Siku ya Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu:Kutazama sura ya Barelli
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Padre Agostino Gemelli (OFM) alikuwa anasema juu yake Armida Barelli kwamba “hakuwa na shaka kwa upya wa roho yake, angavu na uwezo uongozi wake. Alikuwa tayari kuelekeza moyo wake hata juu ya kikwazo. Kwa moyo wa mwanamke, yaani, angavu, na uzazi, aliishi kwa ujasiri mkubwa, akiachana na mifumo ya kijamii ya wakati huo na kutumia fikra ya kike. Mwanamke mwenye uwezo wa kuwaunganisha wanawake wa nyadhifa zote za kijamii, mhamasishaji wa Ukatoliki uliojumuishwa, wa kukaribisha na wa ulimwengu wote, katika wakati wa kihistoria wa kurudi kwa demokrasia na alihimiza kuelewa ni nini kanuni za kijamii za Kanisa ili kutekeleza wajibu wao kama raia. Kwa sababu wanawake ni nguvu nchini Italia alisema. Katika maisha yake, Barelli alijitofautisha kwa malezi ya kiroho, dhamira ya kikanisa, uhamasishaji wa kiutamaduni na hatua za kijamii za wale wote aliokutana nao katika hali halisi tofauti, kwa uangalifu maalum kwa takwimu ya kike.
Siku ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu itaangukia mnamo Mei Mosi 2022
Ndivyo Ujumbe wa Maaskofu wa Italia wanaadilia katika siku ya 98 ya Siku ya Chuo Kikuu Katoliki Italia kwa kuangaza na sura ya mwanzilishi mwenza wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu ambayo itaangukia mnamo Mei Mosi, 2022. Katika historia ya Armida Barelli wanaamasisha mwaliko wa kuhamasisha umoja, na Ukatoliki jumuishi. Katika ujumbe huo wanaandaika kwamba kama Injini wa Chuo Kikuu, aliweza kumshawishi Papa Pio XI, ambaye alikuwa ni muunga mkono mkuu wa Chuo Kikuu kama ilivyokuwa kwa warithi wake wote, kuanzisha rasmi Siku ya Chuo Kikuu ya kila mwaka katika parokia zote za Italia.
Sifa bora za nembo katika kutafuta ukweli na nguvu muhimu
Mtumishi wa Mungu Armida Barelli anawajibika kwa jina la Moyo Mtakatifu, kwa Athenaeum (yaani Taasisi ya Kipapa) iliyokuwa changa kwa Wakatoliki wa Italia, wanaandikia Maaskofu Italia. Kuwekwa kwake Wakfu kunaoonekana kupindukia na kwa hakika unafafanua uhusiano kati ya ibada na tafakari, mpangilio wa mapenzi na mpangilio wa Neno, hatimaye kati ya imani na sababu. Wito wa kuwa taasisi ya elimu na kitamaduni ambayo, kwa kufahamu kikamilifu umoja wa Ukristo, inalenga kuchanganya sifa bora za nembo katika kutafuta ukweli na nguvu muhimu zaidi za upendo zinazolenga uzuri na wema wa maisha.
Shukrani na shauku, yenye uwezo wa kuzalisha utamaduni unaoishi kweli
Kwa mtazamo huo,katika hali ya tishio leo zaidi ya hapo awali la mgawanyiko usioweza kupunguzwa kati ya imani na sababu, jumuiya ya Chuo Kikuu inahitajika kuwa na uwezo wa kufikiri unaokaliwa na shukrani na shauku, yenye uwezo wa kuzalisha utamaduni unaoishi kweli na kwa sababu istahiliyo mwanadamu. Hatimaye, marejeo ya ujumbe kwa njia ya video wa Papa Francisko wakati wa uzinduzi wa mwaka wa kitaaluma wa Chuo Kikuu mnamo tarehe 19 Desemba 2021 katika miaka mia moja ya kuanzishwa kwae na kusisitiza maneno matatu muhimu ya kukuza: “moto, matumaini na huduma”, kwa kufuata mfano wa Barelli, ambaye ni mfano katika kuchanganya maono ya ujasiri, shauku ya elimu na kujitolea kwa kiutamaduni, katika huduma ya upendo kwa Kanisa na kwa jamii.