Tafuta

Mahangaiko wa wanawake na watoto wao wakikimbia kujificha na mabomu. Mahangaiko wa wanawake na watoto wao wakikimbia kujificha na mabomu. 

Kampeni ya Wafranciskani Konv.kwa ajili ya kusaidia watu Ukraine

Imezinduliwa Kampeni ya mshikamano iliyoandaliwa na Ndugu wa Wadogo Wakonventuari wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis wa Assisi kwa ajili ya kusaidia Conventi za Kifranciskani zilizoko nchini Ukraine.Katika Nchi ya kivita, wapo ndugu wadogo wanaojitahidi kukaribishwa wakimbizi na kuwasindikiza,lakini watu hao wakiwa hawana lolote.Mshikamano wa dhati ni muhimu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ndugu Wadogo Wafranciskani Wakonventuari(OFM.konv,) wa Konventi Takatifu ya Assisi walioko huko Ukraine wako mstari wa mbele katika kupokea wakimbizi wanaokimbia vita. Kila siku wanakaribisha familia zinazotaabika kukimbia na kuwasindikiza hadi kwenye mpaka na zaidi ya mipaka. Kwa maana hiyo kupitia nyumba mama wanaomba kuwapa mshikamano ndugu hao wa Ukraine kwa kupitia kampeni waliyozindua na inatosha kufanya ishara ndogo ya kutuma ujumbe Sms mfupi au kupiga namba 45515 ili kuweza kusaidia Ndugu Wadogo walioko karibu na watu wanaokimbia vita.

Padre Cesareo akielezea kuhusu Kampeni ya mshikamano kwa ajili ya wakimbizi huko Ukraine

 Sio rahisi kugeuza kisogo mbele ya mateso ya wakimbizi

Kwa mujibu wa msemaji wa Konventi Takatifu ya Assisi, Ndugu Mdogo Giulio Cesareo amebainisha kuwa mbele ya macho ya wote kwa kuona picha za mateso ya kaka na dada nchini Ukraine siyo rahisi kugeuza kisogo upande mwingine. Mtakatifu Francis wa Assisi katika maisha yake na mfano wake aliwaachia urithi mkubwa wa kazi ya kukaa karibu na yule anayeteseka. Kwa niaba yake,hado  ndugu zao wadogo wafranciskani walioko Ukraine  wanajibidisha kila siku katika kutoa faraja ya mateso ya kila anayekimbia vita, kwa sababu upendo na mshikamano ndiyo kweli mwanga wa kushinda ubaya. Katika dharura hiyo ya kibinadamu, zimefungulia njia za moja kwa moja, za haraka na muafaka katika Jumuiya tano za Ndugu wadogo Wakonventuari katika Usimamizi wa  Jumuiya ya Msalaba Mtakatifu nchini Ukraine ili kukaribisha na kusaidia wakimbizi.

Ndugu wadogo wanawasindikiza wakimbizi zaidi ya mipaka

Wakimbizi hawa ni familia hasa wanawake na watoto wao, wakiwa na wazee. Wanahitaji kila kitu kuanzia na chakula, nguo, vifaa vya usafi, afya na sehemu za kuweza kulala kabla ya kuendelea na safari. Katika Conventi nyingine wameweza kutengeneza hata andaki kwa ajili ya kukimbilia kujificha humo, dhidi ya mabomu kwa mujibu wa Ndugu Mdogo Mikola Orach, wa Konventi ya Leopoli huko Ukraine. Kwa mujibu wake amesema wanafanya shughuli ya kuwasindikiza watu kuelekea mipaka salama. Kuna ndugu wadogo  wengine ambo wanawasaidia kuendelea na safari.  Hawa ni kama Taxi za kweli za kifransiskani ambazo zinawakikishia kufika salama kwa wale ambao wanatafuta tumaini  la mbali na mabomu, yaani kwenda zaidi ya mipaka.

15 March 2022, 11:21