Mapadre wa Kiorthodox Urusi:wito wa amani haupaswi kukataliwa
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Kundi la mapadre na mashemasi 233 wa Kanisa la Kiorthodox la Urusi limezindua wito wa nguvu kwa wale wote ambao wanataka uwepo mwisho wa vita huko Ukraine, unaofafanuliwa kama “mauaji ya kindugu” wakiomba upatanisho na kusitishwa kwa mapigano mara moja. RWito huo unakuja baada ya Dominika ya Hukumu ya Mwisho na katika juma linalotangulia Juma la Msamaha. “Tunaomboleza mateso ambayo kaka na dada zetu nchini Ukraine wamepatwa nayo isivyostahili.” Kwa kukumbuka kuwa maisha ya kila mtu ni zawadi ya kipekee na ya Mungu, mapadre na mashemasi wanasisitiza jinsi ambavyo Hukumu ya ulimwengu inawasubiri wote.
“Hakuna mamlaka ya kidunia, hakuna daktari, hakuna mlinzi atatulinda kutokana na hukumu hii. Kujali wokovu wa kila mtu anayejiona kuwa mtoto wa Kanisa la Kiorthodox la Urusi, hatutaki aingie hata mmjoja katika hukumu hiyo, akibeba mzigo mzito wa laana za mama. Tukumbuke kwamba damu ya Kristo, iliyomwagwa na Mwokozi kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, itapokelewa katika sakramenti ya Ushirika na wale wanaotoa maagizo ya mauaji, si kwa ajili ya uzima, bali kwa mateso ya milele”.
Matashi mema kwa wanajeshi wa Urusi na Ukraine
Katika wito wao, kuna hata wazo linalowageukia hata wale ambao wako kwenye mapambano, hasa wanajeshi. Matumaini yao ni kwa ajili ya warusi na waukraine wote ili waweze kurudi kwa haraka katika nyumba na familia zao. Wanaonesha huzuni sana kufikiria giza ambalo watoto wao na watoto wa ndugu zao nchini Urusi na Ukraine wanaweza kujazwa kwa ajili ya kuanza kwa upya kuwa marafiki kwa kuheshi na kupendana. Kwa njia hiyo wanaamini kuwa watu wa Ukraine wanapaswa wawe wa kwanza kuwa na uchaguzi kwa namna huru kwani sio chini ya macho ya bunduki, bila shinikizo kutoka Magharibi au Mashariki.
Wakiwa wanasubiri Dominika ya msamaha, mapadre na mashemasi 233 wa Kanisa Kiordhox nchini Urusi wanakumbuka kuwa milango ya mbinguni itakuwa imefunguliwa kwa wote hata wale wenye dhambi kubwa, ikiwa wataomba msamaha, kwa wale waliowadharau, wanatukana au kuua kwa mikono yao au kwa utashi wao. Hakuna lolote linaolonesha mbadala wa upatanisho wa pamoja. Katika mtashi yao ya kuanza kipindi cha Kwaresima, katika roho ya imani, matumaini na upendo, ujumbe umehitimishwa: “hakuna ombi lisilo la vurugu la kutaka amani na kukomesha vita likataliwe kwa nguvu na kuchukuliwa kuwa ni uvunjaji wa sheria, kwa sababu hii ndiyo amri ya kimungu: Heri wapatanishi”. Kwa hivyo mwaliko wao ni wa mazungumzo, “kwa sababu uwezo wa kumsikiliza mwingine tu unaweza kutoa tumaini la njia ya kutoka kwenye shimo ambalo nchi zetu zimetupwa ndani ya siku chache".