Brazil:Mkutano Mkuu wa Maaskofu kuhusu Kanisa la Kisinodi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baraza la Kitaifa la Maaskofu chini Brazil (CNBB) limefungua Jumanne 26 Aprili Mkutano Mkuu wa 59, kwa ajili ya awamu yao ya kwanza ya Mkutano ambayo inafanyika kwa njia ya Mtandao. Mkutano huo ni wa siku tano ambao unajumuisha na awamu ile ya pili, itakayofanyika kati ya 29 Agost na 2 Septemba kwa uwepo wa oja kwa moja huko katika madhabahu ya Mama Maria Aparecida. Mkutano wao mkuu unaongozwa na Mada ya “Kwa ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, ushiriki na utume” sambamba na mchakato mzima wa Makanisa katika kujiandalia na Sinodi itakayofanyika mjini Vatican kama ilivyoomba na Baba Mtakatifu Francisko.
Mkutano wao unataka kutoa kipaumbele kuhusiana na mada mbali mbali hasa kuanzaia na ripoti ya mwaka ya Rais wa Baraza hilo; Ripoti ya uchumi na masuala yanayotazama Tume ya maaskofu kwa ajili ya Liturujia, kuhusu utafsiri wa Maandishi ya kiliturujia (CETEL) na kwa ajili ya Mafundisho Tanzu ya Kanisa (CEPDF). Na mada nyinginezo kama therathini hivi zinazojikita katika masuala ya kila siku hasa umuhimu wa mawasiliano na uchunguzi wa hali halisi ya sasa ya Kanisa la Brazil lakini ambao hauna kula mbele ya maaskofu.
Maaskofu wataandaa vile vile mchango wao wa kuwakilisha kwa Papa kupitia Baraza la kipapa la Maaskofu na kwa watu wa Brazil. Matashi mema ya kwa maana hiyo ni kwamba mkutano uwe ni wenye utajiri wa uzoefu na matunda ya umoja, udugu na jitihada katika kutangaza Neno la Mungu umetolewa kutoka kwa Askofu Walmor Oliveira de Azevedo Rais na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Joel Portella Amado na ili uweze kutoa Jumuiya ya Kikanisa ya Kimisionari katika kila kona zote za nchi yao pendwa Brazil. Na kwa maombezi ya Mama Maria wa Aparecida awalinde katika huduma yao Maaskofu aidha wametoa sababu za kufanya mkutano wao kwa njia ya mtandao kuwa ni kutokana na busara ya kiafya ambayo bado inaendelea kuthibitiwa hadi sasa.
Na kwa kuwa wameanza matembezi ya kitume katika majimbo yao ni muhimu kubaki kwa muda mrefu katika majimbo yao. Na awamu ya pili ya Mkutano utafanyika katika Madhabahu ya Mama Maria huko Aparecida, ambapo utaangukia katika mwaka wa tatu katika eneo hilo. Itakuwa kwao ni kujishughulisha na masuala yanayohusu Muhimili wa Baraza hilo la Maaskofu Nchini Brazil CNBB na Sheria ya Kanoni, ambayo ni mantiki zinazohitaji uwepo kura za moja kwa moja. Aidha watakabiliana kwa mfano juu ya kukubaliwa kwa toleo la Tatu la Misale ya Waamini. Na kila siku Baraza la Maaskofu Brazil watatangaza mbashara maadhimisho ya Misa Takarifu ambayo pia ni sehemu ya Mkutano wao Mkuu, saa 1 asubuhi, masaa mahalia. Kila siku katika tovuti ya Maaskofu watatoa yaliyojiri ya Mkutao huo.