Iraq:Kard Sako,Mwanga wa Pasaka ya Kristo uangaza giza katika nyakati za vita
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Louis Raphael Sako, Patriaki wa Kanisa la Wakaldayo ametoa ujumbe wake wa Pasaka uliochapishwa kwamba: Katika Kipindi cha Pasaka ambacho mwaka huu kinaendana na sehemu ya Mfungo wa Ramadhani kila mwaamini katika Mungu na kwa namna ya pekee wakristo lazima wakatae mantiki ya vifo katika vita”. Patriaki anawaalika wakristo watazame ufufuko wa Kristo kama mwanga pekee ambao unaweza kuangaza katika giza la wakati huu uliogubikwa na vita vya kidunia. Akitazama hasa juu ya vita, vilivyoenea ulimwengu, Patriaki amewaeleza waamini wote, wakristo na waislamu ambao kwa sasa wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hata Wayahudi wote, kutazama janga la vita nchini Ukraine na katika Nchi ya Mashariki ya kati kama udhalilishwa na uharibifu wa majengo yao mazuri.
Ni Kristo mfufuka aliyekuja kwa ajili ya wokovu wetu
Kardinali Sako amesema: “Leo hii kuliko hapo awali, maadhimisho ya Pasaka yanawakilisha fursa muhimu ili kujua kwamba hata katika kipindi hiki upendo wa Mungu kwa watu, ukaribu wake na huruma yake isiyo na kikomo kwa wote , ambao anauonesha kwa njia ya ufufuko wa Kristo aliyekuja kwa ajili ya wokovu wa ubinadamu”. Ufufuko wa Kristo unakuja kuangaza wale ambao wako katika giza na kivuli cha mauti, kuongoza nyayo zetu katika njia ya amani, amekumbusha Kardinali Sako, akirudia maneno ya wimbo wa Kiiinjili wa Zakaria, baba yake Yohane Mbatizaji. Ni ufufuko wa Kristo ambaye anafanya kuchanua ishara za bure za upendo kwa ndugu na kukukaribishana mmoja na mwingine kama ilivyojitokeza kwa mitume wa Yesu, ambao waliunganika kwa pamoja mara baada ya Ufufuko wake na walishirikishan upendo kwa kila kitu walichokuwa nacho.
Suluhisho la kivita kwa njia ya mazungumzo ya kidiplomasia
Lakini je ni kwa nini thamani za kiroho za kikristo zimepotea katika sehemu kubwa ya jamii ya sasa, kuanzia na ile ya Mashariki, ameuliza swali. “Je tumeweka wapi mafundisho ya Kristo ambayo alituita kupenda wote, wakijumuishwa adui?” Kanisa linaalikwa kuongoza usasa ambao unaunda maisha ya jamii zetu katika mwanga wa Injili. Ikiwa hili halitokei na ikiwa hili haliwi tunu ya mwanga ule, hata mipango mingi ya kikanisa inaishia kutozaa matunda. Akigusia tena juu ya vita vya umwagaji damu vinavyoendelea katika moyo wa Ulaya Mashariki amesema Marais, Mamlaka za kidini, na jumuiya za kijamii, lazima kwa pamoja kusafanya kazi ili kusimamisha vita kati ya Urussi na Ukraine, ili kusuluhisha migororo kwa zana ya kidiplomasia badala ya kutumia silaha.
Matashi mema ya uwajibikaji wa sera za kisiasa
"Vita vikome. Waathirika, uchungu, uharibifu, uhamiaji, umaskini na magonjwa. Lazima kusitisha uzalishwaji wa silaha za maangamizi kila sehemu, na kila mtu awe mkweli wa kukataa kuzimu huko". Akizungumzia hata wazo kwa upande wa taasisi za kisiasa, zilizoundwa huko Iraq baada ya uchaguzi mwezi Oktoba, Kardinali Patriaki Sako, ametoa matashi mema akiwatakia sera za kisiasa ziweze kuchukua uwajibikaji wake mbele ya hatima ya taifa. Amehimiza waweze kuchukua mtindo wa lugha ya mazungumzo, ya maelewano pamoja ambayo ndiyo njia pekee ya kuondokana na wasiwasi na kuunda serikali ya kitaifa, yenye uwezo wa kujikimu katika dharura na hekima katika mageuzi ya lazima ili kuokoa uchumi na maelewano ya kijamii ya nchi.