Tafuta

Viongozi wa Baraza la Makanisa Sudan Kusini Viongozi wa Baraza la Makanisa Sudan Kusini 

Sudan Kusini:Kubariki uwanja utakaodhimishwa misa ya Kipapa

Askofu Nyodho,mkuu wa kamati ya ziara ya Papa aliwaambia waamini kuwa nia ya kubariki uwanja mahali ambapo Papa Francisko ataadhimisha Ekaristi Takatifu ni kuomba ulinzi wa Mungu ili kazi na mahali hapo Baba Mtakatifu anapoitembelea nchi pawe patakatifu na utakatifu kwa watu wa Mungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maandalizi ya ziara ijayo ya Papa Francisko nchini Sudan Kusini mwezi wa Julai, uongozi wa Kanisa Katoliki hivi karibuni ulikusanyika pamoja kwa ajili ya kubariki uwanja ambapo ambapo Papa ataadhimisha misa na kuikabidhi nchi nzima katika ulinzi wa Mungu. Akizungumza katika Kumbu kumbu la John Garang huko Juba katika mji mkuu wa Sudan Kusini, ambako ziara hiyo ya siku tatu inatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 5-7 Julai 2022 Askofu Stephen Nyodho Ador Majwok wakati wa sherehe za baraka alisema: “Tunawakabidhi kila mtu ambaye atashiriki kazi hii kwa Mungu. Tunaiweka nchi yetu katika ulinzi wake wa kimungu na tunamwamini rais wetu na serikali wanaotusaidia kufanikisha mradi huu mikononi mwa Mungu.” Mkuu wa kamati ya ziara ya Papa  nchini Sudan Kusini,m Askofu Nyodho, aliwaambia waamini kwamba nia ya kubariki uwanja mahali ambapo Papa Francisko ataadhimisha Ekaristi Takatifu ni kuomba ulinzi wa Mungu ili kazi na mahali pawe mahali pa utakatifu na utakatifu kwa watu wa Mungu, wakati wa ziara ya  Baba Mtakatifu ya nchi yao.

Askofu wa Jimbo la Malakal amesisitiza kwamba ziara ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko inapaswa kuwa wakati wa kuimarisha imani ya watu wa Sudan Kusini na kuhimiza umoja nchini humo. Mkuu wa jimbo la  Malakal tangu 2019 alisema: “Tumekuwa tukingojea ujio wa Baba Mtakatifu na tunaomba kwamba wakati huu uwe wa mabadiliko kwa sisi sote Sudan Kusini, kwamba utakuwa wakati wa kuimarisha imani yetu na kufanya kazi pamoja.” Kwa kusisitiza alisema: “Sote tutambue kwamba sisi ni watoto na wana wa Mungu ili tufanye kazi bega kwa bega na kumsifu Mungu na kumtumikia kwa kujitolea, kujitolea na uaminifu wote kwa nchi hii pendwa.”

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Juba, Michael Lado Allah-Jabu aliyekuwepo wakati wa hafla hiyo, alibainisha kuwa Sudan Kusini ina bahati ya kutembelewa na viongozi Watakatifu wa Kanisa hilo, kitendo ambacho ni cha kihistoria duniani. “Nafikiri ziara hii itakuwa ya kwanza katika historia ya dunia kwamba viongozi watakatifu wanaweza kutembelea Sudan Kusini na hasa jiji la Juba,” Meya alisema hayo kwa kuzungymzie suala la Papa Francisko na ya Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby na Mchungaji mkuu  wa Kanisa la Presbyterian la Scotland. Aliahidi kwamba kama Serikali, wataunga mkono kikamilifu kupatikana kwa mafanikio kuelekea ziara ya Papa Julai na kuona uboreshaji wa matatizo huko Juba. “Tunapaswa kufanya kitu kizuri kwa Baba Mtakatifu atakapokuja Sudan Kusini,” Meya alisema na kupendekeza kwamba ikiwa kila kitu kitaenda vizuri barabara inaweza kuitwa kwa jina la Papa Francis. Alitoa wito kwa Makanisa yote bila kujali madhehebu kujiandaa kwa ziara hiyo ya kihistoria.

20 April 2022, 16:56