Tafuta

Siku ya Watawa duniani 2022 Siku ya Watawa duniani 2022 

Siku ya Watawa Duniani:CLAR,ni kipindi cha kurudisha kitovu cha kiinjili

Ni wakati sasa wa kuhamasisha mahusiano ya kisinodi kwa namna kupaisha jitihada.Ni wakati wa kutembea kwa pamoja wakiwa wadogo kati ya watu na kuwa sababu ya mwendelezo wa kushirikiana na uwajibikaji,kwa kuwa na ushiriki wa wote na kujifunza kuishi kuanzia na ukaribu kwa pande zote.Ameandika Rais wa Shirikisho la Watawa wa Bara la Amerika Kusini na Visiwa vya Caribbean wakati wa kesha la Siku ya Watawa duniani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baraza la Watawa wa kike na kiume wa Bara la Amerika ya Kusini, na visiwa vya Caribbean, katika kesha la Siku ya Watawa ulimwenguni, inayofanyika tarehe 2 Februari, sambamba Siku Kuu ya Kutolewa kwa Bwana Hekaluni, wameandika ujumbe wao kuwa: “Katika wasiwasi wetu wa kinabii tunaona kwa uwazi kuwa ni kipindi cha kutazana vizuri miundo yetu, mashirika na shughuli za mamlaka na kurudisha lengo la kiinjili katika utoaji wa huduma. Mamonaki kike na kiume, watawa wa ndani, kike na kiume, watawa wa  mashirika mengine na  vyama vya kilei vya kitume, tunataka kutoa ushuhuda wa upendo kwa Kristo na kwa wote katika kila nyanja ya maisha ya kikanisa na kijamii. Mtindo wetu  wa maisha ni kutatufa  kuwakilisha tu tiba ya kiroho dhidi ya mabaya ya kipindi cha wakati”

Katika ujumbe wao uliotumwa kwa Shirika la Habari za kimisionari la Fides, watawa hao wanabanisha kwamba wanajikuta wakiishi maisha ya kina kwa wakati uliopo ambao umejazwa na mambo yasiyo na uhakika huku wakitafuta kutoa jibu la maswali mengi yanayowazunguka. Wapo wanazindua na kujifunza mtindo mpya wa kuwa Kanisa, ambalo kwa hakika lina uso wa kisinodi na ambao linawasukuma kurudi katika unabii na ndiyo kanuni pekee ya maisha! Kwa mujibu wa Rais wa chombo hicho cha Kikanisa kinachoongozwa na Sr. Liliana Franco, amesema “ni wakati sasa wa kuhudumia ubinadamu, na kuondoa kila aina ya utumwa. Ni wakati sasa wa kuhamasisha mahusiano ya kisinodi kwa namna ya kuwa na katika kazi zetu”. Bado Sr huyo amesisitiza kwamba ni wakati wa kutembea wao kwa pamoja wakiwa wadogo na watu, kuwa na sababu ya mwendelezo wa kushirikiana na uwajibikaji, kwa kuwa na ushiriki wa wote na kujifunza kuishi kuanzia na  ukaribu kwa pande zote.

Kwa mujibu wa Chombo hiki cha kikanisa (CLAR) cha Bara la Amerika Kusini na Visiwa vya Carribbean, kinabainisha kuwa katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Baraza la Kikanisa wa Amerika ya Kusini, na Visiwa vya Carribien, ulitambua Shirikisho la Baraza la Watawa hao kwamba,  tangu mwanzo linachangia kuunda mtindo ulio bora wa kiakili na kiroho katika  kufanya kazi ya sinodi inayojumuisha Kanisa lao lote.  Utambuzi huo inathibitisha na jitihada zao kwa kuunda hali ya kuhamasisha mazungumzo kati ya maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa  kike na kiume na  wanawake walei wa vyama vya kitume kwa kushirikisha kuunda imani na maendeleo ya kazi za pamoja na juu ya masuala ya maisha, kuwa na moyo mmoja na roho moja inayoelekeza kwa Mungu. Katika matarajio hayo inabaki jitihada za kuhamasisha zaidi na kuunda uongozi mpya hasa kati ya wanawake walei, walio mstari wa mbele kwa niaba ya kiungo cha Kanisa.

Maisha ya kitawa kwa miaka ya mwisho umepitia mchakato wa safari ya kina kwa ajili ya kujitakasa, mungano na utume. Mchakato wa kisinodi kwa maana hiyo unaowaunganisha katika usikivu, katika muungano, katika ushiriki na utume na  ni kwa ajili ya kutajirisha Kanisa kwa fadhila na karama nyingi ili kuweza kutoa katika ulimwengu ule ushuhuda wao wa furaha, kwa kujitoa  kabisa kwa Bwana, wanasisitiza. Kwa kuhitimisha wanabainisha kuwa katika siku kuu ya uwakilishi wa Bwana hekaluni, tunataka kupyaisha shukrani kwa Mungu kwa zawadi ya Maisha ya kitawa, ambayo kwa Roho Mtakatifu alitoa ndani ya Kanisa na ni mwaliko wa kupyaisha jitihada zetu ili kufuata Kristo, mtiifu, fukara  na msafi wa moyo. Kwa njia ya ushuhuda wetu wa Kiilinjil uwepo wa Kristo mwanga wa watu uangaze katika Kanisa na kutoa nuru kwa Ulimwengu”.

Katika fursa ya kutolewa kwa Yesu Hekaluni, sambamba na siku hiyo hiyo ya Watawa, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuongoza ibada ya Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paetro mjini Vatican tarehe 2 Februari Jioni. Mwaka jana 2021, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alifafanua juu ya siku kuu hii kwamba Roho Mtakatifu   leo  hii bado  anatoa kwa wazee wazo na neno la hekima, wao ni sauti msingi kwa sababu inaimba sifa kwa Mungu na kulinda mizizi ya watu. Hiyo inatukumbusha kuwa uzee ni zawadi na babu na bibi na wazee ni peke zilizounganishwa kati ya kizazi ili kuridhisha vijana ule uzoefu wa maisha na imani. Wazee mara nyingi wamesahaliwa utajiri huu wa kulinda mizizi na kuendelezwa. Kwa maana hiyo Papa alitangaza kuanzisha Siku ya Wazee na babu na bibi ambayo inafanyika kwa Kanisa lote kila mwaka ifikapo Dominika ya Nne ya Mwezi Julai, ambayo inakwenda sambamba na Siku kuu ya Mtakatifu Anna na Yohakimu, babu na bibi wa Yesu. Ni muhimu bibi na babu wakutane na wajukuu zao kwa sababu kama asemavyo Nabii Yoeli, babu mbele ya wajukuu wataota ndoto na watakuwa na shauku kubwa na vijana watakuwa na nguvu za wazee na watakwenda mbele kutoa unabii. Kwa njia hiyo siku ya tarehe 2 pia ni siku kuu ya kukutana na babu na wajukuu. Ni  Siku ya Watu Kukutana. Mzee Simeoni na Ana wakiwa wameongozwa na Roho Mtakatifu walimtambua Kristo Yesu kuwa ni Masiha wa Bwana. Mzee Simeoni akamshukuru Mungu kwa utenzi wa sifa, aliyewawezesha kuuona wokovu, nuru na utukufu kwa watu wake Israeli.

01 February 2022, 14:36