Mkutano mkuu wa 19 wa SECAM huko Accra,Ghana Julai 25-1Agosti 2022
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM watafanya mkutano wao Mkuu wa 19 kuanzia tarehe 25 Julai hadi Mosi Agosti 2022 Jijini Accra nchini Ghana. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa SECAM Padre Terwase Henry Akaabiam amesema Mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu:Umiliki wa SECAM: Usalama na Uhamiaji Barani Afrika na Visiwani, awali ya yote utajikita katika upanuzi wa wajumbe wake wenyewe, kuhusu migogoro mingi ya bara la Afrika, matokeo ya vifo na kutawanyika kwa mamilioni ya watu, maaskofu Katoliki, vile vile kufikiria usalama hasa kwa kujengwa upya Afrika yenyewe kitovu kikiwa juu ya Mungu, kama kilelezo cha Hati ya Kampala iliyocahapishwa mara baada ya Jubilei ya Dhahabu ya SECAM mnamo 2019.
Mkutano utadhuliwa na wajumbe wa Kanda nane za Mabaraza ya Maaskofu Barani Afrika
Kwa kawaida mkutano mkuu huo ufanyika kila baada ya miaka mitatu, hivyo katika fursa ya Mkutano mkuu huwa utawaudhuliwa na wawakilishi kutoka Kanda nane za mabaraza ya maaskofu barani Afrika; mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati (ACEAC), Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika ya Kati, ACERAC, Umoja wa Wakatoliki wa Misri (AHCE), wajumbe wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA), Mabaraza ya Maaskofu wa Bahari ya Hindi (CEDOI), Shirikisho la Kanda ya Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Kaskazini (CERNA), Shirikisho la Kanda ya Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini (IMBISA) na Umoja wa Baraza la Maaskofu wa Afrika Magharibi (RECOWA/CERAO).
SECAM iliundwa mbamo mwaka 1969
SECAM ilizaliwa mnamo 1969 jijini Kampala Unganda kwa utashi wa Maaskofu Katoliki waliokuwapo katika Mtaguso wa II wa Vatican ili kuweza kuzungumza kwa sauti moja juu ya masuala yanayohusu Kanisa barani Afrika. Na hii ilikuwa ni wakati wa ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu wakati ule Papa Paulo VI nchini Uganda na kwa maana hiyo kuanzishwa kwa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM ulikuwa ni tarehe 29 Julai 1969.
SECAM alitambulia na Umoja wa Nchi za Afrika 2015
Katika kuleta pamoja sauti ya Kanisa Katoliki katika masuala mema ya utawala na maendeleo endelevu, na kuhamasisha utumishi wa uongozi kwa bara zima na visiwa, vyake SECAM ilipata utambulisho wake katika ngazi ya Umoja wa Nchi za Afrika (AU) mnamo 2015. SECAM inatumia lugha tatu rasima za kuzungumza katika Kanisa kwenye bara, Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Uendeshaji wake wa kichungaji unajikita kupitia Tume zake mbili zinazoitwa: “Uinjilishaji na Haki pamoja na Amani na Maendeleo. Ikumbukwe kwamba Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM ilifanya Mkutano mkuu wa 18 kuanzia tarehe 20 Julai hadi tarehe 29 Julai 2019, kwa kuudhuriwa na wajumbe 400 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika. Mkutano huo uliongozwa kauli mbiu: “Kanisa, familia ya Mungu Barani Afrika; Sherehekea Jubilei yako! Mtangaze Kristo Yesu Mkombozi wakokatika kieleleza cha Jubilei ya Miaka 50 ya uwepo na utume wa SECAM, Barani Afrika. Kilele cha Jubilei hiyo kilianzia tarehe 23-28 Julai 2019, huko Uganda.