Wasi wasi maaskofu wa Ulaya kwa ajili amani ya Ulaya na kwingineko!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Katika taarifa zilizotolewa zenye wasiwasi wa maaskofu wa Umoja wa Ulaya kutokana na mivutano inayoendelea mipakani mwa Mashariki mwa Umoja wa Ulaya zinabainisha kuwa: “ uthibitisho na matendo ambayo sasa yanawakilisha tishio, ambalo si tu kwa ajili ya Ukraine lakini pia kwa kuweka hatari hata ya amani ya bara zaima la Ulaya na kwingineko”.
Kwa mujibu wa Kardinali Jean-Claude Hollerich, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu ya Jumuiya za Umoja wa Ulaya katika taarifa iliyotolewa tarehe 26 Januari 2022 anasema kwamba nguvu za kijeshi zinazovamia na kuendeleza vurugu za migogoro zinaweza kuharibu Ulaya kwa miaka mingi ijayo. Kama walivyo kuwa wamebainisha hata maaskofu wa Poland, kuhusiana na nguvu za uzoefu wa kizazi kilichopita, maaskofu hofu wanatoa wito kwa wakuu wa serikali ili waweze kuacha vita na kwa sababu vita daima ni kushindwa kwa ubinadamu.
Kwa kufanya kama mwangwi wa maneno ya Papa Francisko, Maaskofu wote wa Ulaya wanawaalika sehemu zote ili kuweka pembeni maslahi binafsi, kuacha kuhamasisha mizozo na badala yake kuongeza imani kwa kutafuta wakati huo huo suluhisho la amani na kusaidia mgogoro unaoendelea ili mazungumzo ya wazi yaweze kuwapo yenye misingi ya haki kimataifa. Maaskofu aidha wanashauri jumuiya ya kimataifa pamoja na ya Umoja wa Ulaya, kupyaisha jitihada zao kwa ajili ya amani na kuchangia uhai wote katika jitihada hizi za mazungumzo, bila kuonesha nguvu na kuongeza silaha, badala yake kutafuta njia za ubunifu wa kufanya michakato ya amani na jihudi zenye misingi ya thamani adili. Hata hivyo Maaskofu Barani Ulaya wanakaribisha tangazo la hivi karibuni la Tume ya Ulaya la kutoa kifurushi kipya cha usaidizi wa kifedha cha Euro bilioni 1.2 kwa ajili ya Ukraine na kutoa wito wa kupitishwa na kutekelezwa kwa haraka kwa manufaa ya watu wa Ukraine.