Tafuta

2020.02.20 Luigi Giussani akiwa na baadhi ya wanafunzi huko Portofino 2020.02.20 Luigi Giussani akiwa na baadhi ya wanafunzi huko Portofino 

Kard.De Donatis:Kumfuata Kristo ni kutii mamlaka ya Kanisa pia mamlaka ya Papa!

Inatazamiwa kuwa vipimo vya maisha na kazi ya Padre Giussani vitaeleweka na kuviishi kwanza kabisa na wale wanaofuata nyayo zake katika harakati za Umoja na Ukombozi.Lakini wataweza kuwa hivyo kwa kadiri kila mmoja atakavyo gundua kupitia kwake,anafikia hata yeye kuwa sadaka ya urafiki na Kristo.Ni ushauri wa Kardinali De Donatis wakati wa mahubiri 20 Februari 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Padre  Giussani alifariki mnamo tarehe 22 Februari 2005. Maelfu ya watu kila upande wa dunia wameweza kufikiwa tangazo la kikristo shukran kwake, ya moja kwa moja au kupitia kwa harakati ya ‘Comunione e Liberazione’ yaani ‘Umoja na Ukombozi’. Kila mwaka majimbo mengi, marafiki wa harakati wanakutanika fursa ya kumbu kumbu ya kifo cha Padre Giussani ili kuadhimisha misa Takatifu na maaskofu wao. Maadhimisho ya mwaka huu, yana maana kubwa. Padre Gussani alizaliwa mnamo tarehe 15 Oktoba 1922. Kwa maana hiyo ni rahisi kufukiria kwamba miezi ijayo, Harakati ya ‘Comunione na Liberazione’ itakuwa na safu za matukio mbali mbali kwa ajili ya kukumbuka mwanzilishi wao akitimiza  miaka 100 ya kuzaliwa kwake. Mipango hii ni ya kuweza kujua vema mantiki mbali mbali za sura ya padre na shughuli za kitume za Padre Giussani. Ni maelezo ya Kardinali Angelo di Donatis, Makamu wa Papa Jimbo la Roma wakati wa maadhimis ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Laterano Roma, Dominika jioni Tarehe 20 Februari 2022, katika fursa ya kufanya kumbu kumbu ya Padre Giussani. Kardinali De Donatis amesema kuwa hii inatutaka kujiuliza ni kitu gani aliwaachia watoto wake kiroho na kwa ujumla kwa Kanisa zima. Itakuwa ni fursa nzuri kwa wote ikiwa kwa yule ambaye hakumjua Padre Giussani aweze kuwa na fursa ya kumjua na yule aliye mjua awe na fursa ya kugundua kwa upya umuhimu hata zaidi ya ule ambao tayari alikuwa anaujua.

Kardinali Angelo De Donatis Makamu wa Papa , Jimbo la Roma
Kardinali Angelo De Donatis Makamu wa Papa , Jimbo la Roma

Kardinali Di Donatis, akianza kujikita na tafakari ya masomo ya siku ya Dominika, yaliyosoma amesema mbele ya macho ya Daudi, Sauli  sio mfalme kama wengine, lakini ni yule aliyewekwa wakfu na Bwana; kwa upande wake, alikuwa na Mahusiano na Bwana kwa sababu ya uchaguzi, mapatano na kuwekwa wakfu.  Na Daud, anasubiri. Hii ina maana kuwa ana utambuzi na kumuheshimu sio tu Sauli, lakini kile ambacho Mungu alifanya kwake. Muktadha wake wa mang’amuzi na hukumu havipo katika kile ambacho Sauli aliweza kufanya, kwa namna ya pekee dhidi yake, lakini ni kwa kile ambacho Bwana alifanya kwa ajili ya Sauli. Ni namna tofauti ya kutazama, ya kuhukumu na kutenda. Si kuhukumu mwingine kwa kile anachofanya, lakini kile ambacho Bwana alitenda kwake. Kile ambacho napaswa kuona kwa mwingine sio tu kile ambacho anatimiza, bali kile ambacho Bwana mwenyewe anatenda kwa ajili yake. Mtume Paulo akiandika kwa Wakorinto, anathibitisha kuwa, “ mtu wa kwanza, Adamu, akiwa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuvuviwa (1Cor 15,45). Kila mwanaume na kila mwanamke, anayetambua katika adamu kuwa asili moja, wanatambua hata tofauti hii  kati ya kwanza na Adamu wa mwisho. Wakati wa kwanza alipokea Roho ambaye ni Baba aliyempa pumzi yake, wa mwisho akawa yeye mwenyewe Roho mtoa uzima.  Roho Mtakatifu alipuliza juu yetu wakati baada ya ufufuko wake, anavuvia juu ya uso wa mitume na kusema “ Pokeeni Roho Mtakatifu (Mt 20,22).

Jumuiya ya Comunione e Liberazione
Jumuiya ya Comunione e Liberazione

Neno ambalo Yohane katika Kigiriki analitumia, kuvuvia ni sawa na neno ambalo Biblia ya kigiriki ya LXX inaendeleza ili kuelezea ishara ambayo Mungu anapuliza kwa  Adamu ili kumfanya awe na uzima (Mw 2,7). Bwana anatupatia Roho wake ambayo ni kwa ajili ya kujipatanisha,  ya msamaha wa dhambi na huruma kuelekeza wadhambi. Kwa upande wa Daudi ilikuwa fumbo la matendo hayo ya Roho Mtakatifu, ambaye anapelekea kumsamehe Sauli  na kumwokoa maisha . Huo ni upendo ambao Bwana anawaalika wafuasi wake na ambao amezungumza leo hii Maneno ya Yesu yanatimilizika kwa wito mkubwa wa kuwa watu wenye huruma kama Baba alivyo na huruma kwetu sisi (Lk 6,36). Mwaliko huko wazi wa kuwa wana wa Baba, na Mwana ambaye hawezi hasifanane na wazazi wake. Maneno hayo ndiyo yamefanya pia kutazama sura sasa ya Padre           Giussani, amebainisha Kardinali De Donatis kwamba mantiki muhimu ya Padre huyo ni mengi mmo lakini cha msingi  kinachovutia kwa kila aliyekutana naye na ambacho kinaendelea kuvuta hata kwa kila akutananaye kwa njia ya maandikio na yale ambayo ameita ukweli wa imani. Kwa upande wake imani haikuwa hakika hisia tu zinazotofautiana, au kuingia kwa ndani ambako kunasukuma jitihada za kiadili na kijamii. Lakini wala sio kukubali mafundisho tu ambaye yanabaki mbali na maisha. Kwa upande wa Padre Giussani anao mtazamo wa kina wa uhalisia wa Kristo, wa wakati wa sasa, wa umoja ambao lazima kujua alionao wa Yesu na ambao Yeye mwenyewe  aliuunda kama ishara yake  (L’attrattiva Gesù, BUR, Milano 1999, p. 148).

“Hakuna kinachoweza kuchukua nafasi ya Kristo. Kupitia matukio ya historia, Kristo anabaki kuwa somo la mpango ambao ni wake pekee. Na Kristo anapojidhihirisha jinsi alivyo, hakuna kinachoonekana kuwa cha kuamua zaidi kuliko uhusiano naye. Padre Giussani alionesha kwa uwazi undani wa uhusiano wake na Kristo: “Kristo ni maisha ya maisha yangu. Ndani yake kunajumlishwa kila kitu ambacho ningependa, kila kitu ninachotafuta, kila kitu ambacho ninajitolea, kila kitu kinachotokea ndani yangu kwa sababu ya upendo kwa watu ambao aliniweka pamoja nao (Kutoa uhai kwa ajili ya kazi ya Mwingine, BUR, Milan 2021, ukurasa wa 63). Kardinali De Donatis amesema msukumo wa kimisionari unaodhihirisha shughuli za Padre Giussani unazaliwa kutokana na uhusiano na Kristo. Mwanamume aliye katika upendo na Kristo anatamani kumjulisha kwa wengine. Wale wanaomjua Kristo, kwa upande mwingine, hawawezi kushindwa kutazama kwa hamu maisha ya watu wanaotafuta kwa njia elfu moja kuwa na furaha na kushindwa. Na, kiukweli, bila Kristo wanadamu hukosa kile kinachotimiza matarajio yao katika nyakati za furaha na kile kinachowapa tumaini wakati inaonekana kwamba hakuna kitu zaidi cha kutumaini.

Utume hauwezi kamwe kuwa juhudi ya pekee kwa Padre Giussani. Kinachofanya tangazo la Kikristo kusadikika kiukweli ni juu ya umoja wote wa waamini. Umoja ambao Padre Giussani anazungumzia ni dhihirisho la utendaji wa Kristo miongoni mwa wanadamu kwa hakika kwa sababu ni jambo ambalo wanadamu pekee hawawezi kamwe kufikia. Binadamu kwa urahisi hujikusanya ili kumpinga mtu. Umoja wa waamini, kwa upande mwingine, haupingani na mtu yeyote. Ni mkubwa kuliko urafiki  wa kila mmoja na pia ni mkubwa kuliko mafanikio ambayo kila mmoja anaweza kuyapata peke yake na pia mafanikio yanayoweza kupatikana kwa pamoja. Kwa upande mwingine, umoja wa waamini ambao Padre Giussani anauzungumzia ni umoja wa “harakati”. Baada ya yote, hivi ndivyo Papa Francisko anatukumbusha anapozungumzia sinodi kwamba waamini hawaunganiki wanapokuwa imara katika imani au nyadhifa zao, bali wanapogundua kwamba wanatembea pamoja katika kumfuata Kristo, amesisitiza Kardinali De Donatis.  Kumfuata Kristo kwa upande wa Padre Giussani kuna hakikisho la mwisho na la uhakika katika kutii mamlaka ya Kanisa na hasa mamlaka ya Papa.

Katika utii ambao Padre Giussani alihubiri na kuishi hakuna kitu cha utumishi, cha rasmi, chenye fursa. Padre Giussani alitii Kanisa kwa sababu alitaka kumtii Kristo na alitambua kwamba uhusiano naye unapitia kwa ukamilifu juu ya uhusiano na wale walio na kazi ya kuliongoza Kanisa lake. Kwa maana hiyo Kardinali amesisitiza kurudi kwenye uhusiano huo na Kristo ambao unafafanua mtu yaani Padre Giussani. Uhusiano huu unakuwa ndani yake msukumo wa kimisionari, shauku inayowaka kwa ajili ya umoja wa waamini, utii huru na usio na masharti kwa Wachungaji wa Kanisa. Inatazamiwa kuwa vipimo vya maisha na kazi ya Padre Giussani vitaeleweka na kuviishi kwanza kabisa na wale wanaofuata nyayo zake katika harakati ya “Comunione e Liberazione” yaani Umoja na Ukombozi’. Lakini wataweza kuwa hivyo tu kwa kadiri  ya kila’ mmoja wao atakavyoweza kugundua kupitia kwa Padre Giussani, jinsi ya kufikia  hata yeye pia  sadaka ya urafiki na Kristo. Kwa maana hyo amehimisha Kardinali kwamba “Uhalisia wa imani uwe hai ndani yetu daima: maisha yanatuweka katika utambuzi mgumu, katika hali nzuri ambamo tunapewa uwezekano wa kutenda mema badala ya mabaya. Kuongoza vigezo vyetu vya hukumu na vitendo ni shauku ya kufanana sana na Kristo”.

20 February 2022, 19:57