Ujasiri na amani ndiyo matashi mema ya Pasaka kutoka kwa Maaskofu wa Poland
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika fursa ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, Askofu Mkuu Gądecki wa Jimbo Kuu Katoliki la Poznań, nchini Poland amechapisha ujumbe wakekatika Tovuti ya Baraza la Maaskofu akiwageukia wapoland nchini humo na wale walioko nchi za nje, ikiwa ni pamoja na wakimbiz ambao wanaishi kipindi hiki kwa cha siku kuu katika nchi yao kutokana na vita nchini mwao ili wasikate tamaa. Askofu Mkuu anaandika kwamba: “Katika wakati huu mgumu uliotokana na vita nchini Ukraine, watu wengi wamekumbwa na wanateseka na mbele ya macho ya ulimwengu wote, na kwa maana hiyo ni matashi mema kutoka kwetu ili wawe na ujasiri na amani”.
Imani, tumaini na upendo
“Bwana mfufuka ajaze mioyoni mwetu imani, matumaini na upendo ili tuweze kuadhimisha muujiza wa asubuhi ya Pasaka, kwa kuwa na imani kuwa Yeye alishinda ubaya, hata ule ambao umekumba ulimwengu wa kisasa”. Askofu ameongeza kuandika kuwa uzoefu wa fumbo la Pasaka unasaidia kukumbatia kwa uthabiti Kristo ambaye analeta wokovu na wakati huo huo kuwa shuhuda wa upendo wa huruma.