Ukraine:Ukraine haiwezi kuogopeshwa namna hii.Ukraine inapambana
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ujumbe kwa njia ya Video wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kigiriki la Ukraine, Sviatoslav Shevchuk uliotolewa Ijumaa ameanza kusema:“Tumsifu Yesu Kristo kaka na dada katika Kristo leo tarehe 18 Machi 2022 na Ukraine inaishi kwa siku 23 sasa katika vita vya umwagaji damu. Leo usiku makombora na mabomu yameanguka katika vichwa vya raia huko Summy katika Mkoa wa Donetsk, Luhansk, Mykolaiv, hata katika sehemu ya mashariki ya Ukraine, ikiwemo Lviv”. Kiongozi huyo amesema “ Lakini Ukraine haiwezi kuogopeshwa namna hii. Ukraine inapambana. Ukraine iko inapambania uhuru na kwa ajili ya kupata uhuru wake. Ukraine ipo”. Akiendelea kiongozi huyo amesisitiza kuwa wao wanaendelea kulipa gharama wakiwa wa kwanza, kwa nguvu zao za kijeshi, nguvu za maaskari ambao wameweza kusimamisha adui wengi ambao hawawezi kuingia ndani kabisa mwa nchi yao. Adui ambaye wakati uliopita waliitwa vita vya kiimla. Kwa maana hiyo kiongozi huyo ameomba kusali sala maalum ya kusindikiza wahudumu wao katika sekta ya kiafya, madaktari, wauguzi, watu wa kujitolea na wale ambao wakiwa mstari wa mbele kugusa uchungu uziolezeka wa kibinadamu nchini Ukraine.
Kwa mujibu wake amebainisha kwamba ni wahudumu wa kiafya ambao leo hii wanalengwa sana katika mashambulizi ya adui kwa raia. Kwa kutoa mfano amesema “Kulingana na takwimu rasmi za Wizara ya Afya , katika wiki hii nchini wameshambulia hospitali 117 na taasisi za kiafya. Miongoni mwake, saba zimeharibiwa kabisa haiwezekani kuzikarabati. Ambulensi 43 ziimeharibiwa kabisa. Wamekufa madkatari kadhaa na wahudumu wa kiafya. Kiongozi huyo amependa kumshukuru Mungu kwa ajili yao kwa kazi ya kishujaa kwa watu wao. Lakini amesisitiza kwamba licha ya hayo madaktari na wahudumu hao wanaendelea kuokoa maisha ya kibinadamu huko Ukraine. Katika sala ameomba pia kumshukuru Bwana hasa kwa ajili yao madaktari wanaosaidia wanawake kujifunga katika hali ya baridi sana na bila hata taa huko Chernihiv, Mariupol, Kharkiv na sehemu nyingine zilizovamiwa na maadui. Kiongozi huyo amependa pia kumshukuru Bwana kwa wale ambao usiku na mchana wanajaribu kuokoa maisha ya binadamu. Ulimwengu mzima umemtambua katika Hospitali ya Kiev kuhusu yule Mama na Mtoto aliyepata pigo la shambulio la ndege na kufa, lakini hospitali hiyo inaendelea kufanya kazi kishujaa. Amependa kumshukuru Bwana kwa ajili ya wadaktari wao kwa sababu wao wanatoa ushuhuda wa mateso ya kibinadamu na kuokoa.
Kiongozi huyo vile vile akiendelea na ujumbe wake kwa njia ya video amependa kuonesha shauku kwa Shirika la Kimataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) , taasisi mbali mbali, mashirika ya kimataifa kama vile Madaktari wasio na Mpaka akiomba kuomba wainue neno moja kuhusiana na utetezi na ulinzi wa maisha ya binadamu huko Ukraine. Ameshuru kwa msaada ambao leo hii umetolewa kwa madaktari wao, lakini anaomba watoe wito kwa pamoja kusimamisha mauaji wa watu huko Ukraine. Hatimaye: “Tunakushukuru kwa ukweli kwamba, pamoja na misaada ya kibinadamu nchini Ukraine, nchi inapokea misaada kwa njia ya madawa, vifaa vya matibabu na kila kitu ambacho kinaweza kuokoa maisha leo. Leo tunamwomba Bwana wetu, daktari wa roho na miili yetu: wabariki madaktari wetu na wafanyakazi wa matibabu, kuokoa waliojeruhiwa, watoto, wanajeshi, wazee, ponya majeraha ya watu wako. Mungu okoa Ukraine. Ninawapa baraka za Bwana juu yenu kwa neema na upendo Wake kwa wanadamu sasa na siku zote na milele na milele. Amina. Tumsifu Yesu Kristo”