodhesha sana katika mbinu hiyo. Hata hivyo alishukuru kwamba tayari roho hiyo imepandwa na jambo ambalo litawasaidia hata siku za usoni. Kwa kuhitimisha Katibu Mkuu wa AMECEA alisema wajumbe wa Sekretarieti wanafahamu kuwa wao ni vyombo na vyombo vya maaskofu hivyo wajibu wao ni kuongeza thamani na kuwa mali katika kanda nzima.