Mkusanyo wa sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu ni tumaini la Wakristo wa Mashariki
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tumaini kwa ajili ya mustakabali wa Wakristo wa nchi za Mashariki”: hivi ndivyo Msimamizi wa Nchi Takatifu, Padre Francesco Patton, anavyofafanua kuhusu mkusanyo wa Fedha kwa ajili ya Nchi takatifu katika ujumbe wake wakiutamaduni, uliochapishwa tarehe 29 Machi 2022 kwa matazamio siku ya Ijumaa Kuu Takatifu tarehe 15 Aprili mwaka huu. Padre Patton amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida kama ile ya miaka miwili iliyopita Wafransisko walio chini ya ulinzi wa Nchi Takatifu wamejaribu kuendeleza utume wao. Katika madhabahu yasiyo na mahujaji, wamezidisha maombi, wakitoa sauti kwa kilio cha ubinadamu wote. Dhamira ya Uhifadhi iliendelea katika parokia ambapo waliendelea kusherehekea na kuwa karibu na watu, waamini wa ndani, wafanyakazi wahamiaji na wakimbizi, shuleni ambapo walijaribu kuelimisha katika udugu na matumaini. Katika vituo vya masomo walikaribisha na kutoa mafunzo kwa mapadre vijana, lakini pia makuhani, watawa wa kike na kiume watu wa kawaida walei kutoka ulimwenguni kote.
Padre Patton amesema kwamba kwa shida walimejaribu kuzisaidia kwa hali na mali jumuiya dhaifu zaidi: jumuiya za Bethlehemu na zile za Yerusalemu, zisizo na mahujaji tena na kazi; jumuiya za Lebanon, zilizoharibiwa na mzozo wa kiuchumi na kisiasa unaozidi kuwa mbaya; wale wa Siria, wafungwa wa vita ambavyo vinaonekana kutoisha. Kwa hivyo wito kwa waamini ni kuchangia. Pia mwaka huu katika siku ya Ijumaa Kuu, Padre Patton anasema wakumbuke kaka na dada wote wanaoishi katika Nchi Takatifu. Wasaidie kwa kadiri ya ukarimu wa moyo wa kila mtu, kwa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu: 'Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko kupokea'.
Mkusanyo wa sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu ni tumaini la mustakabali wa Wakristo wa Mashariki
Mkusanyo wa sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu, pia unajulikana kama ‘Collecta pro Locis Sanctis’, ulizaliwa kutokana na mapenzi ya mapapa ili kudumisha uhusiano wenye nguvu kati ya Wakristo wote duniani na Mahali Patakatifu. Kiutamaduni na kimapokea inakusanywa katika siku ya Ijumaa Kuu, ambayo inawakilisha chanzo kikuu cha riziki ya maisha ambayo hufanyika karibu na Mahali Patakatifu. Sadaka inayokusanywa na Parokia na Maaskofu wa Makamishna wa Nchi Takatifu kwenye usimamizi wa Nchi Takatifu ambayo utumika kwa ajili ya matengenezo ya Maeneo na kwa ajili ya Wakristo wa Nchi Takatifu. Kwa njia ya Mkusanyiko, wa sadaka, usimamizi wa Nchi Takatifu unaweza kusaidia na kutekeleza utume muhimu unaoitwa: “kulinda na kuhifadhi Mahali Patakatifu, mawe ya Kumbukumbu, na kuunga mkono uwepo wa Kikristo, ambayo ni mawe hai ya Nchi Takatifu, kupitia shughuli nyingi za mshikamano. Usimamizi wa Nchi Takatifu upo pamoja na mapadre Wasimamizi 300 katika Israeli, Palestina, Jordan, Siria, Lebanon, Misri, Cyprus na Iraq, Ethiopia, Eritrea, Uturuki, Iran. Daima umekuwa karibu na idadi ya watu walioathiriwa na vita, magonjwa ya milipuko na majanga mbali mbali kama vile la sasa la UVIKO-19
Historia ya Sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu
“Nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue zawadi yenu mpaka Yerusalemu. (1 Kor 16,3). Kwa sentensi hiyo Sadaka kwa Ajili ya Nchi Takatifu (Pro Terra Santa) ni mojawapo ya mkusanyo wa lazima (pamoja na Sadaka kutoka Mfuko wa Mtakatifu Petro wa tarehe 29 Juni na Siku ya Umisionari Ulimwenguni) na ile ambayo uweza kufanyika katika siku ya Ijumaa Kuu (au tarehe ambayo watu wa kawaida wanaona inafaa zaidi) kwa neema ya kazi na mahitaji ya Nchi Takatifu. Katika Wosia wa Kitume wa Papa Paulo VI, wa tarehe 25 Machi 1974, juu ya kuongezeka kwa mahitaji ya Kanisa katika Nchi Takatifu, taratibu za Mkusanyiko zilibainishwa.
Namna ilivyo anzishwa sadaka hii
Katika karne zilizopita, Mapapa sio tu kwamba wamepyaish imani yao kwa Wafransisko, wakiwathibitisha tena katika nafasi ya kuwa wasimamizi halali wa Mahali Patakatifu (waliokabidhiwa na Kiti cha Kitume mnamo 1342), lakini pia wamewaunga mkono katika kila nyanja ya maisha yao hadi ngazi ya kidini, kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ingetosha kukumbuka idhini ya kufanya mazoezi ya matibabu katika Nyumba ya Mlima Sayuni kwa ajili ya wagonjwa na wahitaji n, katika karne zilizofuata, mapendeleo, msamaha, ulinzi wa haki zao. Zaidi ya Hati mia moja za kipapa zilirejea Nchi Takatifu, pamoja na idadi sawa ya dikrii na barua kutoka kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishai wa Watu ambalo linasaidia wana wa Mtakatifu Francis katika Utume wao Nchi Takatifu.
Kipengele muhimu cha usaidizi huu unaoendelea kilikuwa, na bado ni, Mkusanyo kwa ajili ya Ardhi Takatifu, inayojulikana pia kama Collecta pro Locis Sanctis. Alikuwa ni Papa Paulo VI ambaye, kupitia waraka wake wa kitume Nobis wa tarehe 25 Machi 1974, alitoa msukumo wa uhakika katika kupendelea Nchi Takatifu. sanjari na watangulizi wake, Papa alisifu kazi ya Wafransiskani na kusisitiza juu ya hitaji la ushirikiano zaidi kutoka katika ulimwengu wa Kikristo, kwani, hasa tangu mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa, Wafransiskani walikuwa wameongeza shughuli zao za kijamii, za upendo, na kiutamaduni katika Nchi Takatifu na Wakristo wa huko wakati mwingine wakikosa njia. Papa Paul VI, baada ya kusema kwamba katika historia Ndugu Wadogo wameshughulikia moja kwa moja wawe wakubwa ay wadogo kwa unyenyekevu kukusanya misaada, na wale wa kitawa waliokusudiwa kwa kazi hiyo waliopokea jina rasmi la Mawakili au Makamishna wa Nchi Takatifu, alikumbuka kwamba katika nyakati za sasa mahitaji yameongezeka na kwa hiyo Mapapa wamechukua jukumu la Mkusanyo ya sadaka kwa ajili ya"pro Terra Sancta" yaani Nchi Takatifu.
Papa Paulo VI alizifanya upya kanuni zilizotolewa na watangulizi wake na katika mawaidha ya kitume aliweka kanuni za mkusanyo huo. Katika miongo kadhaa iliyopita, Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki limekuwa na shauku ya pekee kwa upande wa Vatican katika kudhihirisha mahitaji ya Nchi Takatifu na sheria zilizotolewa na Papa Paulo VI, zikiwemo zile zinazorejea Tume mbali mbali. Katika miaka ya hivi karibuni, asilimia 80 ya makusanyo yaliyopokelewa na Wafransiskani yamekusudiwa kwa ajili ya kazi za kichungaji na kijamii na asilimia 20 tu ya madhabahu. Ni muhimu kukumbuka kwamba chini Usimamizi hupokea asilimia 65 pekee ya michango, wakati asilimia 35 iliyobaki inaelekezwa kwa taasisi zingine zinazofanya kazi katika Nchi Takatifu. Shughuli za Upatriaki wa Kilatini, kwa agizo la Vatican, zinaungwa mkono na Shirika Kijeshi la Kaburi Takatifu na taasisi zingine.