Tafuta

Mshikamano wa Watu kukusanya mahitaji muhimu kwa ajili ya Ukraine katika Kanisa la Mtakatifu Sofia Roma. Mshikamano wa Watu kukusanya mahitaji muhimu kwa ajili ya Ukraine katika Kanisa la Mtakatifu Sofia Roma. 

Roma:wito wa kukusanya msaada kwa ajili ya watu wa Ukraine

Kanisa Katoliki la Mtakatifu Sofia njia ya Boccea 478,Roma liko linakusanya vifaa muhimu vya kuweza kutuma nchini Ukraine kwa ajili ya kuwasaidia watu.Ukusanyajii na msaada huo unaratibiwa na Msimamizi wa Kanisa hili Padre Marco Semehen.Na wakati huo huo maelfu ya wakimbizi wanakimbia ambapo inakadiliwa zaidi ya watu 500,000 kwa mujibu wa(UNHCR).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mgogoro wa Ukraine na Urusi unaeondelea  tayari unaathiri sehemu kubwa ya  ulinzi na usalama wa raia, hasa wanawake na wasichana, ambao wako katika hatari kubwa ya unyanyasaji na zaidi kukosa msaada. Kila sehemu, wameanza kuafuta namna ya kutoa msaada wa kupeleka mahitaji. Kutokana na hiyo Kanisa Katoliki la Mtakatifu Sofia njia ya Boccea 478, Roma nchini Italia liko linakusanya vifaa muhimu vya kuweza kutuma nchini Ukraine kwa ajili ya kuwasaidia watu. Ukusanyajii na msaada huo unaratibiwa na Msimamizi wa Kanisa hilo Padre Marco Semehen.

Watu wa kujitolea wa Ukraine wa jumuiya ya Waukraine Roma wakifunga vifaa muhimu
Watu wa kujitolea wa Ukraine wa jumuiya ya Waukraine Roma wakifunga vifaa muhimu

Miongoni mwa vitu muhimu vilivyo vya kwanza vyakula kama vile pasta, mafuta ya alizeti ya makopo, mchele, kahawa, chai, Nutella, vitafunio, tuna ya makopo, kunde na chakula cha makopo, maziwa ya unga kwa watoto. Vitu hivyo vya chakula visiwe kabisa katika vyombo vya vioo kwa ajili ya usalama wa usafirishaji. Na zaidi vinahitajika vitu vya usafi wa kibinafsi kama vile (sabuni, taulo za usafi, pampas kwa ajili ya watoto, pedi za wanawake, gozi za kufunga na kusafisha vidonda, tishu za kusafisha mikono; dawa kama aspirini, ibuprofen, ferments lactic, sindano, plasters, disinfectants; insulini ya muda mrefu, metformin na vitamini na kadhalika; pamoja na  viberiti na betri.

Watu wa kujitolea wa Ukraine wa jumuiya ya Waukraine Roma wakifunga vifaa muhimu
Watu wa kujitolea wa Ukraine wa jumuiya ya Waukraine Roma wakifunga vifaa muhimu

Na kwa yule anayetaka kutuma fedha: Iban: IT10B0503403239000000003649 (sababu ya kutuma ni msaada Ukraine) CHIESA SANTA SOFIA, yaani Mtakatifu Sofia.

Katika masaa ambayo vikosi vya kijeshi vya Ukraine vinapozidi kuendelea kupambana na mtiririko wa wakimbizi unaendelea kuondoka zaidi na zaidi. Kwa kutumia Mabus, kwa njia ya Treni na  kwa magari binafsi inapowezekana vilevile wanasafiri kilomita nyingi kutafuta kimbilio. Wakati huo huo kwa umbali na wengine wakitembea kwa miguupia  wakikabili na baridi, wakiwa wamebeba watoto wadogo mikononi mwao na mizigo iliyofungwa kwa haraka. Njia kubwa ya kutoroka ni mto uliofurika watu zaidi ya 500,000 tayari wamevuka mpakani, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Walio wengi wanakimbilia zaidi ya yote nchini Poland na baadaye Hungaria, Moldavia, Romania na Slovakia. Nchini Serbia pia iko tayari kuwakaribisha kwa kufanya maeneo yenye kuwezesha watu elfu 6. Ni katika nchi ya Romania, katika mji wa Sighet, mita 800 kutoka mpaka na Ukraine, kwa mujibu wa mshirika wa chama cha “Suntem Vocea Lor” yaani “Sisi ni Sauti yao na Kazi ambalo i shirika la kibinadamu Bi Florentina akizungumza na Vatican amethibitisha uhitaji sana wa mafuriko ya watu wanaovuka mpakani kuhitaji kila kitu.

Hawa ni wakimbizi wakisubiri Busa kwenda Moldavia
Hawa ni wakimbizi wakisubiri Busa kwenda Moldavia

Hawa ni watu, familia zinazoonesha hadhi na heshima kubwa, amesema Bi Negres.  M Mwanzoni hawataki kitu chochote wanapofika, na  polepole wanaelewa kwamba wanaweza kupata  msaada, kwa mahitaji msingi, lakini pia kwa ajili ya malazi, kuzunguka, kufikia maeneo mengine. Kuna hofu machoni mwao, kiasi kwamba katika vyumba walivyopangiwa wanajifungia ndani. Baadaye kutoka katika kutoaminiana kwa asili kunakuwa shukrani na mvutano wao unayeyuka na kuwa mpango wa ukombozi. Takriban watu 100,000 wanakimbia Ukraine kwa siku: na hivyo inawezekana ukawa mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu barani Ulaya katika miongo ya hivi karibuni, kama alivyo sema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Alhamisi tarehe 24 Februari mjini Brussels, kwa mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja ambao watatoa ulinzi wa muda kwa wakimbizi kwa kuwapatia visa ya mwaka mmoja, ambayo itawafanya Waukraine kukimbia vita ili waweze kukaa kisheria katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Msaada wa kibinadamu wa Msalaba Mwekundu Ujerumani kuandaliwa kwa ajili ya wakimbizi huko Poland
Msaada wa kibinadamu wa Msalaba Mwekundu Ujerumani kuandaliwa kwa ajili ya wakimbizi huko Poland

Maagizo hayo yanatanguliza mfumo wa ugawaji kwa hiari: wakimbizi watachagua nchi gani wanataka kwenda. Wataweza kufanya kazi, kupata huduma za afya, kuhudhuria shule na kozi za mafunzo. Italia imeongeza uwezo wa Mfuko wa Dharura kwa milioni 10 na imepanga nafasi 13,000 katika Vituo maalum vya Mapokezi na vingine 3,000 katika Mfumo wa Mapokezi na ufungamanishwaji.

01 Machi 2022, 15:35