Marekani:Mwaliko wa Maaskofu kuhusu mchango wa ufadhili wa Makanisa ya ndani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni majimbo na Makanisa ya Upatriaki ya Marekani ambayo hayajiwezi kuendesha shughuli zake na kwenda mbele bila ufadhili kutoka nje, ambayo yatawezeshwa kwa mwaka huu kutoka makusanyo ya sadaka katoliki kwa makanisa hayo ya ndani, kati ya tarehe 23 na 24 Aprili 2022 ijayo katika eneo lote nchini Marekani. Kama ilivyo kawaida ya kila mwaka sadaka hiyo itakayolisanywa na kuwekwa kwenye mfuko wa Tume y ya utume wa Ndani ya Baraza la Maaskofu wa Marekani.
Fedha ni kwa ajili ya jumuiya zilizotawanyika
Katika mfuko huo, parokia mbali mbali zinashirikishana baraka zao na wakatoliki wengine ambao wanaishi katika jumuiya ndogo sana za watu katoliki zilizotawanyika katika maeneo mengine na mengine makubwa au ya mbali na mengi hayo yana wakatoliki lakini hawana namna ya kujitosheleza kwa mujibu wa Maelezo ya Askofu W. Shawn McKnight, wa mji wa Jefferson na rais wa Tume ya Maaskofu wa Marekani kwa ajili ya Utume katoliki wa ndani. Akiendelea na maelezo amebainisha kwamba anapenda kila mkatoliki ajue wema mkubwa ambao unafanyika kwa njia ya zawadi zao. Ukarimu wao unawawezesha watu kuona ambavyo Yesu anavyoendelea kupelekea upendo na uponyaji kwa njia ya Kanisa aliloanzisha.
Mnamo 2021 walikusanya zaidi ya dola milioni 9
Mnamo mwaka 2021 kwa usahihi walikusanya sadaka ya dola milioni 9,3 na shukrani ya makusanyo hayo maalum waliweza kuzigawanya katika majimbo 76, na upatriaki huko Marekani. Vile vile kwa sababu ya sadaka hiyo, wanawezesha kusaidia shughuli za uinjilishaji na mafunzo ya kuimarisha imani na maisha ya binadamu yenye hadhi, kwa kuongeza nguvu za wenye ndoa na familia, miito ya kikuhani na watawa, wahudumu wa watu wa Hispania, watu wa Asilia wa Marekani na wale wa Alaska na usaidizi wa majimbo na maparokia yenye uhitaji zaidi wa uchungaji maalum.
Mkusanyo wa sadaka hata kwa kusaidia utume wa bahari na wakimbizi
Kati ya mipango ya mkusanyo huo wa mwaka kuna hata baadhi muhimu, kwa mfano huduma ya mabaharia na wavuvi wa Visiwa wa Marshall ambapo wanatoa huduma ya kijamii, kichungaji na sakramenti kwa mabaharia ambao wanaweza wasione hata familia zao kwa miaka. Huko Gallup, kinyume chake majimbo yanashindwa kuandaa elimu ya dini kwa juma kwa ajili ya watoto , ambapo kawaida huandaa kambi ya kiangazi kwa juma tatu za mafunzo ya imani na kwa miaka iliyopita ilileta mafanikio makubwa. Upatriaki wa Kimelkiti wa Newton huko Massachusetts, ambao unafunika Marekani yote, unatoa shukrani kwa sadaka hiyo, huduma ya kiroho na sio ya wakimbizi wa vita nchini Siria tu. Hatimaye wanachangia hata ununuzi wa vifaa vya mawasiliano ya elimu ya dini kwa ajili ya Shule za De La Salle Blackfeet ya Jimbo la Helena, ili kuongeza nguvu za shughuli za uinjilishaji huko Montana. Zawadi kwa jili ya mfuko Katoliki wa Utume wa Ndani zinaongeza imani ya wakatoliki kati ya watu wa nchi yao ambao wana zana duni kwa kusaidia huduma msingi. Kwa maelezo na kuhimitimisha Askofu Mkuu McKnight.