Warsaw:Bartolomeo I na Gadecki wasali pamoja kwa ajili ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican
Kila mahali kuna milioni mbiliza Waukraine ambao vita vilivyoanzishwa na Urussi vimewafanya kukosa ardhi mara moja na ambao ukarimu mkubwa wa Poland umewapa makazi na kurejesha kwa namna fulani hadhi yao. Takriban 90 pia wako kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha Kardinali Stefan Wyszyński. Ni mahali hapo ambapo Patriaki Constantinople Bartholomew I alikutana na wakimbizi na akatokwa na machozi. “Hakuna uwezekano wa kufikiria ni uharibifu gani mkubwa umesababisha uvamizi huu wa kutisha kwa watu wa Ukraine na katika dunia nzima,” anasema hayo, baada ya kukutana ana kwa ana na rais wa maaskofu wa nchi hiyo, Askofu Mkuu Stanisław Gądecki.
Alipojikuta mbele ya wakimbizi, Patriaki wa Kiekumene ambaye alianza ziara yake tangu tarehe 27 Machi kwa mwaliko wa Rais Andrzej Duda, ambaye amezungumza naye ameishukuru nchi hiyo kwa ukarimu mpana sana unaotolewa kwa Waukraine. Wakati mwingine, alisema, maneno hushindwa kuelezea hofu, na kinachobakini mshikamano wao ambao ni zawadi ya kweli kutoka mbinguni. Ni kitu pekee ambacho kinaweza kushinda uovu na giza duniani, amesema Bartholomew I. Na akipongezwa na Askofu Mkuu Gądecki alisema hata miaka 80 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kutimia Ulaya inakabiliwa tena na tamaa ya kutawaliwa na ukosefu wa heshima kwa maisha na hadhi ya mwanadamu huku akikumbuka maneno ya barua yake iliyopita aliyomwelekeza Patriaki wa Moscow Kyrill kwamba: “Vita daima ni kushindwa kwa ubinadamu. Vita hivi (...) kutokana na ukaribu wa watu wote wawili”.
Wengi wa watu wa Ukraine, nchini Poland ni Waorthodox na Askofu Mkuu Gądecki aliwahakikishia kwamba Kanisa mahalia litawasaidia katika mahitaji yao madhubuti na katika yale ya kiroho, kuheshimu upekee wao. Katika mkutano huo, taarifa iliripoti, pamoja na mambo mengine, kwamba maombi yalikuwa ni kuomba Bwana kukomesha haraka kwa vita, kwa ajili ya uponyaji wa majeraha yaliyosababishwa na ukatili, kwa ajili ya waathirika na uongofuwa mioyo ya wale walioanzisha mzozo. Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza na Kiukreni na ishara ya amani ilihitimisha mkutano huo, pamoja na baraka za Askofu Mkuu Gądecki na Bartholomew I ambaye amehitimisha ziara yake nchini Poland baada ya mikutano aliyokuwa nayo, miongoni mwa mengine, na wakimbizi wa vita katika Kituo cha Utamaduni cha Kiorthodox huko Warsaw na waamini katika Kanisa la Kiorthodox la Jan Klimak huko Warsaw-Wola, akisindikizwa na Mkuu wa Kiorthodox wa Kipoland.