Poland:wito kwa wakristo wa Urusi na Ukraine kuungana katika sala ya pamoja
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Poland ameandika barua na kutoa wito kwa Maaskofu wa Kiorthodox na Wakatoliki wa Urusi na Ukraine ili kunganisha nguvu za pamoja za kiroho ambazo ziweze hatimaye kushinda mivutano ya vita isitokee tena katika kanda yao. Anawaomba ili kwa waamini wote katika Kristo kila mmoja katika hali yao ya ukristo na ili kanda yao iweze kuendelea na amani. Wito huo umetolewa na Askofu Mkuu Stanisław Gądecki, Rais wa Baraza la Maakofu Poland katika barua na kwamba anawageukia wao kama askofu wa Nchi inayopakana kati ya Ukraine na Urusi. Askofu Mkuu amesisitiza kuwa wao wamekuwa na uhusiano wa kihistoria wa pamoja na imani takatifu ya kikristo. Kwa njia hiyo ni muhimu waunganishe nguvu za sala kiroho na waamini wote katika Kristo na madhehebu mbali mbali ya Urusi, Ukraine na Poland kwa kusali pamoja kwa Yule ambaye ni Bwana wa Amani ili azuie upeo wa vita vingine vya kikanda.
Watu wasio kuwa na hati, hasa walio wadhaifu
Askofu Mkuu Stanisław Gądecki anaandika kwamba nguvu zao za sala ziwe kilio cha kuzuia matendo na vifo vya maelfu ya watu wasio kuwa na hati, hasa walio wadhaifu zaidi na wasio kuwa na mlini ambao hawatakuwa na nguvu na wala fursa za kukimbia kuibuka kwa vita. Rais wa Baraza la Maaskofu Poland wakati wa kuzungumza kwa vyombo vya habari kuhusu hali kubwa ya migogoro ya kisilaha huko Ukraine amesisitiza kuwa kila vita ni janga la kibinadamu na wanaokufa miongoni mwake ni maelfu ya watoto na walio wengi katika sehemu zote wanabaki bila kujulikana. Kuhusiana na balaa la vita kati ya Urusi na Ukraine, amesema linaongezea suala la watu wote kwa sehemu mbili Wakristo na madhehebu mengine.
Vita kwa ujumla haileti suluhisho la matatizo yalisababisha kugombana
Kwa mtazamo wa kibinadamu na hukumu ya Mungu watu hawa wanapaswa wawe na mambo ya pamoja yanayowaunganisha na si kutegemea chuki, lakini kwa kuheshimiana na urafiki wa pamoja. Hali misingi lakini ni ile ya haki za watu, zikiwepo haki za kujikamilisha na ufungamanishwa wa maeneo, amesisitiza Askofu Mkuu Gądecki. Kwa kukumbusha juu ya vita vilivyotokea katika mchakato wa karne iliyopita, amekumbusha hata maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye katika Ujumbe wake wa Siku ya Amani duniani mnamo 2000 aliandika kuwa vita mara nyingi ni sababu ya vita nyingine, kwa sababu inaongeza chuki ya kina na kuunda hali ya ukosefu wa haki, na kukanyaga hadhi na haki za watu. Vita kwa ujumla haileti suluhisho la matatizo yaliyosababisha kugombana na zaidi ni kutishia na uhalibifu, na matokeo yasiyo na maana. “Kila vita ni uwenda wazimu” ameongeza Askofu Mkuu, Gądecki, neno ambalo tayari Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana alisema hivyo.