Kituo cha Astalli:Wakimbzi wameongeza mara mbili wanaopitia njia za bahari
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Pamoja na vita nchini Ukraine, idadi ya watu waliokimbia makazi yao duniani itafikia milioni 90. Idadi ya kutisha iliripotiwa tarehe 13 Aprili na Padre Camillo Ripamonti, rais wa Kituo cha Astalli, ambacho ni ni cha Wajesuit wakati wa uwasilishaji wa Ripoti ya Mwaka ya 2022 ya Huduma ya Wakimbizi ya Jesuit, iliyoko Roma. Hadi sasa, kwa kuzingatia takwimu kutoka katikati ya 2021, inakadiriwa kuwa wakimbizi na watu waliohamishwa wanafikia karibu milioni 84, ikilinganishwa na zaidi ya milioni 82 katika mwaka uliopita. Katika wiki chache tu, wakimbizi wengi wa Ukraine walifika kuliko wahamiaji na watafuta hifadhi ambao walifika mnamo 2021.
Kwa maana hiyo vita vya Ukraine, ripoti inasisitiza, inaonesha kuwa uwepo huu hauwakilishi uvamizi, wala tishio kwa usalama wao. “Dharura tunayokumbana nayo nchini Ukraine inatufanya tufikirie juu ya dharura nyingine nyingi ambazo zimewahi kutokea duniani. Tayari tumesahau hali ya Afghanistan mnamo Agosti 2021 na vita katika Pembe ya Afrika. Kwa hivyo, dharura nyingi ambazo ni sehemu ya vita hivyo vya ulimwengu vilivyoendelea na ambavyo Papa Francisko mara nyingi anazungumzia juu yake ”, amesema Padre Camillo Ripamonti, rais wa Kituo cha Astalli akifafanua na vyombo vya habari Radio Vatican.
Katika kipindi cha mwaka 2021, ripoti bado inabainisha kwamba idadi ya wahamiaji wanaowasili kwa njia ya bahari imeongezeka maradufu, ikihesabiwa kuwa jumla ya zaidi ya 67,000. Kati ya hawa, watoto ambao hawajasindikizwa walikuwa chini ya 9,500. Kituo cha Astalli kinaandika juu ya ongezeko la mateso na dhuluma wanayopata wale wanaokaribishwa katika kituo hicho. Mfano mzuri unahusu wanawake waliofuatiliwa na huduma ya magonjwa ya wanawake, zaidi ya 200 mwaka 2021, ambao wengi wao waliteswa, unyanyasaji wa kijinsia au unyanyasaji mwingine, katika nchi za asili au walipokuwa safarini. Matukio ya wale ambao wameishi gerezani nchini Libya, ambao karibu kwa kauli moja wanaripoti unyanyasaji, ghasia na mateso pia ni ya kushangaza.
Ikiwa mnamo 2021 Ulaya haikuweza kupata sera ya kuona mbali na inayojumuisha juu ya uhamiaji, kwa mujibu wa kituo cha Astalli, nchini Italia, miaka miwili baada ya amri za usalama, dharura bado haijatokea, ambayo athari zake zina uzito na ambayo yamezidisha udhaifu wa wakimbizi na kutengwa kwa jamii. Hata leo, takriban wahamiaji wawili kati ya watatu wanakaribishwa katika Cas, Vituo vya vya Mapokezi maalum. Urasimu wa kuchukiza, uliochangiwa zaidi na hatua zinazohitajika kudhibiti janga la uviko haujazingatia ugumu wa watu dhaifu na umeishia kuwatenga wale ambao wangehisi kujumuishwa na kukaribishwa haraka.
Moja ya vikwazo vya kwanza vya kupata ulinzi wa kimataifa, kama imekuwa katika miaka ya hivi karibuni, ni kupata usajili ambao ni muhimu kupata haki za kijamii. Uwekaji wa mfumo wa kidgitali wa ofisi nyingi, umewakilisha kuzorota kwa maisha ya wahamiaji wanaolazimishwa. Haja ya mpango wa kuunganishwa unazidi kuwa na nguvu, hata zaidi kutokana na kuendelea kwa janga la uviko, pia kwa kuzingatia juhudi kubwa za familia za wakimbizi ambazo haziwezi kutegemea mitandao isiyo rasmi, ya wazazi au ya marafiki.
Haikubaliki na ni aibu kwa ustaarabu wetu kwamba, katika Ulaya, tangu 2014, wahamiaji 24,600 wamepoteza maisha yao, hasa katika Mediterania. Hivi ndivyo, wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo, Kadinali Jean-Claude Hollerich, rais wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya, (Comece) alivyoingilia kati kwa njia ya video, kulingana na hali na unyanyasaji wanaokutana nao katika safari yao. , kama hali ya Libya inavyoonesha ambapo mateso, ukatili, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia ni mambo ya siku zote . Nchi za Ulaya kwa maana hiyo alisema haziwezi kushirikiana na mchakato huu wa kudhalilisha hadhi ya wahamiaji na wakimbizi ambao pia unawadhalilisha, akibainisha jinsi ya kuwa hawawezi kuwa watazamaji tu, mbele ya mabadiliko ya kienzi, ambayo inaonekana duniani kote. “Tuna wajibu wa kimaadili kukemea haya yote, kutaka mamlaka zetu zichukue kila mtu kibinadamu bila kujali hali yake ya kisheria” . Kardinali amesema Nchi zilizostaarabu haziwezi na huku akinukuu maneno ya Papa Francisko akiwa huko Malta kwamba vikwazo kwa maslahi yao binafsi katika mikataba mibovu na wahalifu wanaowafanya watu kuwa watumwa.