Tafuta

2022.02.16 Hii ndiyo Nembo Mpya ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika Kusini na Visiwa vya Caribbean(CELAM) 2022.02.16 Hii ndiyo Nembo Mpya ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika Kusini na Visiwa vya Caribbean(CELAM) 

Maaskofu wa CELAM wawakilisha nembo mpya ya muhimili wao!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu na Caribbean(Celam) wamewakilisha nembo mpya ya mhuhili wao ikiwa na fimbo ya kichungaji,msalaba na ramani ya bara zima ndani mwake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika kwenda sambamba na mchakato wa upyaisho na uundaji kwa upya ambao Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (Celam) wako wanapeleka mbele, tarehe 15 Februari 2022,  Nembo mpya ya muhimili huo wa kikanisa imeanza kutumika rasmi. Nembo imezaliwa na ambayo inawakilisha uwepo wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbean (Celam). Katika nembo hiyo wametumia rangi, tabia na ishara zinazoonekana wazi zenye maana maalum kwao: Fimbo ya Kichungaji kama kitovu kinachowakilisha maaskofu; msalaba ambao unawakilisha Ukristo na shughuli zake za uinjilishaji wa Kanisa; na ramani ya Bara la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbean, nafasi za kimisionari kwa ajili ya uundaji wake wa Kikanisa.

Fimbo ya kichungaji na msalaba vimefungamanishwa

Katika nembo hiyo fimbo ya kichungaji na msalaba vinafungamana kama kitu kimoja ambacho kinaunganisha ndani mwake kwenye eneo na kwa kufungamanisha uwazi na mwendelezo wake wa kikanisa. Kwa namna hiyo uongozi wa kichungaji wa Kanisa Katoliki unaeleza katika mchakato wa safari ya uinjilishi  na katika matendo ya kichungaji ambayo inawezekana kabisa kuwa ndani ya utamadunisho wa Injili katika “bara la Matumaini na matarajio ya sinodi”. 

Muungano wa mbingu na dunia, usawa kati ya shughuli zake

Msalaba pia unawakilisha sehemu kuu nne, muungano wa mbingu na dunia, usawa kati ya shughuli zake lakini uvivu, pia ni uwakilishi wa Ukristo. Fimbo ya kichungaji ni ishara ya mamlaka, lakini juu ya mamlaka yote kama huduma ya kusimamia haki, mabadiliko na inawakilisha wito wa kichungaji wa maaskofu. Ramani ya Amerika ya Kusini na Caribbean inaashiria eneo la kumbukumbu la wamisionari wa Amerika ya Kusini na visiwa vyake (Celam). Mtindo wake unawasiliana na nguvu kubwa ya kikanisa, ufunguzi wazi na muungano katika Kanisa linalotaka kutoka nje kutangaza Injili.

18 February 2022, 12:27