Tafuta

Askofu Mkuu Justin Welby wa Kianglikani nchini Uingereza Askofu Mkuu Justin Welby wa Kianglikani nchini Uingereza 

Kanisa nchini Uingereza kuomba ladhi dhidi ya sheria kwa

Sinodi ya 1222 huko Oxford ilipitisha sheria zilizokataza maingiliano ya kijamii kati ya Wayahudi na Wakristo.Sinodi hiyo iliweka zaka maalum kwa Wayahudi na kuwataka wawe na alama maalum kama utambulisho.Baada ya miaka 800 iliyopita imefanyika ibada ya kuomba msamaha kwa Jumuiya ya Wayahudi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kanisa la Uingereza limeomba msamaha kwa jumuiya ya Wayahudi kuhusu sheria zilizopitishwa miaka 800 iliyopita na kuendelea, ambazo zilifungua njia ya kufukuzwa kwa wayahudi kutoka Uingereza kwa mamia ya miaka. Hayo yalisikika katika Ibada maalum ya kuadhimisha miaka mia nane ya Sinodo ya Oxford iliyolenga kuwahimiza wakristo kukataa aina za kisasa za chuki dhidi ya Uyahudi.

Sinodi ya 1222 huko Oxford

Ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kristo huko Oxford ambayo iliudhuliwa na viongozi wa serikali ya raia na viongozi wa dini, akiwemo Mkuu Wayahudi Ephraim Mirvis na wawakilishi wa Askofu Mkuu Justin Welby wa Canterbury, Uingereza. Sinodi ya 1222 huko Oxford ilipitisha sheria zilizokataza maingiliano ya kijamii kati ya Wayahudi na Wakristo, Sinodi hiyo iliweka zaka maalum kwa Wayahudi na kuwataka wawe na alama maalum kama utambulisho. Wayahudi pia walipigwa marufuku kutoka katika mahekalu fulani walizokuwa nazo na kujenga masinadogi  yao mapya. Aidha vikwazo na vizuizi vingine vikali viliendelea kuwekwa dhidi ya Wayahudi kwa miaka mingi, ambavyo vilisababisha kufukuzwa kwa takribani Wayahudi 3,000 wakati huo, kwa amri ya 1290 na mfalme Edward I.

Umuhimu wa kuomba msamaha

Kwa takribani ya zaidi ya miaka 360 ilipita kabla ya  Wayahudi kurejeshwa nchini Uingereza na Oliver Cromwell mnamo mwaka1656. Ingawa Kanisa la Uingereza liliundwa katika miaka ya 1530 wakati wa Mfalme Henry wa VIII alipojitenga na Papa, viongozi wa Kanisa la Uingereza wameweza kusisitiza juu ya umuhimu wa kuomba msamaha.  “Ibada ya leo ni fursa ya kukumbuka, kutubu na kujenga upya. Tuombe kwamba iwatie moyo Wakristo leo hii kukataa será za kisasa za chuki dhidi ya Wayahudi na kuthamini, kupokea zawadi ya majirani zetu Wayahudi. Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu Welby  katika ujumbe wake wa Twitter Diminika tarehe 8 Mei 2022 . 

Wakati umefika wa wakristo kutubu matendo ya aibu

Katika taarifa nyingine ya mwezi uliopita kabla ya hafla hiyo, Jimbo la Oxford lilibainisha kuwa, nia  ya kufanya maadhimisho haya ni kuwa ishara kubwa inayoakisiwa katika kina cha mkutano wa dini na huduma ambazo zinazidi kuwepo Oxford na katika jumuiya yote”. Akizungumza Bwana Onathan Chaffey, Shemasi Mkuu wa Oxford, alisema kuwa wakati umefika kwa Wakristo kutubu matendo yao ya aibu na kurekebisha vyema uhusiano wao na jumuiya ya Wayahudi. Pia alibainisha kuwa Kanisa Katoliki lilikubaliana na msamaha huo.  Ibada ya Misa hiyo maalum  inafuatiwa na hatua nyingine za kukuza nia njema na jamii ya Wayahudi katika miaka ya hivi karibuni. Mnamo mwaka wa 2019, hati ya Kanisa la Kianglikani  lenye jina la “Neno la Mungu lisiloshindwa” ilionesha umuhimu wa uhusiano wa Kikristo na Kiyahudi na kuwahimiza Wakristo kupinga kikamilifu chuki dhidi ya Wayahudi.

13 May 2022, 22:06