Tafuta

Zaidi ya makatekista 200 katikaKkanisa la  Malaysia wamepyaisha juhudi zao kichungaji Zaidi ya makatekista 200 katikaKkanisa la Malaysia wamepyaisha juhudi zao kichungaji 

Malaysia:zaidi ya makatekista 200 wapyaisha jitihada zao kichungaji!

Padre Paul Lo anawashukuru Makatekista wa Jimbo la Kuala Lumpur kwa huduma yao ya malezi ya imani kwa njia ya mafundisho ya katekesi na kushirikishana Neno la Mungu.Hasa katika nchi ya Malaysia,nchi yenye lugha nyingi na makabila mbalimbali,huduma ya katekesi inaendeshwa na makanisa mbalimbali katika lugha tatu: Bahasa Malaysia,Kichina na Kiingereza.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Jimbo Kuu la Kuala Lumpur, makatekista walei na watu wa kujitolea ni watu wenye thamani sana kwa ajili ya kuhudumia Kanisa mahalia. Zaidi wa makatekista 200 wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu, na Kanisa la Maria Mkingiwa la Kuala Lumpur Walipyaisha jitahada zao kwa kupewa katika daraja dogo la utume wa kichungaji la Katekesta mnamo tarehe 23 Januari 2022, wakati wa Dominika ya Neno la Mungu wakati wa maandhimisho yaMisa takatifu katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu. Ibada iliandaliwa katika Matazamio ya “Dominika ya Katekesita 2022 iliyokwa na Jimbo Kuu kuanzia Dominika ya  tarehe 30 Januari 2022 siku ambayo tangazo la imani na mchakato wa makatekesita ulikuwa inaanza katika Kanisa.  Padre Paul Lo aliwashukuru Makatekista kwa huduma yao ya malezi ya imani kwa njia ya mafundisho ya katekesi na kushirikishana Neno la Mungu. Hasa katika nchi ya Malaysia, nchi yenye lugha nyingi na makabila mbalimbali, huduma ya katekesi inaendeshwa na makanisa mbalimbali katika lugha tatu: Bahasa Malaysia, Kichina na Kiingereza.

Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatoa nyenzo kuu ya kufundisha imani

Padre Paulo Lo alithibitisha kuwa: “Kwa njia ya ubatizo, sisi wana wa Mungu tunakabidhiwa utume wa kueneza Habari Njema ya wokovu na upendo kwa watoto, vijana na wale wote wanaotaka kuungana na Yesu Kristo na Kanisa. Makatekista ni waalimu na wahudumu wa Neno la Mungu kwa ajili ya mema ndani ya Kanisa”, huku akikumbuka kwamba, “Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatoa nyenzo kuu ya kufundisha imani”. Makatekista na watu wakujitolea kwa maana hiyo walipyaisha  kujitolea kwao ili kuingia katika uhusiano wa karibu zaidi na Yesu na kushiriki mafundisho, ushuhuda na kushiriki imani na wengine. Padre Lo alisema:  “Makatekista wakiwa washiriki wa huduma ya kichungaji, wanasaidia waamini, watoto na watu wazima, kwa maneno, matendo na maisha”, na kuendelea  kueleza furaha yake kuona walei wengi wakijitokeza kuhudumu katika huduma ya katekesi. Kwa maana  hiyo aliwasihi kwamba: “tumikieni kwa furaha, kwa maana Bwana mwenyewe atawakirimia  ninyi kwa baraka nyingi”.

Jimbo kuu linakusudia kuandaa siku maalum ya sala na mkutano

Zaidi ya hayo, Jimbo kuu linakusudia kuandaa siku maalum ya sala, mkutano na udugu itakayowekwa wakfu kwa Makatekista tarehe 17 Septemba 2022, katika fursa ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Roberto Bellarmino, mlezi wa makatekista. Ukristo nchini Malaysia ni dini inayofuatwa na asilimia 9.2% ya wakazi (kulingana na sensa ya 2010). Theluthi mbili ya Wakristo wa Malaysia milioni 2.6 wanaishi mashariki mwa Malaysia, inayoundwa na majimbo ya Sabah na Sarawak (kwenye kisiwa kikubwa cha Borneo), ambako wanaunda asilimia 30 ya wakazi.

01 February 2022, 15:14