Papa Francisko anakutana na vijana wa Italia Jumatatu 18 .04.2022 Papa Francisko anakutana na vijana wa Italia Jumatatu 18 .04.2022 

Papa Francisko anakutana na vijana wa Italia jijini Vatican

Katika siku kuu ya Jumatatu ya Pasaka iitwayo ya Malaika,maelfu ya vijana wamefika katika hija jijini Roma wakisindizwa na maaskofu na viongozi wao.Ni tukio kubwa sana la kitaifa jijini Vatican tangu kuanza kwa janga la uviko. Jioni kutakuwa na mkesha ambapo kutakuwa na kusikiliza historia za vijana kuhusu Injili ya Yohane na maneno ya Baba Mtakatifu kwa vijana.

Na Angella Rwezayla - Vatican

Ni zaidi ya vijana hamsini elfu kuanzia wenye umri wa miaka 12 hadi 17 kutoka Italia yote  wakiongozwa na maaskofu 60, pamoja na makumi ya mapadre, watawa na wahusika wakuu wa vijana , vyama, harakati na jumuiya. Hawa wanaongozwa na kauli mbiu ‘Nifuate, hija ya Roma ya vijana’. Ni kutaniko lililoandaliwa na Baraza la Maaskofu Italia ambapo Jumatatu tarehe 18 Aprili 2022 kwaoni kipindi muafaka cha kukutana na Papa Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Vijana wakijiandaa kukutana na Papa Jumatatu ya Pasaka 2022
Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu
Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu

Saa 6 kamili wameungana na Baba Mtakatifu kusali sala ya Malkia wa Mbingu. Hawa ni vijana waliofika kwa mabus na treni ili kuweza kufika Roma mapema asubuhi sana na wengi walifika kabla na kukaribishwa na maparokia mengi ya Roma. Shauku ya vijana ni kubwa isio na kifani. Janga kwa hakika limegusa kila sehemu hasa katika ukawaida wao wa kila siku japokuwa haukuzima shauku hiyo ya nguvu itokayo ndani na wanataka kuionesha ili hata watu wazima labda wanaweza kuilewa.

Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu
Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu

Kwa maana hiyo wamefanya hija kutoka Italia nzima kufika Roma ili kuishi uzoefu wa muungano kidugu na wa imani. Huu umekuwa ni mkutano wa kwanza wa Papa mjini Vatican na watoto wa Italia baada ya kusimama kwa muda mrefu kutokana na janga la uviko na ni muhimu kwamba umefanyika siku moja baada ya Pasaka, sikukuu inayoleta imani, inatia matumaini na ni ishara ya kuzaliwa kwa upya.  Pamoja na hija ya vijana jijini Roma na mkutano wao na Papa, ambao unataka kuwatia moyo na kutoa ishara za matumaini kwa wale wanaojitolea katika ukuaji wa watoto na wale wanaoitazama Jumuiya ya Kikristo kama walinzi wa maisha yajayo ambaye amezaliwa kwa imani katika Yesu Aliyefufuka”,  amesema hayo Padre  Michele Falabretti, mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya uchungaji wa  Vijana ya Baraza la Maaskfu Italia CEI.

Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu
Mkutano wa Vijana na Baba Mtakatifu

Kwa kufafanua zaidi kuhusiana na tukio hilo amesema “Wakati huu unaendelea kutujaribu  hatutaki kuacha hisia ya uwajibikaji kwa heshima na shughuli za kielimu ambazo zimekuwa zikionesha uchungaji wa kawaida wa majimbo yao. Mpango huo umeona kwa hakika vijana wanahija kushiriki sala ya Baba Mtakatifu ya Salamu Malkia katika.  Na wakati huo huo jioni shughuli yao kuanzia saa 11.30 Papa ataingia katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuwasalimia vijana wote akizungushwa na kigari. Baada ya salamu kwa washiriki wote, kusikiliza na kutafakari Injili ya Yohane 21 wataanza mkesha wa sala, mazungumzo kati ya vijana na pia hotuba yake, sala ya imani na tukio hilo linatarajiwa kumalizia saa moja usiku.

18 April 2022, 11:52