Tafuta

Wakimbizi wakisubiri Treni kwenda Poland kupitia Lviv Wakimbizi wakisubiri Treni kwenda Poland kupitia Lviv 

Jumuiya ya Papa Yohane XXIII kujumuika katika kukaribisha huko Lviv

Mamia elfu ya wakimbizi waliofika Lviv wa Ukraine ambao uko kilomita chache kufika mpakanai mwa Poland.Katika eneo hili yupo Alberto Capannini wa Jumuiya ya Mtakatifu Yohane XXIII,ambaye amesema watu wamechoka sana,wanaume wanasindikiza wake na watoto hadi mpakani na kurudi nyuma kwenye mapigano.Ni baridi sana,kuna theluji,sasa ni digrii mbili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Watu elfu kumi wako karibu na kituo, kilomita sabini ikitenganisha Lviv kutoka Poland, digrii mbili za mwisho mkali wa majira ya baridi sana. Lviv kwa siku kadhaa imekuwa jiji la kukaribisha wakimbizi, ambapo maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wa Ukraine wanafika baada ya masaa au siku za kukimbia miji iliyovamiwa na Warusi. Hao wanakimbia kutoka katika mabomu, kutoka katika nyumba zilizoharibiwa, kutoka katika maombolezo, lakini pia kutoka katika njaa na kiu, kama ilivyokuwa kwa Mariupol. Kuanzia Jumatano tarehe 2 Machi 2022 baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Papa Yohane XXIII wamekuwa huko Lviv. Wapo kwa ajili ya kutoa mchango wao kwa wakimbizi, kuelewa kinachotokea, kujenga sio tu ukarimu, bali pia amani. Miongoni mwao ni Alberto Capannini, Mkuu wa Operesheni Colomba, Kikosi cha Amani kisicho na Vurugu cha Jumuiya. Kwa maelezo yake amesema walivyofika tarehe 2 na mara moja walikwenda kwenye kituo cha kati cha jiji ambako watu wamekusanyika. Kwa upande wake amethibisha kuwa  kuna angalau elfu kumi, kati ya wale wa ndani na nje ya kituo. Kuna wanaosubiri treni kwenda Poland. Ni baridi sana, kuna theluji, sasa ni digrii mbili. Watu hawa wanajaribu kufika Poland kwa njia yoyote na baadaye kuendelea na nchi nyingine za Ulaya pia ikiwezekana

Sehemu kubwa ya hawa nwakimbizi ni wanawake na watoto hata kama wanaume ni wengi kwa sababu wanawasindikiza wake zao na watoto mpaka mpakani, na baadaye kurudi nyuma, wakijua kwamba mtu atawachukua wanawake au watoto baada ya kuvuka mpaka kwa miguu, kwenye theluji hiyo. Kuna vituo vya mapokezi nchini Poland. Ukraine ni tupu saa, kuna wale ambao tayari wanasema ya watu milioni ambao wamekwenda mbali. Katika kila nchi, katika kila kijiji katika kilomita hizi 70 zinazotenganisha Lviv na Poland kuna makundi ya watu walio na bunduki, mabomu yaliyotengenezwa papo hapo. Hii inaonesha kwamba kuna hofu ya uvamizi wa Kirusi hata hapo, katika sehemu ya magharibi ya nchi. Umuhimu wa kuwa na wakimbizi hao katika sehemu hiyo amethibitisha kuwa anaamikwamba wengi wao, ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe, wametumia muda mwingi katika maeneo yenye migogoro kwa sababu hakuna kinachoweza kuchukua nafasi ya kuwa huko. Kuona,na kuzungumza na watu. Katika usiku, mahali alipolala, kengele ililia na akashuka kwenye chumba cha chini. Msichana ambaye alitoroka kutoka mbele alimuuuliza ikiwa anatambua kinachotokea,  na jinsi ambavyo  ni muhimu kutowaacha watu wa Kiukreni peke yao.

Kwa kujibu suala kama hili kwamba jibu la Ulaya haliwezi kuwa la kijeshi, yaani, kutoa changamoto kwa mamlaka kama Urusi katika ongezeko la kijeshi. Ni wazi kwamba haikubaliki kwa Urusi kuikalia Ukraine kijeshi, mabomu hayo yanaongezea na kukuza chuki tu. Hakuna mtu ana haki ya kwenda vitani. Jibu la Ulaya lazima liwe tofauti, linaweza kuwa nguvu kuu ya kukaribisha, ya kusimamia migogoro kwa njia ya kidiplomasia. Nyakati hizi ngumu ni zile ambazo utambulisho wa watu hufafanuliwa, nani huteleza, ambaye kwa upande mwingine hufanya kila kitu kujenga amani na ambaye, badala yake, hutumia silaha kuvamia. Anaamini ni muhimu kwamba mataifa ya Ulaya na raia binafsi kuchukua nafasi. Akijibu kuhusu shukrani za papa alizowashukuru watu wa Ukraine kwa makaribisho ya wakimbizi tarehe 2 Machi wakati wa Katekesi yake  na kama  shukrani hizi kwa wale wanaokaribisha huko Lviv tayari wamepumua, kwa asili iliyochanganywa na hofu, maumivu, hasira amesema “Hisia ya kwanza ambayo imeandikwa kwa kukaa hapa, hisia ya kwanza ni kwamba watu waliotoroka ni watu walioangamizwa.

Jamaa mmoja niliyemuuliza alipokimbia akaniambia hajui kuhesabu siku. Yeye hajui kikamilifu kinachotokea, kwa sababu athari za vurugu huharibu. Hisia nyingine ni kwamba tunazungumzia wakimbizi wa Ulaya, ambao wanajua wapi wanatafuta hifadhi, yaani, wanaojua Ulaya. Kuna mshikamano wa kweli, nadhani kukaribishwa ni kwa kila mtu. Tusipokaribisha, tunapoteza ubinadamu wetu. Hapa kuna hali ya kukaribisha, lakini pia ya shida kwa wale wanaokimbia Ukraine labda na hati zisizo za kawaida, watu wanaotoka Afrika au Mashariki ya Kati. Hakika ni wakati mgumu, watu wengi wanatupigia simu kutafuta msaada. Watu wanatafuta ni nani anayeweza kuwakaribisha, labda wafuatiliwe wakimbizi na jamaa na marafiki. Tunafanya kazi sio tu kurekebisha uharibifu uliosababishwa na vita, lakini pia kuhakikisha kuwa vita haipo tena. Haiwezekani kukubali kile kisichostahili na cha aibu”.

04 March 2022, 16:17