Caritas Italia na Pembe ya Afrika:dharura zaidi ni vita na ukame
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Katika kesha la Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels kwa mkutano wa kilele unaojikita kujadili ushirikiano na mataifa ya Ulaya mashariki tarehe 17 na18 Februari 2022, Caritas Italia imeunganisha miito ya Makanisa Mahalia, Ya Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa ili serikali ziweze kutenda kwa hara kujibu mahitaji ya watu ambao wanahitaji msaada wa lazima. Dola bilioni 1.5 zinahitajika ili kukabiliana na mzozo huo, sawa na takriban elfu 1 ya matumizi ya kijeshi ya kila mwaka ya ulimwengu. Hadi sasa ni asilimia 2.3 tu ndiyo iliyoahidiwa na wafadhili. Na kwa bahati mbaya, licha ya maombi ya mara kwa mara ya Papa Francisko, ambaye pia hivi karibuni alisisitiza kwamba kwa mwaka bila kutengeneza silaha kutakuwa na chakula na elimu kwa ulimwengu wote, vita vinaongezeka.
Sera za kisiasa zishughulikie migogoro ya Tigray na Somalia
Kwa maana huyo ni dharura zaidi na lazima kutenda kwa haraka juu ya sababu za kina zinazoweza kupelekea mwisho wa vita huko Tigray na kuruhusu bila vizingiti vyovyote vya kufika na mgawanyo wa msaada kwa watu; inahitaji zaidi ya hayo, matendo ya dhati ya sera za kisiasa na umoja unaogeukia kumaliza mgogoro wa Somalia, jitihada za wote katika mapambano ya tabianchi na msaada wa kuimarisha mifumo ya chakula endelevu na ustahimilivu wa wakazi wa eneo hilo katika muda wa kati.
Mchanganyiko wa migogoro na ukame mkali na viwango vya nguvu
Hakuna wakati wa kupoteza barua hiyo inasisitiza. Mchanganyiko wa migogoro na ukame mkali na viwango vya nguvu ambavyo havijawahi kurekodiwa tangu 1981, vinasababisha moja ya migogoro mbaya zaidi ya chakula katika miaka 10 iliyopita. Hali ni sawa na ile ya 2011 wakati mwitikio wa polepole wa ulimwengu kwa shida ulisababisha vifo vya zaidi ya 250,000 kutokana na njaa na athari zinazohusiana, nusu yao wakiwa chini ya umri wa miaka 6. Tayari kuna watu milioni 20 walio katika hali ya uhaba mkubwa wa chakula ambao wana hatari ya janga ikiwa hakuna hatua madhubuti na ya haraka.
Vifo na upotevu wa mamia elfu ya mifugo,kupanda kwa bei ya mazao ya chakula
Msimu wa tatu mfululizo wa mvua chache mwishoni mwa 2021 ulisababisha hasara kubwa ya mazao na mifugo katika maeneo ya mashambani ya kusini na kusini mashariki mwa Ethiopia, Somalia, na mashariki na kaskazini mwa Kenya. Msimu wa nne wa mvua za chini ya wastani unatarajiwa kati ya mwezi Machi na Mei 2022. Vifo na upotevu wa mamia ya maelfu ya mifugo, kupanda kwa bei ya mazao ya chakula na mahitaji ya chini ya kazi za kilimo kunapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kaya wa kujikimu kimaisha, angalau hadi katikati ya mwaka. 2022.
Watu milioni 9 wanaohitaji msaada wa kibinadamu,Tigray,Amhara na Afar
Vita vya kaskazini mwa Ethiopia katika eneo la Tigray, Amhara na Afar kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kikanda ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu Novemba 2020 tayari vimesababisha, pamoja na waathirika wa ghasia, maelfu ya vifo vya njaa, watu milioni 4 waliokimbia makazi. Watu milioni 9 wanaohitaji msaada wa kibinadamu kwa kiasi kidogo iwezekanavyo kutokana na vita na vikwazo vya upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Hali inayoendelea sasa ya ukosefu wa utulivu, ukosefu wa usalama na migogoro ya ndani nchini Somalia na migogoro ya ndani ya Sudan Kusini na Sudan (Darfur na Kordofan Kusini) inazidisha athari za ukame na kuongeza idadi ya watu waliokimbia makazi na uhaba wa chakula.
Ushirikiano wa Caritas Italia na kuwasiliana mara kwa mara na Caritas za nchi
Caritas Italia inawasiliana mara kwa mara na Caritas ya nchi zilizoathirika na hasa katika Ethiopia, Sudan Kusini, Somalia na Kenya ili kukabiliana na mgogoro huo. Nchini Ethiopia, mpango mpya wa msaada umezinduliwa kusaidia wakazi wa kaskazini ambao ni wahanga wa mzozo wa Tigray na wale wa kusini na mashariki ambao ni wahanga wa ukame. Nchini Kenya, uingiliaji kati unaendelea katika eneo la pwani na hatua zinazowezekana kaskazini zinatathminiwa.