Tafuta

2022.02.04 Padre Richard Masivi Kasereka, Padre wa Congo aliuawa tarehe 2 Februari huko Kivu Kaskazini 2022.02.04 Padre Richard Masivi Kasereka, Padre wa Congo aliuawa tarehe 2 Februari huko Kivu Kaskazini 

Mazishi ya Padre Richard Masivi Kasereka,huko kaskazini Kivu,DRC

Jumamosi tarehe 5 Februari,yamefanyika mazishi ya Padre Richard Masivi Kasereka,mtawa wa Congo DRC wa Shirika la Watawa Mapadre Wadogo wajulikanao kama“Caracciolini”, Mtawa huyo aliuawa mnamo tarehe 2 Februari katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Congo DRC na kundi la watu wenye silaha akiwa anarudi kutoka kwenye sherehe ya Siku ya Watawa Ulimwenguni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Padre Richard Masivi Kasereka, Mkongo na washirika la Mapadre Wadogo wajulikanao kama “Caracciolini”, aliyeuawa mnamo tarehe 2 Februari huko Kivu,  Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mazishi yake yamefanyika Jumamosi tarehe 5 Februari 2022. Kwa mujibu wa Shirika hilo katika taarifa yao  katika Shirika la Habari za kimisionari Fides, wamethibitisha kuwa kwa sasa hawana taarifa zaidi zilizo sababisha tukio hilo la mauaji ya ndugu yao zaidi ya zile zilizo tolewa na Jimbo Katoliki la Butembo-Beni.

Katika taarifa  la tukio hilo zilikuwa zinasema: “Kwa uchungu mkubwa, jimbo letu linatangaza kifo cha ghafla cha Padre Richard Masivi Kasereka, ambaye ni mwanashirika wa Shirika la Mapadre Wadogo na paroki wa Parokia ya Mtakatifu Arcangelo ya Kaseghe”. Ujumbe huo ulikuwa ni kutoka kwa Askofu  Melchisédec Sikuli Paluku, wa jimbo katoliki la Butembo-Beni DRC.

Kwa mujibu wa taarifa za kwanza ni kwamba Padre Richard Masivi Kasereka aliuawa tarehe 2 Februari na watu wenye silaha huko Vusesa, kati ya Kirumba na Mighobwe, katika eneo la Lubero(Kaskazini-Kivu), wakati alikuwa anarudi kwenye parokia yake, mara baada ya kuudhuria shereza  za kuadhimisha Siku ya Watawa ulimwenguni huko Kanyaboyonga. Aidha taarifa hiyo ilikuwa inabainisha kwamba wakiwa katika kusubiri matokeo ya uchunguzi unaoendelea, jimbo la  Butembo-Beni linatoa pole kwa mapadre, watu waliowekwa wakfu na walei wa Butembo-Beni, alisema Askofu Sikuli Paluku, ambaye mawazo yake kwa hakika yaliwaendea familia ya damu ya Padre Richard na pia kwa shirika lake na kwa jumuiya nzima ya Kikanisa.

Hata Mkuu wa shirika kwa upande wa Afrika wa Shirika la mapadre Wadogo, Padre Jean-Claude Musubao, alitoa salamu za rambirambi katika ujumbe wake na alikumbuka kuwa Padre Richard alinyakuliwa maishani siku tatu kabla ya kuadhimisha mwaka wake wa  thelathini na tano wa kuzaliwa na ambapo aliongoza Parokia ya Kaseghe kuanzia tarehe 31 Oktoba 2021.

05 February 2022, 14:14