Sudan Kusin:Ziara ya Papa Francisko ni thamani ya kiekumene ya nchini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baada ya kupata taarifa kuhusu ziara ya Papa Francisko chini Sudan Kusini, wameteua Kamati ya wawakilishi wanne kutoka Baraza la Maaskofu nchini Sudan Kusini na Sudan (SSCBC) ili kuanza maandalizi. Kamati hiyo itaunganishwa na ile ya maandalizi ya Serikali kwa ajili ya kufanya kazi pamoja. Ndivyo amethibitisha hayo Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mulla, wa Jimbo Kuu la Juba, kuhusiana na maandalizi ya Baraza la Maaskofu kuhusu Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Sudan Kusini, inayotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia tarehe 5 hadi 7 Julai 2022 mara baada ya kutoka siku hiyo hiyo nchini DRC hasa maeneo ya Kinshasa na Goma(2-5 Julai 2022).
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ameyu ambaye pia ni msimamizi wa Jimbp la Torit nchini Sudan Kusini, amesema kama Taifa na kama Kanisa, wanahisi kupata heshima kubwa kwa tangazo hilo la ziara ya Baba Mtakatifu. Itakuwa ni kipindi kikubwa cha faraja kwa watu wote wa Sudan Kusini kwa ajili ya kuhamasisha amani na maridhiano. Ni matumaini yake kuwa ziara ya Papa iweze kuwatia moyo watu wote kuchuchumalia mazungumzo, amani na haki ili kuwezesha msimamo thabiti wa amani katika nchi. Ziara ya Papa Francisko ni ya kiekumene. Kwa sabababu itawaona Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby wa Ungereza Mkuu wa Kanisa la kianglikani na Mratibu wa Kanisa la Kipresibiterian wa Scotland. Ziara ya Baba Mtakatifu ya kutembelea nchini Sudan Kusini, imedumu tangu kupata fursa ya mkutano uliofanyika jijini Roma mnamo Aprile 2019, Askofu Mkuu Canterbury Justin Welby na viongozi wa kisiasa Sudan Kusini, katika mchakato huo, Papa aliwamboa watafute amani.
Naye Askofu Charles Sampa Kasonde wa jimbo la Solwezi, Zambia, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika mashariki katika maoni yake amesema wanayo furaha kubwa na siku hazikimbii ili Baba Mtakatifu Francisko aweze kufika nchi hizo. Ziara hii kwa namna moja inatimiza ahadi yake zaidi ya ukakika wa upendo wake kwa Sudan Kusini na jitihada zake kwa uhakikisho kuwa amani inaweza kutawala katika uso wa ardhi.