Ukraine:Kanisa la Moldavia linakaribisha wakimbizi kutoka Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baada ya siku kumi na moja tangu mwanzo wa mzozo na juhudi nyingi katika kuwakaribisha wakimbizi kutoka nchi jirani ya Ukraine, iliamuliwa kutuma wawakilishi wa moja kwa moja kutoa taarifa kwa vyombo vya habariili kufahamisha kile ambacho Kanisa Katoliki linafanya huko Moldovia ana mipakani mwake. Na kabla ya kuwasilisha takwimu juu ya uwezo wa mapokezi, wanahisi kubainisha mambo mawili muhimu. Ndivyo wamtoa habari wawakilishi wa Radio Vatican Jean Charles Putzolu walioondoka kwenda Moladavia kuona kile kinachoendelea kwa wakimbizi kutoka Ukraine. Kwa njia hiyo wakiendelea kuelezea wanasema msingi wa kwanza ni kuhusu ukweli kwamba Kanisa Katoliki nchini Moldovia na inawezekana kufikiri kwamba hii pia ni kesi kwa waamini wote, inaelezea matumaini kwamba hali ya amani na utatuzi wa mgogoro unaweza kufikiwa haraka iwezekanavyo. Papa Francisko amekuwa akiomba hili kwa muda, sasa na huku akielezea wasiwasi wake na mateso yake.
Vivyo hivyo, Askofu Anton Cosa hakukosa kuhimiza jumuiya za Kikatoliki huko Moldavia ili zisali kwa sababu hiyo hiyo. Jambo la pili msingi ni lile la kutaka kutoa shukurani za dhati kwa wananchi wa Moldovia kwa ukarimu na upatikanaji wanaouonesha katika kuwakaribisha na kuwa karibu na maelfu ya wakimbizi wanaokuja nchini mwao. Dhamira ya mamlaka husika katika kushughulikia tatizo gumu la ukarimu inapaswa pia kutiliwa mkazo, pia kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na mashirika ya hiari yakiwemo yale ya Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki, kwa mwaliko wa Askofu Anton Cosa, tangu mwanzo kabisa, limejitolea kukaribisha mashirika yafuatayo: Caritas Moldovia, Regina Pacis Foundation, Fides, Casa della provididenza, Optima fide, Don Bosco Foundation, Upyaisho wa Roho, Njia ya Neokatekumenal, parokia na jumuiya za kidini. Miundo ya mapokezi imeandaliwa, pamoja na baadhi ya parokia na vyumba vya kijamii, ambavyo kwa sasa vinahakikisha uwezo wa vitanda 390, pamoja na huduma za afya na chakula.
Kwa kuongezea, mtandao wa mshikamano wa familia uliundwa, ambapo familia za binafsi zilijitolea kupokea. Huduma za kusindikiza pia zinatolewa wakati wa kuwasili Moldovia kwenye mipaka na wakati wa kuondoka kuelekea maeneo ambayo wao wanataka wakimbizi kwenda, vile vile wanatoa usaidizi wa kisaikolojia na afya mtandao wa habari unafanya kazi na wanafamilia ambao bado wako Ukraine na wale ambao wakimbizi wanakusudia kwenda. Kazi ya taarifa sahihi inafanywa, ili wakimbizi waepuke aina za unyonyaji, usafirishaji haramu wa binadamu na kuomba watoto au wanawake wasio na waume zao. Kuna upatikanaji wa kantini za kijamii za Kikatoliki, ambazo zimekuwa zikifanya kazi kila wakati, ili kusambaza milo katika vituo vyao wenyewe na nje, katika vituo vingine vya mapokezi au pale inapoombwa. Hakuna ufahamu wa wazi wa nyakati za mapokezi na muda wa mzozo utakavyokuwa, lakini ni wazi kuwa Kanisa Katoliki pamoja na mashirika yake yatakuwepo ilimradi mapokezi ya dharura ni wajibu na hata zaidi ya familia zinazoomba. Kanisa Katoliki, pamoja na kushirikiana na miundo ya Jimbo la Moldovia, linawasiliana mara kwa mara na mashirika mengi ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, Mabalozi na taasisi mbalimbali zinazounda mtandao wa mshikamano wa kimataifa, ambao ni muhimu sana kwa kupokea msaada katika shughuli za kukaribisha.
Uwepo muhimu ni ule wa waamini wa Kikatoliki huko Moldovia, ambao kwa kila njia na kwa rasilimali zao wanafanya kazi hasa pamoja na parokia. Rasilimali nyingine ni wale wanaofanya mawasiliano kutoka nje ya nchi, ambao kwa njia tofauti hujitolea kila siku kutoa ushirikiano na msaada wa kila aina. Hakuna ukosefu wa uungwaji mkono kutoka kwa mashirika ya Kikatoliki ya baadhi ya nchi za Ulaya, ambayo kwa njia tofauti yangependa kuunga mkono kazi yao ya ukaribishaji, kwa matumaini kwamba mikondo ya kibinadamu inafaa kwa ajili ya kuhakikisha mapito yote na kuwasili kwa marudio ya kile kinachohitajika. Shughuli ya kukaribisha zinafanywa kwa umakini wa kina kwa watu, kwa roho ya kiinjili, utayari wa kusikiliza na mazungumzo. Heshima na utunzaji wa mahitaji ni lengo la kwanza, pamoja na kuambatana na kurejesha utulivu. Uangalifu hasa kwa watoto wadogo, ambao ni sehemu tete zaidi ya mapokezi, ambao hupewa fursa ya kupata wakati wa uhuishaji na burudani. Wana hakika kwamba kazi hii ya kibinadamu inaweza kuwakilisha wakati wa tafakari ya kibinadamu na ya Kikristo juu ya maisha na zaidi ya yote inasaidia kurejesha maadili ya maisha ya binadamu, ambayo lazima yaheshimiwe na si kutumwa kwa migogoro inayozalisha kifo na uharibifu. Mungu mwema aongoze hatua zao na awaongoze kwenye amani.