Tafuta

2022.03.30:Mkutano Baraza la Maaskofu nchini Amerika Kusini na  Visiwa vya Caribbean (celam). 2022.03.30:Mkutano Baraza la Maaskofu nchini Amerika Kusini na Visiwa vya Caribbean (celam). 

Amerika Kusini(Celam):Sinodi kuhusu upamoja na changamoto za kikanisa

Safari ya umoja wa Kanisa la Amerika Kusini na Visiwa vyake,ndiyo lengo la mkutano pamoja na mashirika mengine ya kikanisa ili kuweza kuzungumzia juu ya maandalizi ya miaka 15 tangu kufanyika mkutano huko Aparecida na changamoto 41 zilizoibuliwa wakati wa mkutano wa mwezi Novemba 2021,kwa matazamio ya Sinodi ya maaskofu 2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (Celam), pamoja na mashirika mengine ya kikanisa ya bara hilo wameitisha mkutano wa kikanisa kwa njia ya Mtandao kwa ajili ya Baraza hilo na  visiwa vya Carribean, tarehe 30 Machi 2022 kwa lengo la kuunganisha mchakato mmoja wa kichungaji wa safari ya kuelekea Sinodi ya Maaskofu na kuhusu  changamoto 41 zilizoibuliwa katika Mkutano wa Kikanisa uliofanyika mnamo tarehe 21-28 Novemba 2021. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Celam, Mkutano huo wa kwanza unapendekeza upyaisho wa kile ambacho kilipyaishwa katika Mkutano wa Kikansa kwa kuongozwa na sala na tafakari kama alivyoeleza Padre Padre David Jasso, mhusika mkuu wa Sekretarieti ya Celam.  Zaidi ya hayo watasheherekea miaka 15 tangu kufanyika Mkutano Mkuu wa Aparecida, kama mojawapo ya kufikia kilele cha Mikutano itakayo fanyika kwenye kanda kuanzia tarehe 13 hadi 31 Mei 2022.

Mapendekezo ya kufanya mang'amuzi ya Kanisa katika bara la Amerika Kusini

Katika mkutano huo wamewaalika wajumbe ,000 wa kikanisa ambao pia waliudhuria mwezi Novemba 2021. Hawa ni: wajumbe wa Baraza la Vituo vyote vya kichungaji vya Celam, Kundi la kutoa tafakari la Kitaalimungu, wahuishaji wa Sinodi Kitaifa, Marais na Makatibu wa Mabaraza ya maaskofu, Mitandao ya Kikanda katika Mchakato wa Kusikiliza. Mwenyekiti wa Celam akitazama upeo wa mchakato wa kichungaji wa Kanisa la Amerika Kusini na visiwa vya Carribiena, huku ikiwa pia na mchakato wa Sinodi na Mkutano wa Kikanda amewakumbusha jukumu la sasa hadi mwezi Aprili 2022 ili kuchukua hatua kama kianzio cha changamoto na miongozo ya kichungaji. Hiyo ni lazima kuifanyia kazi kwa kutoa mapendekezo ya kufanya mang’amuzi ya Kanisa katika bara. 

Mojawapo ya njia ya kiroho katika kipindi cha Kwaresima 

Timu ya tafakari ya Taalimungu kichungaji ya Celam kwa sasa inakusanya michango mbali mbali ya maoni kwa kuifangamanisha katika hati moja. Baadaye katika uwakilishi wa hitimisho utaanza  ambapo pia katika kipindi cha kuanza kuyaweka yote katika matendo ya dhati. Tume mbili za Mkutano wa Kikanisa kwa ajili ya matendo yake na Celam juu ya mchakato wa Sinodi kwa sasa inafanya kazi pamoja na mashirika mengine katika shughuli mbali mbali, mmojawapo ni njia ya kiroho ya Kwaresima ili kusaidia tafakari juu ya uongofu binafsi, kijumuiya na kichungaji katika mtazamo  mkuu wa Sinodi.

Miaka 15 ya Mkutano wa Aparecida na Semina kuhusu utambulisho wa utume wa kichungaji

Katika maandalizi kuhusiana na mwaka wa 15 tangu kufanyika Mkutano Mkuu wa Maaskofu huko Aparecida,  wanatarajia kufanya mikutano kwa njia ya mtandao kwa Kanisa na hatimaye mkutano na ushirikishwaji wa tumaini katika safari ambayo inaendelea. Katika muktadha wa mchakato huo Celam itafanya mkutano maalum mwezi Julai 2022 kwa namna ambayo maaskofu wanaweza kutafakari kwa kina yale matunda ya pamoja na maelekezo ya kichungaji ambayo yatatoa nuru ya michato yote na mipango ya kichungaji ya jumuiya mbali mbali. Hatimaye wanatarajia kuandaa semina moja kuhusu Utambulisho na utume wa kichungaji kama nafasi ya kutafakari ili kuona upeo wa Kanisa katika upyaisho na uundaji wake kwa upya na msingi wa sinodi. Yote hayo ni katika matarajio ya kutimisha hatua ya koara ya Sinodi ya 2023.

30 March 2022, 15:08