Tafuta

Watoto wakimbizi kutoka Ukraine wanakaribishwa huko Lodz. Watoto wakimbizi kutoka Ukraine wanakaribishwa huko Lodz. 

Ukraine,wasalesiani:Sikiliza sauti za watoto wanaokufa bila hatia

Kusikiliza sauti za watoto wanaokufa kwa sababu ya mabomu;ulimwengu lazima utambue majanga haya.Kama Wasalesiani wa kike na kiume wanabainisha kwamba hawawezi kukaa kimya katika nyakati hizi za kusikitisha ambazo wanaona mvamizi akishambulia na kukiuka maisha ya watu wasio na hatia.Lazima wapige kelele,wazungumze na ulimwengu mzima uliostaarabika kuhusu matendo haya mabovu ya kutisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shirika la Wasalesiani wa huko Ukraine wamepaza sauti zao ili kutetea maisha ya watoto wadogo kutokana na vitisho vya vita. Katika wito uliotolewa na shirika la Habari la Walesian (Ans) wanashutumu kwamba tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, karibu watoto 80 wameuawa na wengi wamejeruhiwa. Maelfu ya watoto wanalazimika kukimbia milipuko ya mabomu na kujificha katika vyumba vya chini vya ardhi vilivyotelekezwa na vilivyochakaa, wakibaki huko kwa siku na siku kwenye baridi, bila mwanga na bila chakula na maji. Maelfu ya watu wakiwemo watoto na vijana wamepatwa na kiwewe cha kisaikolojia kutokana na hofu ya kifo na mapambano ya maisha.

Wakimbizi wanapata mahali pa kulala kila eneo wanapofikia
Wakimbizi wanapata mahali pa kulala kila eneo wanapofikia

Kama Wasalesiani wa kike na kiume wanabainisha kwamba hawawezi kukaa kimya katika nyakati hizi za kusikitisha ambazo wanaona mvamizi akishambulia na kukiuka maisha ya watu wasio na hatia. Lazima wapige kelele, wazungumze na ulimwengu mzima uliostaarabika wa matendo haya ya kishenzi na ya kutisha. “Sikia sauti za watoto wanaokufa kutokana na mabomu! Nani atawalinda isipokuwa sisi tuliotumwa kwao? Hatupaswi kuogopa kusema ukweli. Viongozi wa dunia na ulimwengu lazima wajue kuhusu mambo haya ya kutisha”.

Wakimbizi wanapata mahali pa kulala kila eneo wanapofikia
Wakimbizi wanapata mahali pa kulala kila eneo wanapofikia

Kwa maana hiyo wanatoa ombi kwamba “Tuungane pamoja kuwalinda watoto, si katika maombi tu, bali hata katika matendo madhubuti. Asante kwa kila mtu kwa msaada na msaada. Pamoja tuna nguvu! Tunaomba sala za nguvu zaidi kwa ajili ya watoto na kwa maelfu ambao wamepoteza kila kitu. Mungu, kaa karibu nasi katika nyakati hizi za huzuni. Tunajisikia salama tukiwa na Wewe!”

16 March 2022, 15:30