Zambia:Askofu Mkuu Chama asisitizia sala,toba na kufunga kipindi cha Kwaresima
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kipindi cha Kwareseia ni wakati maalum ambapo ni kufungaua mikono zaidi kwa wenye shida, walio athirika, wagonjwa, wafungwa na watu wote wenye kuhitaji. Amesema hayo Askofu Mkuu Ignatius Chama wa jimbo kuu katoliki la Kasama nchini Zambia, ambaye pia ni rais wa Baraza la Maaskofu wa Zambia (ZCCB), huku akikumbusha wakristo wajitahidi kusali, kufanya zoezi la kusamehe na kufunga wakati huu wa kipindi cha Karesima kama jinis ambavyo Mama Kanisa ameanza kuadhimisha kuanzia Jumatano ya Majivu tarehe 2 Machi 2022.
Injili ya siku ya Jumatano ya majivu inaonesha wazi kile ambacho kila mkristo anapaswa afanye katika kuendelea na mchakato wake wa safari ya Kwaresima, na ambapo Askofu Mkuu Chama amefafanua hata hivyo kuwa Mfuko ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Zambia wa Kwaresima ni kwa ajili ya kusaidia watu walio katika shida wakati wa majanga ya asili kama vile mafuriko au dhoruba kali iliyotokea hivi karibuni na kusababisha madhara makubwa katika Nchi yao na nchi za jirani. Askofu Mkuu Chama amewaeleza waamini kwa maana hiyo kuwa wawe tayari kutoa mchango wao kwenye mfuko huo kila Dominika wakati wa kipindi cha Kwaresima.
Katika siku ya kuanza Kwaresima, Baba Mtakatifu Francisko amerudi kutazama kwa karibu jamii, wakati akitoa salamu zake kwa lugha ya kireno na ktuoa ujumbe kwa Kanisa la Brazil ambalo limezindua Kampeni ya Udugu kwa Mwaka 2022 kwa kipindi chote cha Kwaresima, inayoongozwa na kaulimbiu: “Udugu na Elimu”. Papa amesema “Ukiangalia jamii ya leo, mtu huona kwa uwazi sana udharura wa kuchukua hatua za kuleta mabadiliko katika nyanja ya elimu ili kupata elimu inayokuza udugu wa ulimwengu wote na ubinadamu kamili”.