Tafuta

Hitimisho la Mkutano wa Maaskofu na mameya wa miji ya Kimediteranea uliofanyika huko Firenze 23-27 Februari 2022 Hitimisho la Mkutano wa Maaskofu na mameya wa miji ya Kimediteranea uliofanyika huko Firenze 23-27 Februari 2022 

Kard.Bassetti:Misa ya hitimisho la Mkutano kuhusu Mediteranea

Wazo kwa Ukrane na Giorgio La Pira,aliyekuwa Meya wa Firenze,mwanasiasa na mkristo shuhuda wa udugu,ndiyo yalikuwa mambo muhimu yaliyosikika katika hitimisho la Mkutano wa Mediteranea pia katika mahubiri Kardinali Bassetti raisi wa CEI ameshauri kufanya kazi kwa ajili ya amani ambayo daima inaanzia ndani ya moyo.Ni katika kuhitimisha Mkutano ulioanza 23-27 Februari 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Watu wa Mediterania wawe mashuhuda kwa ulimwengu wote wa amani iwezekanayo, ambayo inaanzia kutoka moyoni iliyogeuzwa kuwa Injili na kutoa maamuzi thabiti kwa manufaa ya wote, Hayo yamesisika kutoka kwa Kadinali Gualtiero Bassetti, askofu mkuu wa Perugia-Città della Pieve na rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), katika Kanisa Kuu la Santa Croce, yaani Msalaba Mtakatifu huko Firenze,  mbele ya Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia, maaskofu 60 na mameya 65, kutoka nchi 20, walioshiriki katika mkutano uliofanyika kuanzia tarehe 23 Februari na ambao umehitimishwa na Misa Takatifu Dominika tarehe 27 Februari. Akitazama sura ya Watu kama vile ya Giorgio La Pira, Kardinali amebainisha kuwa “wamekuwa manabii wa amani katika ulimwengu ambao ulionekana kuzuiwa na mivutano iliyojificha na vita vinavyoendelea. Kardinali amebainisha kwamba hata leo Neno la Mungu linafunua tumaini kwamba kubadilisha ulimwengu kunawezekana, mradi  mioyo ya watu tu ikubali kubadilishwa”. Mediterania, ambayo ni nafasi ya kijiografia ambayo Mwana wa Mungu aliamua kuzaliwa na ambapo Injili yake ilichukua hatua zake za kwanza, iwe sauti kubwa ya ujumbe huu wa udugu, na tumaini la mwisho.  Hata hivyo Kardinali mara moja aliweza kumtakia kupona haraka Papa na kumshukuru sana Mkuu wa Serikali ya Italia kuwapo katikati yao. Katika mahubiri wazo lake limekwenda Ukrane na migogoro inayoendelea ya kuvamiwa na Urusi. Amebainisha juu ya habari zinazofika kutoka Ukrane, na kwamba katika Dominika Neno la Mungu linaangaza kusihi  kila mtu.  Mungu anaomba kwenda moja kwa moja katika moyo wa matatizo na ili kuweza kuona namna ya kuweza kuishi katika dunia iliyo bora zaidi

Maadhimisho ya Misa katika hitimisho la Mkutano wa 'Mediteranea mpaka wa amani'
Maadhimisho ya Misa katika hitimisho la Mkutano wa 'Mediteranea mpaka wa amani'

Akijikita katika  Injili  Kadinali huyo analinganisha tambarare ambayo Yesu anahubiri na Firenze iliyolala kwenye mto Arno, ambako Bwana ameonekana katika siku hizo za Mkutano, ili kusema kwa mara nyingine tena kwao kama wachungaji na wajumbe wote waliohudhuria neno la wokovu. Baadaye Kardinali alijikita kutazama juu ya picha ya Yesu aliyomia kwenye mithali ya mwalimu na mwanafunzi, kibanzii na boriti, na mti na matunda yake. Kwa mujibu wake amesema, nyuma yake kabisa kuna hekima ya Mediterania ambayo wote wanapaswa kujifunza tena ile ya makabiliano ya kuendeleza. Kwa maana hiyo mwaliko wake ni kutojifungia binafsi na kufuata njia iliyochukuliwa huko Firenze, inayojumuisha na udugu. Maneno ya Kardinali yanatiwa alama zaidi pia na uzoefu wa Giorgio La Pira, sura muhimu ya kuigwa mfano, kwa kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kuhamasisha maisha yake na chaguzi zake kwa ajili ya yule Mwana wa Mungu, ambaye alikuja kutumikia na sio kutumikiwa. Njia ambayo imewezesha kuifanya Firenze kuwa jiji lenye uwezo wa kusuka uhusiano wa amani na mataifa yote na kati ya mataifa yote. Nabii wa amani ambaye, kwa Neno la Mungu, anatumaini kwamba mabadiliko ya ulimwengu, ameondoa mivutano iliyojificha na ambaye amewatia moyo manabii wengine wa amani.

Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) pia alibainisha sura ya mti na matunda, akikumbusha kwamba kwa kushinda unafiki kwa msaada wa mwingine, mtu anaweza kubadilisha moyo wake na kupanda mema duniani. Kwa hakika, chuki au udugu huzaliwa moyoni. Kwa njia ya Injili, moyo au mambo ya ndani ya mtu hufikiwa kwa shukrani katika mahusiano na wengine na matendo yetu wenyewe, ambayo yanafanana na sisi. Kwa kuhitimisha mahubiri yake, Kadinali Bassetti anaonyesha tumaini kwa Mediterania, eneo la kijiografia ambalo Mwana wa Mungu aliamua kuzaliwa na ambapo Injili yake ilichukua hatua zake za kwanza, ili iwe eneo kubwa la sauti ya ujumbe huu wa udugu. Watu wa Mediterania wawe mashuhuda wa ulimwengu mzima wa amani iwezekanayo, ambayo inaanzia mioyoni mwao kwa kuongoka kwa njia ya Injili na kuzalisha chaguzi thabiti kwa ajili ya wema wa wote.

Maadhimisho ya Misa katika hitimisho la Mkutano wa 'Mediteranea mpaka wa amani'
Maadhimisho ya Misa katika hitimisho la Mkutano wa 'Mediteranea mpaka wa amani'

Ikumbukwe hata hivyo kwamba Misa ya hitimisho ilikuwa iongozwe na Papa Francisko ambaye kutokana na maumivu ya goti hakuweza kwenda huko. Kardinali Gualtiero Bassetti katika hotuba yake ya utangulizi wakati wa kikao cha pamoja kati ya maaskofu na mameya chenye tabia ya siku ya mwisho wa mkutano huo ambao uliandaliwa na Baraza la maaskofu Italia,  Jumamosi tarehe 26 Februari 2022, akiwa katika Jumba la Kizamani ameelezea kuguswa kwake katika mkutano huo. Kardinali alisema “Zimekuwa siku za kusikilizana, kufahamiana na kushirikishana na ambazo zimefikia kilele cha mkutano wa pamoja. “Ninahisi hisia kali za shukrani ndani yangu kwa uwepo wako katika chumba hiki, kikubwa na muhimu zaidi kutoka kwa mtazamo wa kihistoria-kisanii wa Jengo la Kizamani. Katika mkutano wa Maaskofu 60 wa Mediterania kuna  kama ninavyofikiria katika Mameya  maana ya mali ya kawaida ya Mare Nostrum, ambayo inaweza kuteka uzuri na nguvu ya udugu, lakini pia unabii wa umoja ambao ni asili katika ubinadamu wetu.

Kardinali Gualtiero amethibitisha kuwa  kuna baadhi ya kanuni maalum za kutia moyo katika chimbuko la mkutano wa pili wa Maaskofu, ambao unaitwa kwa mwendelezo wa mpaka wa amani wa Mediterania. "Kiukweli, tangu nilipokutana na meya Mtakatifu wa Firenze Giorgio La Pira, Mediterania imeanza kuzungumza katika moyo wangu. Baadaye  tangazo na pendekezo lilifanywa, na kufikia kilele mnamo 2020 huko Bari, nilipogusa mara ya kwanza kwenye ngozi ya Maaskofu mateso yasiyoweza kuzuilika ya Bahari hiyo, iliyopunguzwa hadi kufika kwa makaburi la maelfu ya dada na kaka. Hivi ndivyo nilivyokumbuka maneno yaliyotamkwa na La Pira kamba: “Bahari ya Mediterania irudi kuwa vile ilivyokuwa”. Kwa njia hiyo upekee wa mkutano wao katika ngazi ya kikanisa, ulikuwa ule wa kueleza njia ya kiinjili ya maisha ya kila siku ya jumuiya wanazoziwakilisha, kutoa sauti kwa matatizo na maswali ya watu wanaopakana na Mediterania, katika wakati ambao ni wa kushangaza kweli. Kwa maana hiyo  Kardinali alisema: “Hatuwezi kushindwa kuangalia mzozo unaoendelea na kueleza wasiwasi na masikitiko yote yanayotokea. Tunakabidhi kwa historia ukurasa ambao hauambii tu tukio, lakini ambao unakuwa ahadi thabiti kwa siku zijazo. Ni kana kwamba historia, yenye herufi kubwa izungumze nasi kuhusu siku za nyuma, ili kutafakari sasa hivi kwa mtazamo wazi juu ya siku zijazo.

Kardinali alisema " Mahali hapa siwezi kukosa kumtaja Giorgio La Pira kwa sababu alisema familia nyingine nyingi waliokuwa wanafika kwenye Jumba la zamani (Palazzo Vecchio) kufichua majanga ya hali zao, hawa walikuwa ni watu maskini waliofukuzwa wakitafuta paa na makazi. na Yeye la Pira anasema:" Je Nilipaswa kufanya nini? Ningeweza kutoka ndani yake kwa kuwaambia waliofukuzwa: Samahani lakini siwezi kufanya chochote kwako. Hoja yangu  ikiwa itabidi nichukue majukumu yangu makubwa kama meya kwa uzito inaweza tu kuwa nyingine: inaweza tu kuwa sababu ya Msamaria, ya kuingilia kati: ambayo ni, lazima nitafute njia zote za kuponya hali ya adhabu ambayo inafanya ucheleweshaji wowote” (La Pira). Kardinali Bassetti ameongeza kusema kuwa haya ni maneno ya kuwajibisha ambayo, tangu zamani, yanafuata njia sahihi sana: kila mmoja wetu, kila mwanamke, kila mwanamume, anaweza kuvutia mwelekeo mpya, hatua ya kugeuza barabara inayosafirishwa kila siku, kujenga iliyo nzuri ya  Pamoja na chaguzi ndogo. Kwa sasa tunaishi masaa makubwa! Pamoja na Maaskofu waliopo Firenze , tulielezea masikitiko yetu kwa hali mbaya ya Ukraine. Tumetoa wito kwa dhamiri za wale walio na majukumu ya kisiasa kufunga silaha zao. Acha wazimu wa vita!

Tunalifahamu vyema janga hili, ndiyo maana tumeomba na tunaendelea kuomba amani. Kila mzozo ni mauaji yasiyo na maana, kama Benedikto XV alivyosema katikati ya Vita vya Kwanza vya Dunia. Vita ya sasa inaweza kuambatanishwa katika neno moja tu ambalo linakuwa ombi: amani! ya wakati ujao. Kwa kukabidhi siku hizi za historia, tunajitoa kuendelea katika mchakato, sio tu ufaao, wa udugu na ujuzi wa utofauti ambao ni utajiri mkubwa lakini kwa uzuri wa picha za mila na tamaduni, zilizokiukwa na mikasa inayowapata watu wetu wengi, na ndiyo ni muhimu kwa  ‘Mare Nostrum’ yaani bahari yetu, kwa mara nyingine tena kuwa njia panda ya historia na tamaduni na sio tena kaburi chungu. Mwanadamu ni kama uwezo wake wa kukutana ambao unalingana na asili yake ya karibu ya kijamii na mpango wa Mungu ambaye, kwa neema yake, anatenda ili wanadamu na watu watunga, kuheshimu tofauti zao zote, umoja wa familia ya kibinadamu”, alisema La Pira . Kwa kuhitimisha Kardinali Bassetti alsema  " basi na tupange mustakabali wetu na matumaini." 

MAHUBIRI NA HOTUBA YA KARD BASSETTI RAIS WA CEI
27 Februari 2022, 16:01