Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Kaskazini mwa Afrika
Na Angella Rwezaula - Vatican
Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Afrika Kaskazini ulimalizika Jumanne tarehe 15 Februari 2022 ambao ulifanyika huko Algeria, kwa kuanza na tukio kusimikwa kwa Askofu Jean-Paul Vesco kama Askofu Mkuu mpya wa Algiers mnamo Ijumaa tarehe 11 Februari. Katika taarifa yao mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo inabinisha kwamba ilianzia Morocco na Tunisia, majimbo mengine kutoka Algeria na Sicili. Katika tukio la Kusimikwa, Rais na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa aliungana nao kwa muda pamoja na kufanya kazi na Balozi wa Vatican nchini Algeria Askofu Mkuu Kurian Mathew Vayalunkal ambaye alifungua kuandamana na kazi yao yote.
Monasteri ya Tibhirine kwa ajili ya sala
Kwa upande mwingine, wajumbe kutoka Libya na Laayoune hawakuweza kuungana nao. Walifanya kazi nao kwa njia ya video, kama walivyokuwa wakifanya kwa miaka miwili mfululizo. Walifurahi kuwa pamoja na wale walioweza kufanya safari hiyo, baada ya kuzuiwa kukusanyika mahali pamoja tangu mwezi Septemba 2019. Baada ya kushiriki furaha ya Kanisa la Algeria katika Kanisa lake kuu, walikwenda siku iliyofuata kwenye monasteri ya Tibhirine. Katika mahali hapo pa sala, kujitolea na kumbukumbu, walimkabidhi Bwana furaha, mivutano na mateso ya watu wao na nchi zao leo hii. Walikuwa wakifikiria hasa kuhusu nchi ya Libya ambapo Kanisa la Sebha liliharibiwa Jumapili asubuhi tarehe 23 Januari 2022 na wanamgambo na ambapo Tripoli imekuwa na mvutano mkali tena kwa siku chache za hivi karibuni. Lakini pia walikuwa tukifikiria ugumu uliosababishwa hapo na vita, huko na hali ya kisiasa au ya kiuchumi, na kila mahali na janga lililopo.
Kila mtu amekumbwa na janga lililosababishwa na UVIKO- 19
Kwa miaka miwili kiukweli, kama kila mtu mwingine, wamekumbwa na janga lililosababishwa na UVIKO- 19. Baadhi ya jamii zap zimepitia vifo; wote waliteseka kutokana na kutengwa kutokana na hatua za kuzuia (harakati ndogo, kusimamishwa kwa shughuli nyingi, maeneo ya ibada yaliyofungwa, nk). Lakini kipindi hiki kigumu pia kilikuwa fursa ya kupima jinsi walivyounganishwa kwa kila mmoja wao, wanabainisha. Katika ulimwengu ambao unaonekana kuvunjika, virusi hivi vimefanya wote watambue jinsi ubinadamu wetu ni mmoja. Wengi wameelewa udhaifu huu wa kawaida na wameonesha uthabiti, wakipinga kishawishi cha kujibagua, na kujaribu kujiweka katika huduma ya wale walio hatarini zaidi kuliko wao wenyewe, au kuchukua hatua za kuomba pamoja hata wakiwa mbali. Kwa mujibu wa taarifa wanasema “Hatujui janga hili litaisha lini, lakini tunaamini kuwa haliwezi kuwa na neno la mwisho juu yetu na uhusiano wetu”. Katika mienendo ya mchakato wa sinodi unaoendelea, maaskofu hawa walishiriki kwa upana juu ya maisha ya jumuiya zao za Kikristo, misimamo yake, mageuzi yake, pointi zake za kawaida na tofauti zake. Kwa kuhisi kuwa changamoto mbalimbali zitaangaziwa na kwamba mapendekezo na maswali yanaweza kuibuka kutoka katika awamu za majimbo na kikanda za sinodi, na wamejipanga ili kuweza kuzifanyia kazi kwa umakini. Kwa upande wa Kanisa lao la Afrika Kaskazini, kutangazwa kwa Charles de Foucauld kuwa mtakatifu ni fursa ya kushangilia na kuongeza zaidi ufahamu wake: kuigwa kwa imani katika kuwasiliana na waamini wengine, kupendezwa na utamaduni wa wengine, hamu ya udugu wa ulimwengu mzima.
Miaka 150 ya Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Afrika
Kwa maana hiyo waliadhimisha Misa ya Jumapili kwenye Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Afrika, ambayo inaadhimisha miaka mia moja na hamsini mwaka huu 2022. Kama kawaida, kusanyiko hili lilikuwa fursa ya kutembelea baadhi ya jumuiya na kugundua uhalisia na shughuli mbalimbali za Kanisa mahalia. Mkutano huo ulichagua Ofisi mpya kwa miaka mitatu, huku Kadinali Cristóbal López Romero, askofu mkuu wa Rabat kuwa kama rais, Askofu Nicolas Lhernould, askofu wa Constantine na Hippo kama makamu wa rais, Monsinyo George Bugeja, Mmsimamizi Kitume wa Tripoli kama mjumbe na kama nyongineza ya Askofu Mkuu Ilario Antoniazzi, wa Jimbo Kuu la Tunis. Alitoa shukrani zake kwa Ofisi ya zamani iliyokuwepo tangu 2015 na rais wake Askofu Mkuu Paul Desfarges,na kuthibitisha katibu wake. Mkutano huo ulimchagua mmoja wa wajumbe wake na mbadala wake ili kumpendekeza kwa Baba Mtakatifu kumwakilisha katika sinodi ya mnamo Oktoba 2023. Mkutano wao utaendelea kufanya kazi kwa ukawaida kupitia mikutano kwa njia ya video na mkuu watakutana tena baada ya mwaka mmoja.