Brazil:Juma Kuu Takatifu linafundisha kupeleka upendo wa Kristo
Na Sr. Angella Rwezaula- vatican.
Kuishi Juma Kuu ni kwa ajili ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu, ambalo ni tendo la hitimisho la maisha ya Kikristo na kwa maana hiyo waamini wote na wenye mapenzi mema nchini Brazil wanaalikwa hata kuishi kupindi kikubwa hiki cha mwaka. Amesema hayo Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo, wa Jimbo Kuu Katoliki la Belo Horizonte na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Brazili. Kuishi ni mwaliko wa upendo katika maisha yetu ya ndani. Yesu, Mwana wa Mungu awezaye yote, anakabiliana na uchungu mkali sana na anakufa kwa ajili ya kutuokoa; anatufundisha kuwa maisha yana maana tu ikiwa yanakuwa sadaka kwa ajili ya wema wa jirani.
Askofu De Azevedo amesema “Wakati maisha yanakuwa sadaka inayojikita juu ya upendo, unashinda hata kifo, maisha yanga’aa na ndio anatufundisha Kristo Mfufuka. Katika ujumbe wake kwa njia ya video, Askofu mkuu amesisitiza, kwamba msingi wa mafundisho ambayo yamo katika Juma Kuu Takatifu, ndiyo, kwa hakika mwaliko wa kupeleka upendo wa Kristo ndani ya maisha yetu na kujikita baadaye kwa udugu wa ulimwengu.
Maisha yetu yageuke kuwa sadaka ya upendo
Ikiwa maisha ya kila mtu yanageuka kuwa sadaka ya upendo hakutakuwa na ugomvi kwa sababu ya kutoelewana ambako ni kwa kawaida , hasa katika kipindi cha uchaguzi (Nchini Brazil Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2022), kuibuka kwa vita kutaacha nafasi ya Amani. Ubinadamu hautakuwa na tabia za kutojali uchungu wa kaka na dada. Kwa mujibu wa Rais wa Maaskofu amesema kila mmoja atashiriki sehemu yake, ulimwenguni hatimaye kutazaliwa Amani sintofahamu za mahitaji ya jirani hazitakuwapo. Juma Kuu na upendo wa Yesu Mfufuka, uwezeshe kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa ulimwengu wa haki zaidi, wa mshikamano zaidi na udugu na ndiyo ilikuwa ni matashi mema ya siku kuu.