Tafuta

Kusikia kwa sikio na kusikiliza kwa moyo.  Kusikia kwa sikio na kusikiliza kwa moyo.  

Maaskofu,Hispania:Unawasiliana ikiwa unasikiliza kwa moyo

Dominika 29 Mei ni maadhimisho ya Kupaa kwa Bwana,sambamba na Siku ya 56 ya Upashanaji habari Ulimwenguni,ambapo maaskofu wa Hispania wametoa ujumbe ambao unakumbusha maneno ya Bwana kwa Mitume:“Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri Injili kwa watu wote duniani”na wakisisitiza jukumu la lazima la mawasiliano kwa ajili ya maisha kamili.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Katika ujumbe uliotolewa na Tume ya Maaskofu ya Mawasiliano ya Kijamii, yenye kichwa “Tunawasiliana kwa dhati tunaposikiliza kutoka moyoni”, maaskofu wa Hispania wakumbusha kwamba “sote tunahusika katika mawasiliano, sote tunashiriki utume huu, kwa njia moja au nyingine, kwa sababu kuishi katika uhusiano ni kuishi katika mawasiliano”. Hata hivyo, yeyote anayesikiliza tu hawasiliani, na anayezungumza tu hawasiliani. Kiukweli, kuna haja ya nyanja zote mbili. Ili kusikiliza ni lazima mtu azungumze  na  mtu asambaze, lakini ili kuzungumza kwa ukamilifu ni lazima kusikiliza kwanza. “Ni kwa njia hiyo tu ndipo yanaweza kutolewa mazungumzo yanayohuisha jamii na kuifanya ikue.” Kama Papa, ambaye katika ujumbe wake kwa Siku ya Upashanaji habari  Ulimwenguni, alisisitiza kusikiliza na kupendekeza kusikiliza kwa sikio la moyo”, maaskofu wa Hispania pia wamesisitiza kwamba mawasiliano ni ya kweli, na  hutokea wakati mwingine unabadilishwa na hii inahitaji kusikiliza kwa moyo kama  Papa Francisko anavyozungumza.

Safari ya sinodi iko katika muktadha wa kusikiliza

Hata safari ya sinodi ambayo Kanisa linaendelea nayo katika kipindi hiki, kwa upande wa maaskofu wanathibitisha, kwamba imewekwa katika muktadha huo wa “kusikiliza”, ili kupelekea “kutambua njia ambazo Kanisa linapaswa kuzifuata katika utume wake wa Kiinjili”. Na kuna mazungumzo ya kusikiliza  ambayo sio tu kwa wale wanaoshiriki katika maisha ya Kanisa, kwa wale ambao ni washiriki au wale wanaopokea msaada wake, lakini, zaidi ya hili, kusikiliza kila mtu. Kila mtu  anaweza “kujifunza kutoka kwa njia hii ya sinodi ambayo inafanya kusikiliza na kupambanua kuwa utamaduni mpya kwa wakati mpya”, katika jamii hii ambayo mara nyingi imejaa maneno mengi, ambayo “haijaribu kusikiliza au kuelewa mwingine na hiyo” iliyokithiri ni matamshi ya chuki, yanayotokea mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii, ambayo humdharau mtu huyo, kumdhalilisha na kumtupilia mbali,  wanasisitiza  viongozi wa Kanisa la Hispania.

Kujaza tumaini la siku zijazo

Kwa hiyo, pendekezo la Kanisa ni lile la “kusikiliza kwa moyo kwamba linenapo halitukani, halisingizii, halidanganyi, halilazimishi au kusaliti, bali linakuja kuchangia na punje yake ya mchanga kwa ajili ya ujenzi wa manufaa ya wote. Ili kusikiliza kwa moyo ni muhimu kumsikiliza Mungu na nyakati, hata jamii ambayo mtu anaishi”. Ujumbe wa Maaskofu aidha unabainisha kuwa “Kumsikiliza Mungu, tunagundua kwa hakika kile anachotaka katika maisha yetu na mahali anapotugawia katika ujenzi wa manufaa ya wote. Kumsikiliza Mungu hakutegemei maisha ya kibinafsi tu  lakini kuyaangazia, kuyapa upeo na maana, kuyajaza na tumaini na siku zijazo. Na kwa kuwa Mungu pia huzungumza nasi kupitia ishara za nyakati, hata matukio ya siku zetu na “lazima yasikike na kueleweka”. Tunapoutazama ulimwengu na kuusikiliza kwa sikio la moyo, basi tunaweza kuwajali wale wanaoteseka, walio peke yao, wagonjwa, walio na huzuni na sio kupuuza mateso ya wanadamu”.

Papa ameomba mara nyingi kwa Bikira Maria

Kila wakati tangu kuanza kwa vita vya kipuuzi na  nchini  Ukraine, Papa  Francisko, kwenye katekesi au mikutano binafsi  hajaacha kuomba  kwa maombezi ya Bikira Maria ili kifo na uharibifu viweze kumalizika na suluhisho la kisiasa na kidiplomasia lipatikane. Ilikuwa Machi 24 wakati ombi kwa Mama Yetu kwa amani na tendo la kuwekwa wakfu kwa ubinadamu, hasa Urussi na Ukraine kwa Moyo Safi wa Maria, katika saa ya giza la ulimwengu, ilileta pamoja mamilioni ya waamini. Na tena katika katekesi zake na sala za Malkia wa Mbingu , vile vile akiwasalimu waamini kutoka sehemu zote za dunia, wa Pompeii hadi Jasna Gora, Poland Papa Fransisko hakuchoka kurudia “kumwamini Mariam” na kumuomba.

Lengo la kuwasiliana kwa waandishi ni kufanya hata mateso yajulikane

Maaskofu nchini Hispania kwa hiyo, wakiwaelekea wataalam wa mawasiliano,  wamethibitisha kwamba lengo la wawasilianaji ni “kufanya mateso yajulikane ili yaweze kukabiliwa. Kwa sababu hii, mahali pao mara nyingi ni miongoni mwa watu wasio na uwezo na, katika hali nyingine, hii inawagharimu maisha yao”. Katika sehemu ya mwisho ya ujumbe, maaskofu wanawashukuru wale ambao wamesikiliza kwa mioyo yao  na wanaotoa uandishi wa habari bila upendeleo unaosikiliza kwa dhati ukweli na sauti ya haki ambayo, kupitia kwao, inatolewa na kujulikan; na wanakumbuka wote waliokufa wakiwa katika kuwasilisha, kutekeleza taaluma adhimu na ya lazima ya uandishi wa habari, huko Ukraine, Mexico na katika migogoro mingi iliyosahaulika ulimwenguni kote.

26 May 2022, 17:30