Baraza la Makanisa nchini Ukraine limetoa Wito kuomba msaada wa NATO
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kufuatia na mgogoro wa kivita unaondelea, Baraza la Makanisa na Mashirika ya kitawa yametoa taarifa ya pamoja kuhusu mabomu yaliyolenga raia wa Ukraine kwa upande wa wavamizi wa Urusi. Katika taarifa hiyo wanabainisha kwamba tangu kuanza kwa uvamizi mkubwa wa kijeshi wa Urusi katika eneo huru la Ukraine na Urusi, wameshuhudia jinsi wavamizi wa Urusi wanavyotumia njia za kijinga na zilizokatazwa za vita chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Kiukweli, Urusi inapigana vita dhidi ya raia wa Kiukreni na inarusha kwa makusudi makombora ya balestiki, pamoja na kutokea eneo la Belarusi, na kutumia mabomu ya anga ya kijeshi katika vitongoji vya makazi, shule za misingi, shule za chekechea, kliniki za uzazi, hospitali na miundombinu muhimu kwa ajili ya maisha ya raia kwa mambomu ya mkupuo yaliyopigwa marufuku na mabomu ya kulipuka.
Mifano ya wazi ya ukatili usio na msingi na uchokozi usiozuilika wa wavamizi wa Urusi ni ulipuaji wa mabomu kwenye hduma za kibinadamu kibinadamu, Bus kwa ajili ya kuwahamisha watu, na hata ambulensi za kukimbiza wagonjwa. Mtazamo wa dharau wa uongozi wa Urusi kwa maisha ya mwanadamu, ambayo wanaona kwa askari wa Urusi waliotupwa katika kitisho cha vita vya uchokozi, sasa inajidhihirisha kwa raia wa Kiukreni, kulazimishwa kukimbia kutoka katika makombora ya Urusi na wakaazi, kuelekea maeneo salama zaidi ya nchi yetu, nchi jirani na Umoja wa Ulaya, wanabainisha. Zaidi ya hayo, mashambulizi ya kijeshi ya Kirusi dhidi ya Ukraine yanafuatana sio tu na moto na mabomu ya miundombinu na nyumba za raia, lakini pia majengo ya kidini.
Kwa mfano, katika kijiji cha Vyazivka, Mkoa wa Zhytomyr, wavamizi wa Kirusi waliharibu Kanisa la Kuzaliwa kwa mwenye Heri Bikira Maria, lililojengwa mwaka wa 1862. Kufuatia mlipuko wa bomu wa Kirusi wa Kharkiv, kati ya tarehe 2 Machi na Kanisa Kuu la Dormition liliharibiwa. Mnamo tarehe 7 Machi, mabomu ya Urusi yalipiga Kanisa la New Life Evangelical katika jiji la Izyum, Mkoa wa Kharkiv, na jengo la Kanisa hilo likaharibiwa kabisa. Baada ya milipuko hiyo, Kanisa la Kiorthodox katika kijiji cha Zavorychi, wilaya ya Brovary, mkoa wa Kyiv, lilishika moto. Kutoka pande mbalimbali za uvamizi wa Urusi kuna taarifa za kulipuliwa kwa makanisa, yakiwemo yale ambayo wakimbizi wamekimbilia. Hatari ya shambulio hilo pia ilifunuliwa katika sehemu patakatifu kubwa zaidi la kiroho, Katika madhababau ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Sophia huko Kyiv.
Kwa kuzingatia hayo yote, ndipo Baraza la Makanisa na Mashirika ya Kidini ya Ukraine yanatoa wito wake kwa NATO kama mshirika wa usalama wa Ukraine, Umoja wa Mataifa, Shirikisho la Ushirikano wa Kimataifa, Usalama na Maendelea Barazani Ulaya, OSCE na Baraza la Ulaya, kuchukua hatua za haraka ili kuanzisha kile kiitwacho n’o-fly’, yaani hapana kuruka ukanda wa juu wa Ukraine, kuwapa Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vifaa vya kisasa vya ulinzi wa ndege, ikijumuisha ndege za kivita, ili kulinda rasilimali yetu ya thamani zaidi, maisha ya binadamu, kutokana na milipuko ya kinyama ya wavamizi wa Urusi na miundombinu ya kiraia.