Mshikamano wa Wapoland kwa watu wanatoka Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kutoka Krakow nchini Poland utafikiri vita viko mbali. Hofu imeshinda kwa njia ya mshikamano mkubwa wa Wapoland ambao wanasubiri watu katika kituo kikuu cha Treni wanaotokea Leopoli na wengine Kiev. Amethibitishwa hayo mwandishi wa habari wa Vativcan News, Luka Collod aliyetumwa huko kutoa habari kwa kile kinachoendelea moja kwa moja. Treni zinafanya kazi, na kuwakilisha tumaini kwa wanawake wengi na watoto wao ambao wanakuta ndugu zao, marafiki hata watu wa kawaida ambao wamejitolea kutoa ukarimu na nyumba kwa wale wanaokimbia vita. Majimbo yameanza kujikita katika ukarimu watoto yatima kwa sababu wamefika maelfu na maelfu kutoka Ukraine na kuna wasiwasi wa Makanisa mahalia na mashirika ya watu wa kujitolea ambao wanakuwepo kwenye vituo ili kuwapokea na kukaa nao karibu kwa sababu ya kuzuia biashara ya binadamu, picha mbaya na biashara ya viungo.
Kutokana na sababu hizo viongozi wa Kanisa wanaomba mamlaka kuweka sheria thabiti ya kuwakabidhi watoto hao katiia mikono sahihi. Katika mipaka, vituo vya kiafya vinafanya kazi kwa juhudi kubwa ya kuwapokea watoto wagonjwa wa saratani. Lakini mshikamano huo pia hausahau wazee wengi wanaofika. Wengi wao wamefika huko Kracaw nchini Poland. Wengi wao wanabaki peke yao nchini Ukraine kwa sababu hawana uwezo wa kukimbia, wengine ni wagonjwa sana na wengine hawana nguvu na wala uwezo wa kuondoka kwani katika kuondoka lazima uwe na fedha kidogo za kusafiria. Vile vile kufika mjini kwenye vituo vya treni lazima uwe na usafiri wa kukufikisha. Kwa wazee walio vijijini hawana uwezo huo.
Hata hivyo katika maoni ya Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuk, kiongozi mkuu na Padre wa Kanisa la Kigiriki- katoliki nchini Ukraine akizungumzia juu ya taarifa ya kuwekwa wakfu Ukraine na Urusi kwa Moyo Safi wa Bikira Maria amesema katika janga la vita vya kumwaga damu nchini Ukraine, habari hiyo katika fursa ya tarehe 25 Machi ya kuadhimisha Ibada ya Toba katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ni “Tendo la kiroho ambalo limesubiriwa sana na watu wa Ukraine. Wakatoliki wa Ukraine tangu kuvamiwa na warusi mnamo 2014 walikuwa wanaomba tendo kama dharura ili kuzuia kuongezeka zaidi kwa vita na hatari zinazotoka huko Urusi.
Askofu Mkuu aidha amesema kwamba katika mikutano yake na Baba Mtakatifu, aliweza kuonesha shauku hiyo ya waamini wa Kanisa lao kwa upendo wa kibaba. Kwa uvamizi wa Urusi, wimbi kubwa kutoka ulimwengu wanasali ili kutimiza tendo hilo. Wanamshukuru Baba Mtakatifu awali yote kwa kukubali ombi lao kwa Mama Maria ili kuelezea tokeo la mnamo tarehe 13 Julai 1917 huko Fatima na kwa watoto wake, kwa kulinda Ukraine na kuthibitisha makosa ya Urusi kuendeleza vita na mateso ya Kanisa. Kwa maana hiyo askofu amebainisha kuwa wanaona maneno ya Mama Maria aliyosema: “Watu wema watakufa kishaidi na Baba Mtakatifu atateseka sana, mataifa mbali mbali yataharibiwa”. Tukabidhi kwa moyo Safi wa Bikira Maria mateso yote na matumaini kwa ajili ya amani ya nchi yao inayoteseka, ameongeza kusema.
Na zaidi askofu amesema kuwa wanataka kuwataarifu kuwa utumaduni wa kuwekwa wakfu kwa Mama wa Mungu ndiyo Historia ya kizamani. Wakati huo watu wa Urusi na Ukraine waliwekwa wakfu kwa ulinzi wa Bikira Maria mfalme Yaroslav wa Hekima, Kardinali Myroslav Ivan Liubachivsky aliyepyaisha kuwekwa wakfu mnamo mwaka 1995 hukoZarvanytsia. Tendo la kuwekwa wakfu Ukraine chini ya Ulinzi wa Bikita Maria lilitokea mnamo Dominika tarehe 6 Aprili 2014 katika Makanisa yote ya Kigiriki - katoliki nchini Ukaine. Na mnamo 23 Oktoba 2016 Askofu Mkuu Sviatoslav huko Fatima alitimiza tendo la kuweka wakfu nchi ya Ukraine kwa Moyo safi wa Bikira Maria.