Tafuta

Waamini wakatoliki wa Moldavia Waamini wakatoliki wa Moldavia 

Ukraine/Moldavia:wakimbizi wanazidi kumiminika!

Askofu Anton Khosa,wa Chisinau,Moldavia anaamini kwamba kwa sasa wanaweza kutoa hifadhi na msaada kwa wakimbizi 500,ingawa inaonekana kwamba sehemu ngumu zaidi inakuja kwani inasemekana kuwa kasi hii ya awali itapungua,jumuiya itachoka na ni katika nyakati hizi ambazo kutakuwa na hitaji hata zaidi la watu wenye imani katika Mungu ambao wako tayari kuondoka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hadi sasa zaidi ya takriban ya wakimbizi 112,000 wamefika Moldovia, na idadi yao inaendelea kuongezea saa na siku. Amesema hayo katika mahojiano na vyombo vya habari vya Radio Vatican Askofu Anton Kosha, wa Jimbo la  Chisinau, wa mji wa Moldavia, kuhusiana na kukaribishwa wakimbizi kutoka Ukraine kwamba  Kanisa lao  na jamii yao yote imeanza maandalizi  tangu siku za awali kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kusaidia wakimbizi wengi. Katika suala hili, inakadiriwa kuwa, hadi sasa, takriban wakimbizi 112,000 wamefika Moldavia, na idadi yao inaendelea kuongezea saa na siku.

Vituo mbali mbali vinasaidia wakimbizi

Hata kabla ya vita kuanza, maeneo yalikuwa yametayarishwa kwa ajili ya wakimbizi, kupitia vituo vyetu na kupitia matoleo kutoka kwa marafiki na watu waliokuwa tayari kusaidia. Kwa hivyo, tangu siku za kwanza, walianza kuwapa huduma mbalimbali kwa msaada wa kujitolea, lakini zaidi ya yote shukrani kwa mashirika yao ya misaada ‘Caritas Moldova’, ‘Regina Pacis’, ‘Optima Fide’, ‘Casa della Provvidenza’, ‘Yohane Paulo II’, ‘Kituo cha Don Bosco’ nakwa saa kuna Upyaisho wa Harakati ya Roho Mtakatifu.

Mgawanyiko wa kazi kwa ajili ya wakimbizi

Wengine wanajishughulisha kuleta watu kutoka mipakani hadi mahali hapo kwenye vituo, wengine wanakusanya mahitaji msingi, au hata kujaribu kujibu maombi maalum kuhusiana na hati au hali dhaifu za kiafya; bado wengine husaidia katika kupanga vifaa kwa wale wanaotaka kusafiri, kutoa habari juu ya uwezekano wa kusafiri, kusaidia kununua tiketi, kuchukua vipimo vya  covid, na mengine. Zaidi ya hayo, kuna waamini katika parokia zao walio tayari kuwakaribisha wakimbizi katika familia zao, na pia kuna wale ambao wanapokuwa nje ya nchi, hufanya makazi yao yaweze kuwa vizuri. Baadaye inapowezekana, tayari wakimbizi wanakaribishwa katika nyumba za parokia na nyumba za mashirika.

Siku ngumu zinakuja za uhitaji zaidi

Askofu huyo anaamini kwamba kwa sasa wanaweza kutoa hifadhi na msaada kwa wakimbizi 500, ingawa inaonekana kwamba sehemu ngumu zaidi inakuja hivi sasa: inasemekana kwamba kasi hii ya awali itapungua polepole, jumuiya itachoka, na ni katika nyakati hizi ambapo kutakuwa na hitaji hata zaidi la watu wenye imani katika Mungu ambao wako tayari kwenda njia yote. Kwa sababu hiyo, pamoja na matendo yao  yote, Jimbo  nzima linamwomba Bwana kila mara kwa nguvu na kuomba zawadi ya amani: Yeye pekee ndiye anayeweza kusaidia kupinga na kutafuta njia ya amani , alisisitiza askofu.

04 March 2022, 15:25