Italia:Ujumbe wa CEI wa Kwaresima 2022:Tusijikabidhi katika majaribu yaliyopita
Na Angella Rwezaula,– Vatican.
Katika Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia, uliochaposhwa Ijumaa tarehe 18 Februari 2022 katika fursa ya kuanza kipindi cha Kwaresima 2022, unajikita kutazama hali halisi ya Kanisa na kijamii kwa ujumla. Maaskofu wanatoa mwaliki wa uongofu wa aina tatu ambao ni wa dharru na muhimu hasa katikahatua hii ya kihisotria kwa namna ya pekee kwa ajili ya Kanisa nchini Italia kwamba wawe na uongofu kwa kusikiliza, kwa ukweli na kiroho, nina shauku moja tu, ya kuwakumbatia babu na bibi yangu tena”. Hata maneno ya vijana vile vile yanafika katika kina cha moyo kusika wanasema “Niko napoteza miaka bora zaidi ya maisha yangu; 'Nilikuwa nimesubiri kwa muda mrefu kuweza kwenda chuo kikuu, lakini sasa kila mara ninajikuta mbele ya kompyuta'”. Sauti za wataalamu, baadaye zinahamasisha kuwa na imani katika sayansi, huku ikibainisha jinsi inavyokosea na kukamilika, vile vile bado tunafikiwa na kilio cha wataalamu wa afya, wanaoomba kusaidiwa juu ya tabia ya uwajibikaji. Hatimaye yanasikika maneno ya baadhi ya mapadre wa parokia pamoja na makatekista na wahudumu wao wa kichungaji, wanaona kupungua kwa idadi ya shughuli na ushiriki wa watu, wakiwa na wasiwasi wa kutoweza kurejea ngazi za awali, lakini wakati huo huo tukijua kuwa hatupaswi kuota ndoto tu ya kurudi kwa kile kinachojulikana kama kawaida” Ujumbe unasomeka.
Kisikiliza ni mtindo wa Yesu na Kanisa linapendekeza kufuata njia hiyo
Baraza la Maaskofu Italia kwa maana hiyo wanaendelea kueleza kuwa kusikiliza kwa kina sauti hizi zote ni nzuri zaidi kwa Kanisa lenyewe. Na kwa jinsi hiyo wanao wanahidi haja ya kujifunza kusikiliza kwa njia ya huruma, kujiuliza kibinafsi kila wakati ndugu anapofungua kwao. Kusikiliza, kwa hakika, kwa hiyo kwanza kabisa humbadilisha msikilizaji, akiepuka hatari ya kiburi na kujirejea mwenyewe. Kanisa linalosikiliza ni Kanisa ambalo pia ni nyeti kwa pumzi ya Roho Mtakatifu. Kusikiliza Neno la Mungu na kusikiliza kaka na dada kunaendana pamoja. Kwa maana hiyo, kusikiliza hata kidogo ni jambo la thamani sana katika Kanisa, kwa sababu linapendekeza tena mtindo wa Yesu, ambaye alisikiliza watoto wadogo, wagonjwa, wanawake, wenye dhambi, maskini na waliotengwa.
Ujinga, hofu na kukosa uvumilivu vinazaliwa kutokana na ubaguzi na kudhania
Ujumbe wa CEI unabainisha kuwa “Tusijikabidhi katika majaribu ya wakati uliopita au wa kungojea siku zijazo kutokea dirisha na hivyo, mwaliko wao ni Utii wa wakati uliopo ambao ni kwa haraka, bila kushindwa na woga wa kupooza, majuto au udanganyifu. Mtazamo wa Mkristo ni ule wa ustahimilivu, wanasisitiza Maasofu na kwamba ustahimilivu huu ni tabia ya kila siku ya Mkristo inayobeba uzito wa historia, binafsi na jumuiya nzima. Katika miezi ya kwanza ya janga waliona kuongezeka kwa ubinadamu, ambapo ulipendelea upendo na udugu. Baadaye msukumo huu wa awali ulipungua polepole, na kutoa nafasi katika uchovu, kutoaminiana, kushindwa, kujifungia ndani binafsi, kulaumiwa kwa mwingine na kutojihusisha. Lakini imani sio fimbo ya viini macho, wanaonya Maaskofu.
Ujinga, woga na kutovumilia magonjwa mabaya
Wakati suluhisho la shida linahitaji safari ndefu, na uvumilivu unahitajika, subira ya Kikristo, ambayo inaepuka njia za mkato rahisi na huturuhusu kubaki thabiti katika kujitolea kwetu kwa faida ya wote na sio kwa faida ya ubinafsi au upendeleo. Kama jumuiya ya Kikristo, na vilevile waamini mmoja, mmoja, ni lazima kuurudisha wakati wa sasa kwa subira na kuendelea kushikamana na uhalisia. Maaskofu wanatoa pendekezo, kwa maana hiyo kwamba wanahisi kazi ya kikanisa ya kuelimisha watu ukweli kwamba ni ya dharura, kusaidia kuziba pengo, kati ya ukweli na mtazamo potofu wa ukweli. Chembe chembe za ujinga, woga na kutovumilia hujificha katika 'pengo' hili kati ya ukweli na mtazamo wake. Lakini huu ndio ukweli ambao wanasema wamepewa na kwamba wameitwa kupenda kwa uvumilivu. Kutokana na hivyo ndipo wanaomba kujibidisha kusoma kwa uzito na uhuru wa akili na kubeba kwa uvumilivu kwa kujua kuwa kuna matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa kwa muda mfupi na kwa juhudi kidogo.
Mchakato wa sinodi unafanya kukomaa mtindo mpya wa kusikiliza uhalisia
Mchakato wa Sinodi umepevuka katika Makanisa nchini Italia kwa namna mpya ya kusikiliza ukweli ili kuuhukumu kwa njia ya kiroho na kuzalisha chaguzi zaidi za Kiinjili. Unabianisha Ujumbe wa CEI na kwamba Roho si mgeni katika historia kwani wakati inaweka mizizi katika wakati uliopo sasa, inasukuma kuibadilisha kuwa bora zaidi. Kwa Mkristo huu sio wakati tu uliowekwa na vizuizi kwa sababu ya janga hili, badala yake ni wakati wa Roho, wakati wa utimilifu, kwa sababu una fursa za upendo wa ubunifu ambao hakuna enzi zozote za kihistoria zilikiwa zimewakilishwa, Maaskofu wanaandika: Labda hatuna uhuru wa kutosha wa moyo wa kutambua fursa hizi za upendo, kwa sababu tunazuiliwa na woga au kuathiriwa na matarajio yasiyo ya kweli, wa uchunguzi wa dhamiri. Wakati Roho, kwa upande mwingine, anaendelea kufanya kazi kama siku zote. Roho anauliza mwamini kuzingatia leo hii tena katika ufunguo wa Pasaka, kama Yesu alivyoshuhudia, na si kama ulimwengu unavyoona, wanakumbusha maaskofu katika ujumbe wao. Kwa mfuasi kushindwa kunaweza kuwa ushindi, kupoteza ushindi. Kuanza kuishi Pasaka, ambayo inatungojea mwishoni mwa Kwaresima, inamaanisha kuzingatia historia kutokana na mtazamo wa upendo, hata ikiwa hii inahusisha kubeba msalaba wake mwenyewe na wa wengine.