Senegal:simamisha mapigano Casamance na kuanza mazungumzo ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika harakati za miaka mingi za kazi ya kuingilia kati upatanisho kwa ajili ya amani kati ya Serikali ya Senegal na Harakati za Nguvu za Kidemokrasia za Casamence, (MFDC), Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaelezea wasiwasi wake wa kina kwa sababu ya kuendelea kwa upinzani wa kisilaha wa sasa huko Kaskazini mwa Casamance. Baada ya mapigano yaliyotokea mnamo tarehe 24 Januari 2022 kati ya wanajeshi wa Senegal ambao wanashiriki utume wa kanda ya Afrika Mashariki ECOWAS na Kikundi cha waasi cha MFDC kikiongozwa na Salif Sadio, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imeingilia kati ili kuvunja ajali nyingine na kuzuia matokea mabaya kwa kuwezesha kurudishwa miili ya wanajeshi wa Senegal waliouawa na kukomboa Wanajeshi wengine saba waliokuwa mateka wa MFDC huko Casamance.
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaomba kwa sasa operesheni ya wanajeshi wa Senegal kuwapo uwezekano wa kulinda msimamo thabiti wa maeneo husika na kutunza uwazi wa mchakato wa mazungumzo. Jumuiya pia inabainisha uwezekano wake wa kuendelea kuwa kati katika kusindikiza mchakato huo wa mazungumzo kwa kuamini kuwa ni kwa njia ya kutathimini kwa pamoja inawezekana kabisa kufikia amani ya kudumu katika eneo la Casamance.
Hata hivyo wanajeshi wote saba waliokuwa wamefungwa walionekana wenye afya nzuri, salama salimini. Waliwasili bila kuwa na silaha zao, wakiwa wamezungukwa na waasi. Makabidhiano ya wafungwa hao yalifanyika katika maeneo ya mashambani, karibu na mpaka na Senegal. Kiongozi wa waasi Salif Sadio hakuhudhuri tukio hilo. Baadhi ya watu walifunga safari, kupitia njia hatarishi katikati ya msitu. Kando ya mwakilishi wa ECOWAS walikuwepo wajumbe wawili wa ICRC, pamoja na kiongozi wa jumuiya ya Mtakatifu Egidio, jumuiya ambayo kwa dhati ilifanya kazi kama mpatanishi ili kuweza kuachiliwa huru kwa mateka hao.
Wakiwa hapo katika makabidhiani walitoa hotuba zilizotanguliwa na kauli za kupongeza: bila kutoa neno lolote, kila askari alitia saini kwenye karatasi inayothibitisha kuachiliwa kwake. Hati iliyotiwa saini tena na Mnigeria Claude Kondor, aliyewakilisha ECOWAS. Alishukuru kwa moyo mkunjufu MFDC kwa hatua hioyo na kusema kwamba “ umeona vita katika baadhi ya nchi, lakini ishara kama hizo hazijawahi kuonekana. Kwa niaba ya ECOWAS, ninataka kukushukuru kwa ishara hii ambayo ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu”. Wanajeshi hao saba walikuwa wameshikiliwa mateka tangu makabiliano ya mwezi Januari 24 2022 kati ya kikosi cha ECOWAS na waasi wa MFDC.